Msaada: Namna ya kupambana na sumu ya nyoka ukiwa pekee yako sehemu ambayo hakuna huduma ya kwanza

fisitembo

Senior Member
Jun 19, 2020
123
250
Nimekulia kwenye maeneo ya joto yanayopaka na mito na milima,kulikuwa na nyoka wengi sana,ilikuwa kawaida nyoka kuingia ndani wanafata panya. Kama mlisafiri siku mnapoludi ilikuwa haturuhusiwi kuingia ndani,ilikuwa inabidi kuchoma mipira ndani ya Nyumba ikiwa na maana nyoka akisikia harufu anakimbia. Tulifundishwa hata kujua sehemu zenye majoka makubwa,ukiona uko polini sehemu inanukia wali kimbia hiyo ni hatali,na ukiona vindege vinarukaruka juu ya mti na kupiga kelele jua kunanyoka anakula mayai ya ndege. Kuna nyoka anapaa anakuja kukugonga utosini unakufu.Babu zetu wakati wanachunga Ng'ombe walikuwa wanabeba jiko la mkaa kichwani na uji unaochemka ili yule nyoka akikulukia anaungua,anaweza kugonga hata N'gombe kumi kwa mkupuo wakafa.Nimeshashuhudia vifo vingi Vya nyoka.Ingawa asilimia kubwa ya nyoka ni waoga sana akikuona atakimbia au atakutemea mate na mate yao yana sumu
 

kikokotoo kipya

JF-Expert Member
Dec 18, 2018
404
500
Mdau mmoja ameongelea mkaa,hiyo ni kweli,saga mkaa halafu kunywa, kisha chukua huo unga wa mkaa ulowanishe halafu weka kwenye kitambaa chepesi kama leso kisha chanja sehemu ulipoumwa halafu kunja kile kitambaa mkaa uwe ndani ya kitambaa,baada ya hapo funga sehemu yenye ule mkaa usawa wa sehemu ulipo umwa.
Pia chimba chini kidogo kisha chukua udongo kutoka sehemu ulipochimba,kisha lowanisha huo udongo,weka kwenye kitambaa baada ya hapo fuata maelekezo niliyotoa kuhusu namna ya kutumia mkaa.Vitu vidogo kama nyuki chukua kitunguu maji kikate halafu sugua sehemu ulipo umwa utajionea matokeo.
 

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,723
2,000
Jamani wadau,

Mimi ni mmoja ya watu wanaoogopa sana nyoka na nimekuwa nikijiuliza hivi ikitokea mtu yuko porini mwenyewe na hakuna uwezekano wa kupata msaada wowote ule halafu akakutana na ajali ya kung'atwa na nyoka mwenye sumu kali nifanyeje ili sumu hio isinidhuru na nimekua nikisikia kuwa sumu husambaa sana mwilini ukianza kukimbia, ukiwa na pressure, pia hurusiwi kufunga mguu kwa juu ili uzuie sumu kusambaa.

Msaada wadau maana bado napata shida sana namna ya kupambana na sumu ya nyoka.
Hali ni mbaya sana. Niko eneo tukio hapa Rhotia mbele kidogo na madukani ila ajabu mpaka sasa hivi hakuna vyombo vya kuweza kunyanyua lile gari. Toka saa kumi na moja watu wanalia ndani ya gari. Tuzidi kuwaombea maana naona wengi bado wako ndani ya gari. Hali sio nzuri. Barabara imefungwa so kama uko mto mbunau karatu baki hapo hapo. Wito wangunkwa kamati yabulinzi nanusalama ya wilaya wajaribu hata kuomba Tanesco watumie winchi wao kugeuza gari waokoe watu. Naona sasa askari wanaanza kufukuza maana sio mtu mwenye maamuzi muhimu hapa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom