Msaada, namna ya kurekebisha jina la awali lifanane na la kwenye NIDA

Liutenant

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
590
899
Salamu wakuu

Naomba msaada wa kufahamishwa namna ya kurekebisha jina kwenye kitambulisho changu kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii.

Yaani ni kwamba jina langu la kwenye NIDA lile la katikati ni tofauti na lililopo kwenye mfumo wa nssf.

Hayo majina yametofautiana lakini yote ni majina ya baba yangu na yapo kwenye cheti cha kuzaliwa lakini nssf wamegoma kutambua hilo.

Ni utaratibu gani unatumika kurekebisha hili?

Asanteni
 
Mtafute mwanasheria upate didi pol...

Gharama kama laki hivi ina tegemea na mwanasheria... Na efd lisiti ikiwa utaitaji...

Tafuta mwanasheria, wapo wengi au fika mahakama iliyo karibu nawe waku saidie, ila sio kila mahakama... Tafuta mahakama yenye ubize ukikutana na kalani ana ongea anacho elewa, au ambayo utakutana na mawakili wakiwa ktk shughuli zao za kusaidia raia
 
Mkuu nenda kwenye ofisi za ardhi mkoani kwako ndiyo wanaruhusiwa kisheria kurekebisha majina ya raia wa TZ. Watakujazisha fomu zinaitwa deed pol halafu utaweka picha yako na kutoa malipo ya Tsh 32,000/=.Baada ya hapo fomu hizo utazipeleka kwa wakili/ mahakama zisainiwe halafu unazirudisha ofisi za Ardhi ili upewe hati yenye majina yako yaliyorekebishwa.Hati hiyo utaiwasilisha huko NSSF ili warekebishe utambulisho wako.Ahsante.
 
Mkuu kwa mimi ambaye jina nalotumia toka naanza shule jina la mwisho sio langu waliniandikisha kimakosa na nataka nibadili nafanyaje ?
 
Deed Poll Ni nini?

Ni nyaraka ya kisheria inayotumika kubadilisha jina la mtu. Nyaraka hii hua inasainiwa na mtu ambaye anabadilisha jina pekee tofauti na nyaraka nyingine za kisheria ambazo zinasainiwa na watu wawili mfano Mikataba. Nyaraka hii kwa kawaida inashuhudiwa na kamishna wa viapo ambae ni hakimu au wakili.

Kwa nini Ubadilishe Jina?

Kisheria huwa ni halali mtu kubadilisha jina. Na baadhi ya sababu za kubadilisha jina zinaweza zikawa kama ifuatavyo:

1. Ndoa-Mtu ameolewa anataka achukue jina la mwisho la mke au mume wake.

2. Dini- Mtu amebadilisha dini ikapelekea kubadilisha jina lake.

3. Ulikua unatumia majina matatu mfano Jua Kali Halishi ukataka utumie majina mawili tu Jua Halishi

4. Kuna mkanganyiko wa majina kwenye nyaraka zako za kudumu mfano jina la kwenye cheti cha kuzaliwa ni tofauti na la kwenye cheti cha shule.

5. Nakadhalika.

Ufanyeje ili mabadilisho yako ya jina yatambulike kisheria?

Unatakiwa uwape(ule kiapo) kwa kutumia deed poll (nyaraka ya kubadilishia jina). Hivyo basi fika kwa hakimu au wakili yoyote ataandaa nyaraka hii kwa kumpa taarifa zako mwisho utatia sahihi yako na wakili au hakimu atashuhudia na kugonga muhuri wake kwenye deed poll aliyoiandaa kwa ajili yako.

Baada ya kupata deed poll ufanyaje?

Kwa mujibu wa sheria, deed poll inatakiwa isajiliwe na msajili wa nyara
ka ili iwe halali na uweze kuitumia sehemu mbalimbali mfano kwenye maombi ya passport, kuomba mkopo, kazi, mafao ya kustaafu nk. Hivyo Basi baada ya kupata deed poll yako unatakiwa uipeleke kwa msajili wa nyaraka (registrar of documents) ili iweze kusajiliwa na kutambulika katika matumizi mbalimbali.
 
Registration of Tittle

1.1 Utangulizi

Ofisi ya Usajili wa Hati inatekeleza majukumu yake chini ya Sheria ya Usajili wa Ardhi, Sura Namba 334 (The Land Registration Act, Cap.334). Sheria ya Usajili wa Nyaraka Sura Namba 117 (The Registration of Documents Act, Cap.117), Sheria ya Usajili wa Mali zinazohamishika Sura Namba 210 (The Chattels Transfer Act, Cap. 210), Sheria ya umiliki wa sehemu ya Jengo (Unit Title Act No 17/2008).

Katika kuhakikisha utekelezaji wa majukumu hayo ofisi ya Usajili wa Hati ipo katika kanda nane za usajili katika mikoa ya Dodoma, Mwanza, Moshi, Mtwara, Mbeya, Tabora, Dar es Salaam na Morogoro.

2.1 Majukumu

Kusajili Hati na Nyaraka kulingana na sheria husika kama ifuatavyo;-

2.1.1 Chini Ya Sheria Ya Usajiliwa Hati Sura Na.334

(i) Hati za kumiliki ardhi (Certificate of Title);

(ii) Milki zilizouzwa (transfers);

(iii) Mikataba ya upangishaji;

(iv) Miliki zilizowekwa rehani (Mortgages) ;

(v) Rehani zilizomaliza deni (Discharge and Releases) ;

(vi) Nyaraka za kuwekesha Hati (Notice of Deposit);

(vii) Nyaraka za kuwekesha Hati zilizoondolewa (Withdrawal of Notice of Deposit);

(viii) Hati za marejesho ya miliki na miliki zilizofutwa (Surrender and Revocation);

(ix) Hati nyinginezo:-

o Maombi ya kuandikishwa wasimamizi wa Mirathi;

o Maombi ya kuandikishwa warithi wa marehemu;

o Mabadiliko ya majina ya wamiliki wa Hati za Kampuni au mashirika mbalimbali;

o Marekebisho ya Hati zilizoandikishwa kwa makosa (Rectification).

(x) Uhamishaji wa miliki unaotokana na maamuzi ya Bunge au sheria mbalimbali (Transmission by Operation of Law).

(xi) Nyaraka za Tahadhari na Vizuizi (Caveats & Injuctions).

(xii) Kutoa taarifa za upekuzi wa Daftari la Hati (Search reports).

(xiii) Utwaaji wa Ardhi (Aquisition of right of occupancy)

(xiv) Maombi ya hati mpya ( replacing lost certificates and mutilated )

(xv) Kusajili renewal of right of occupancy

(xvi) Application by adverse possession

(xvii) Application by survivor of joint tenants

(xviii) Deeds of variation & charges

(xix) Kutoa ushahidi mahakamani na kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu kesi zinazohusu usajili wa Hati na nyaraka mbalimbali

(xx) Kusajili Partition/Division of parcels

2.1.2 Chini ya Sheria ya Usajili wa Nyaraka (Sura 117)

(a) Nyaraka ambazo ni lazima zisajiliwe (Compulsory Registration

Uhamisho/mauzo ya nyumba/mashamba ambayo yana barua ya toleo;

o Mikataba ya upangishaji;

o Rehani;

o Ufutaji wa rehani zilizolipiwa;

o Barua za toleo zilizotolewa kwa maeneo ambayo hayajapimwa (Offer of Right of Occupancy) ;

o

(b) Nyaraka za Hiari (Optional Registration):

o Nyaraka zinazotoa mamlaka (Power of Attorney) ;

o Mabadiliko ya jina (Deed Poll) ;

o Nyaraka za uteuzi (Deed of Appointment) ;

o Nyaraka za maelewano (Memorandum of Understanding)

Wosia (Will);

o Mikataba ya Mauzo (Agreements for Sale);

o Barua za utoaji wa mali (Letter of Hypothecation of Goods)

o Hati ya dhamana (Indemnity Bonds) ;

o Mikataba ya kuingia ubia (Partnership Deeds) ;

o Mkataba wa kutoa huduma za kitaaluma ( Professional Service Contracts)

o Taarifa za upekuzi (Search Reports) na

o Nyaraka nyinginezo kama:

Ø Mikataba ya makabidhiano;

Ø Maombi ya kuvunja ubia;

Ø Viapo;

Ø Mikataba ya ukopeshaji;

Ø Makubaliano ya kuondoa madai;

Ø Mikataba ya kuwekesha Hati;

Ø Vizuizi;

Ø Mikataba ya ajira;

2.1.3 Chini ya Sheria ya Usajili wa Rehani za Mali Zinazohamishika (Chattels Transfer Act) Sura Na.210

Rehani zinazohamishika ambazo dhamana zake ni mali zinazohamishika kama magari, ndege, boti, pikipiki, vyomba vya nyumbani mashine za aina mbalimbali, samani na kadhalika. Rehani hizo husajiliwa katika kitengo cha usajili.

