Msaada: Namna ya kuandaa mbegu za maboga kwa ajili ya uji wa mzazi

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
17,172
34,277
Assalam alayqum,

Jamani ni matumaini yangu mko salama. Naombeni kujuzwa/ kufahamishwa namna ya kuandaa mbegu za maboga zichanganywe kwenye uji wa mzazi. Nazifanyaje baada ya kuziosha?

Je, nazianika nizikaange kidogo ndipo nisage unga wake nichanganyie kwenye uji au nizioshe nianike nikasage straight bila kuzikaanga. Ni ipi njia sahihi?

Asanteni.
 
1. Peta na ondoa uchafu
2. Osha vizuri hakikisha michanga na uchafu wote unatoka
3. Anika juani zikauke vizuri
4. Kaanga kwa moto mdogo, zitakuwa zinanukia vizuri ila uwe makini usiunguze
5. nenda kasage mashineni,
6. Beba na mahindi yako masafi ili yaking'ang'ania mashineni unaweka mahindi yako kusafisha mashine hiyo, beba unga wako na mahindi yenye mchanganyiko wa mbegu za maboga.
 
pia kama una blender ya kusagia vitu vikavyu unaweza sagia tu,
 
Asante mkuu nilikua nishasaga unga wa lishe sema sikua najua namna ya kuandaa hizo mbegu ili maziwa yawe mengi niligugo nikapata taarifa asante mno kwan nishafanya ulivyoeleza na matokeo si mabaya alhamdulillah
1. Peta na ondoa uchafu
2. Osha vizuri hakikisha michanga na uchafu wote unatoka
3. Anika juani zikauke vizuri
4. Kaanga kwa moto mdogo, zitakuwa zinanukia vizuri ila uwe makini usiunguze
5. nenda kasage mashineni,
6. Beba na mahindi yako masafi ili yaking'ang'ania mashineni unaweka mahindi yako kusafisha mashine hiyo, beba unga wako na mahindi yenye mchanganyiko wa mbegu za maboga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom