Msaada: Namna ya kuondoa harufu mbaya kwenye unga wa Soya uliochanganywa na mahindi

Rwaz

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,960
3,310
JF ndio kisima cha maarifa.

Katika kujiandalia lishe bora ya ugali nimechanganya kg 10 za mahindi na kg 3 za soya. Nilianza kwa kuchemsha soya na kuzianika siku 2.

Tatizo unga umetoka na harufu mbaya sana, naiondoaje jamani? Wakati huu wa dunia ya kula kwa sababu na malengo soya ni kitu muhimu bila kusahau utafiti umethibitisha unga wa mahindi kuliwa peke yake unadumaza akili.
 
Mkuu, Unaonaje kama ukichemshia viungo vya chai au vya mboga kila utakapokuwa unakoroga uji ama kuandaa ugali?

Ni mtazamo wangu tu huo, Sina suluhisho hapo katika hitaji lako.
 
JF ndio kisima cha maarifa.

Katika kujiandalia lishe bora ya ugali nimechanganya kg 10 za mahindi na kg 3 za soya. Nilianza kwa kuchemsha soya na kuzianika siku 2.

Tatizo unga umetoka na harufu mbaya sana, naiondoaje jamani? Wakati huu wa dunia ya kula kwa sababu na malengo soya ni kitu muhimu bila kusahau utafiti umethibitisha unga wa mahindi kuliwa peke yake unadumaza akili.
Inawezekana ulivyochemsha soya haikuiva na process ya kupika ugali sidhani kama inatosha kufanya hiyo soya kuiva vizuri ikawa ndio chanzo cha harufu mbaya(ubichi)

Jaribu kuongeza kiasi cha unga wa mahindi ili kiasi cha mahindi kiwe kikubwa zaidi mfano kilo 10:1

Kama Ni mpenzi wa ugali na unajali afya yako Kuna vyanzo Bora vya unga wa ugali vilivyo Bora zaidi ya mahindi ambayo kwa Sasa yanalimwa kibiashara zaidi.

Mimi hua nachanganya mtama, uwele na ngano ya kuotesha kidoogo napata ugali wenye ladha maridhawa sana
 
Inawezekana ulivyochemsha soya haikuiva na process ya kupika ugali sidhani kama inatosha kufanya hiyo soya kuiva vizuri ikawa ndio chanzo cha harufu mbaya(ubichi)

Jaribu kuongeza kiasi cha unga wa mahindi ili kiasi cha mahindi kiwe kikubwa zaidi mfano kilo 10:1

Kama Ni mpenzi wa ugali na unajali afya yako Kuna vyanzo Bora vya unga wa ugali vilivyo Bora zaidi ya mahindi ambayo kwa Sasa yanalimwa kibiashara zaidi.

Mimi hua nachanganya mtama, uwele na ngano ya kuotesha kidoogo napata ugali wenye ladha maridhawa dana
Mkuu, Gnaber Uwiano wa mchanganyiko kati ya MAHINDI, NGANO, UWELE, MTAMA huwa ukoje kwako?

Ni aina ipi ya NGANO unayotumia?
Hiyo NGANO unayotumia ikoje?

Imekobolewa?
NGANO hiyo inapatikana wapi na bei zake zikoje?
 
Ratio zangu zinaendaga kwa kiasi sawa cha mtama na uwele Kisha ngano naweka Kiasi tuu yaani kwa kilo 10 za unga natumia uwele kilo 4.5 mtama kilo 4.5 na ngano kilo 1, inakua ni ngano nzima ambayo haijakobolewa.
 
Shukrani sana mkuu
 
Wakat mwingine kabla ya kuchanyanga soya kwenye mchanganyiko kwa ajili ya kusaga ikaange Kwanza.
 
Back
Top Bottom