2.1.4 Chini ya Sheria ya Umiliki wa Sehemu ya Majengo (Unit Title Act Na. 17

Chini ya sheria hii miliki ya sehemu ya jengo au majengo husajili na kutolewa kwa mmiliki. Sheria hii imeweka masharti yanayopaswa kufuatwa na wamiliki wanaomiliki sehemu ya jengokwa ujumla wao. Pamoja na majukumu tajwa hapo juu kitengo kinahusika na kutunza hati na nyaraka zote zinazosajiliwa pamoja na kutoa taarifa za umkiliki pale inapohitajika.
 
Mkuu nenda kwenye ofisi za ardhi mkoani kwako ndiyo wanaruhusiwa kisheria kurekebisha majina ya raia wa TZ. Watakujazisha fomu zinaitwa deed pol halafu utaweka picha yako na kutoa malipo ya Tsh 32,000/=.Baada ya hapo fomu hizo utazipeleka kwa wakili/ mahakama zisainiwe halafu unazirudisha ofisi za Ardhi ili upewe hati yenye majina yako yaliyorekebishwa.Hati hiyo utaiwasilisha huko NSSF ili warekebishe utambulisho wako.Ahsante.
FUATA UTARATIBU HUU. Ila ni Vema Uanze kwa Mwanasheria.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu nenda kwenye ofisi za ardhi mkoani kwako ndiyo wanaruhusiwa kisheria kurekebisha majina ya raia wa TZ. Watakujazisha fomu zinaitwa deed pol halafu utaweka picha yako na kutoa malipo ya Tsh 32,000/=.Baada ya hapo fomu hizo utazipeleka kwa wakili/ mahakama zisainiwe halafu unazirudisha ofisi za Ardhi ili upewe hati yenye majina yako yaliyorekebishwa.Hati hiyo utaiwasilisha huko NSSF ili warekebishe utambulisho wako.Ahsante.
Asante mkuu.
 
Deed Poll Ni nini?

Ni nyaraka ya kisheria inayotumika kubadilisha jina la mtu. Nyaraka hii hua inasainiwa na mtu ambaye anabadilisha jina pekee tofauti na nyaraka nyingine za kisheria ambazo zinasainiwa na watu wawili mfano Mikataba. Nyaraka hii kwa kawaida inashuhudiwa na kamishna wa viapo ambae ni hakimu au wakili.

Kwa nini Ubadilishe Jina?

Kisheria huwa ni halali mtu kubadilisha jina. Na baadhi ya sababu za kubadilisha jina zinaweza zikawa kama ifuatavyo:

1. Ndoa-Mtu ameolewa anataka achukue jina la mwisho la mke au mume wake.

2. Dini- Mtu amebadilisha dini ikapelekea kubadilisha jina lake.

3. Ulikua unatumia majina matatu mfano Jua Kali Halishi ukataka utumie majina mawili tu Jua Halishi

4. Kuna mkanganyiko wa majina kwenye nyaraka zako za kudumu mfano jina la kwenye cheti cha kuzaliwa ni tofauti na la kwenye cheti cha shule.

5. Nakadhalika.

Ufanyeje ili mabadilisho yako ya jina yatambulike kisheria?

Unatakiwa uwape(ule kiapo) kwa kutumia deed poll (nyaraka ya kubadilishia jina). Hivyo basi fika kwa hakimu au wakili yoyote ataandaa nyaraka hii kwa kumpa taarifa zako mwisho utatia sahihi yako na wakili au hakimu atashuhudia na kugonga muhuri wake kwenye deed poll aliyoiandaa kwa ajili yako.

Baada ya kupata deed poll ufanyaje?

