Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,005
- 20,303
andamana kama wale vijana 800, yatafika.Habari za usiku wapendwa katika bwana.
Leo nimepatwa na ajali iliyosababishwa na dereva wa JW aliyekuwa akiendesha gari aina ya hiace ndogo ivi yenye namba 1834 maeneo ya Ofisi za jiji Mwanza.
Nikiwa natokea maeneo ya maji haouse nikiendesha ki TVS changu, nilipofika yalipomataa pale maeneo ya jiji ghafla gari hiyo ili ni overtake upande wangu wa kulia kisha ikakata kona ya ghafla ili kuelekea maeneo ya seketure.
Gari iliniparamia ubavuni na kupelekea kuanguka pembeni, Nikiwa pale chini dereva wa gari husika aliliondoa kwa kasi kiasi cha kusababisha kuendelea kunisukuma zaidi.
Kwavile sikuwa na mwendo mkali sikuumia sana zaidi ya kupata maumivu mguu wa kulia na hii imesababishwa na vile alivyonipush akitokea upande wangu wa kulia, pia pikipiki imepata hitirafu kidogo.
Dereva wa gari husika hakutamka chochote pia hakushuka ndani ya gari, aliendelea na safari yake.
Naomba kufahamu ni vipi nitatoa malalamiko yangu kuhusu hili tukio ili ndugu zetu hawa wawe na nidhamu wanapokuwa barabarani, niende polisi au niende kambini kwao maeneo ya Airport.