Kwa mujibu wa sheria, deed poll inatakiwa isajiliwe na msajili wa nyara
ka ili iwe halali na uweze kuitumia sehemu mbalimbali mfano kwenye maombi ya passport, kuomba mkopo, kazi, mafao ya kustaafu nk. Hivyo Basi baada ya kupata deed poll yako unatakiwa uipeleke kwa msajili wa nyaraka (registrar of documents) ili iweze kusajiliwa na kutambulika katika matumizi mbalimbali.
Asante sana mkuu, nitafanya hivi.
 
hivi ni kwanini ofsi za ardhi?? why ardhi na sio Rita nk
Hata mimi nimeshangaa.. na zaidi, majina tayari yapo kwenye cheti cha kuzaliwa lakini bado natakiwa nikayasajili.. serikali iko so disorganised. Inatoa document lakini hazitambuliki kwao wenyewe.
 
Salamu wakuu

Naomba msaada wa kufahamishwa namna ya kurekebisha jina kwenye kitambulisho changu kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii.

Yaani ni kwamba jina langu la kwenye NIDA lile la katikati ni tofauti na lililopo kwenye mfumo wa nssf.

Hayo majina yametofautiana lakini yote ni majina ya baba yangu na yapo kwenye cheti cha kuzaliwa lakini nssf wamegoma kutambua hilo.

Ni utaratibu gani unatumika kurekebisha hili?

Asanteni
Nenda mahama yoyote ukabadili nadhani gharama haizidi TSH 10,000/=
 
Mambo yanabadilika, imekuwa laki tena!
Mimi kwenye cheti cha kuzaliwa jina lilikosewa. nilipofika form 2 nilienda Mahakamani nikabadili kwa 7,000 tu yaani buku 7 na hakimu alinipa na risiti kabisa.
 
Deed Poll Ni nini?

Ni nyaraka ya kisheria inayotumika kubadilisha jina la mtu. Nyaraka hii hua inasainiwa na mtu ambaye anabadilisha jina pekee tofauti na nyaraka nyingine za kisheria ambazo zinasainiwa na watu wawili mfano Mikataba. Nyaraka hii kwa kawaida inashuhudiwa na kamishna wa viapo ambae ni hakimu au wakili.

Kwa nini Ubadilishe Jina?

Kisheria huwa ni halali mtu kubadilisha jina. Na baadhi ya sababu za kubadilisha jina zinaweza zikawa kama ifuatavyo:

1. Ndoa-Mtu ameolewa anataka achukue jina la mwisho la mke au mume wake.

2. Dini- Mtu amebadilisha dini ikapelekea kubadilisha jina lake.

3. Ulikua unatumia majina matatu mfano Jua Kali Halishi ukataka utumie majina mawili tu Jua Halishi

4. Kuna mkanganyiko wa majina kwenye nyaraka zako za kudumu mfano jina la kwenye cheti cha kuzaliwa ni tofauti na la kwenye cheti cha shule.

5. Nakadhalika.

Ufanyeje ili mabadilisho yako ya jina yatambulike kisheria?

Unatakiwa uwape(ule kiapo) kwa kutumia deed poll (nyaraka ya kubadilishia jina). Hivyo basi fika kwa hakimu au wakili yoyote ataandaa nyaraka hii kwa kumpa taarifa zako mwisho utatia sahihi yako na wakili au hakimu atashuhudia na kugonga muhuri wake kwenye deed poll aliyoiandaa kwa ajili yako.

Baada ya kupata deed poll ufanyaje?

Kwa mujibu wa sheria, deed poll inatakiwa isajiliwe na msajili wa nyara
ka ili iwe halali na uweze kuitumia sehemu mbalimbali mfano kwenye maombi ya passport, kuomba mkopo, kazi, mafao ya kustaafu nk. Hivyo Basi baada ya kupata deed poll yako unatakiwa uipeleke kwa msajili wa nyaraka (registrar of documents) ili iweze kusajiliwa na kutambulika katika matumizi mbalimbali.
Hivi kuna uwezekano mtu kubadili tarehe ya kuzaliwa kama ilikosewa kwenye mojawapo ya vitambulisho?
 
Sehemu sahihi Ni mahakama yoyote,ofisi ya sheria na SI Vinginevyo
NIDA walikosea wenyewe jina badala ya kuandika JOYCE RICHARD SHIMWETA waliandika RICHARD JOYCE SHIMWETA je na hiyo unaenda mahakamani? saidia mkuu.
 
Back
Top Bottom