Msaada: Namna gani viongozi hawa watamfikia rais wa nchi?

kambagasa

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
2,067
2,000
Ndugu zangu jana nilipata wageni saba (viongozi wa serikali za mitaa) wakitaka mazungumzo ya faraga na mimi. Naomba nisitaje maeneo wanayotoka kwa sababu maalumu lakini baada ya kuwasikiliza kwa makini hata mimi nimeamua kuwasaidia kwa njia hii baada ya kuwaambia sina uzoefu na sijawahi kuwaza jambo kama hili.

Ndugu zangu pasipo kujali vyama vyetu vya siasa kama walivyokuja wao (UKAWA na CCM) wameomba niwasaidie namna watakavyopata nafasi ya kumuona raisi wa nchi hii Mh. Dr. John Pombe Magufuli ikulu Dar es salaam au popote atakapokuwa baada ya jitihada zao za kupatiwa ufumbuzi ngazi ya wilaya kukwama (kuahidiwa pasipo kutekelezewa).

Jumla yao wako kumi na saba (17) na kiini cha ombi lao ni kwenda kumweleza raisi wakiwa na ushahidi uliokamilika namna viongozi wa Kitanzania walioko MGODINI.............. wanavyowakandamiza jamii ya eneo la mgodi huo kwa kutoa rushwa kubwa kubwa kwa baadhi ya viongozi wa wilaya pia wakiingiza makampuni yao mgodini pasipo kuisaidia jamii hata vyumba vya madarasa. Wamewataja mameneja wakuu na makampuni yao (sitawataja hapa) na namna ambavyo wamekuwa wanawakomoa wananchi mara tu raisi alipotoa tamko la kuyataka makampuni yanayochimba dhahabu nchini kuinufaisha jamii INAYOZUNGUKA mgodi na makampuni madogomadogo yaliyoko katika migodi yatokane na jamii inayozunguka migodi hii.

Wenyeviti walienda mbali sana kwa kutoa mifano ambayo ina uhalisia wa wazi. Mmoja wao alisema hata wafanyakazi wanaoajiliwa mgodini asilimia 90% hawatoki maeneo ya vijiji hivi isipokuwa huletwa kwa kujuana, ukabila na rushwa kulingana na kazi unayoomba na mshahara wake na kazi hii huratibiwa kwa umakini na kitengo cha HR.
Ndugu zangu nikiyaandika yote hapa waliyonipatia kwa kopi ambayo wameiandaa kumpa raisi nafahamu sitakuwa salama maana wametaja hadi kampuni moja ina uhusiano na mke kati ya maraisi wetu waliostaafu wakishirikiana na mbuge mmoja mwenye makazi yake Dar ambapo kazi ya kampuni hii hata wao jamii wanaweza kuifanya kwa kuingia makubaliano na kampuni yenye utaalamu huo maana vifaa vyote viko hapo mgodini na ni bure.
 
stickvibration

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
3,210
2,000
Wangeanza kwa mkuu wa wilaya wao,ingependeza zaidi
Kwasasa wafanyakazi wote wa serikalini wanawajibika saana na kazi zao ipasavyo wakiwa maofisini mwao
Sio kama zama zile wakikua wakicheza lelemama maofisini
 
Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
9,963

umeambiwa ngazi ya wilaya imeshindikana.

ila mtoa mada jambo ninalo liona sio hao wazee eti ni namna gani watampata raisi ila amesha fikisha ujumbe wa kile alichotaka kusema kwa namna tofauti.

kama nia ni kuwasaidia hao kumi na saba basi njia atakua anazifshamu vyema maana hao wazee wasenge muendea ili awasaidie yeye ni nani hasa?
 
Mkuu katika maelezo yao na namna ninavyowafahamu hao mameneja wa Kitanzania walioko mgodini na Ukwasi wao kukuziba mdomo ni dakika sifuri. Niliwaambia waanze na ngazi ya wilaya kabla ya kukimbilia juu wakaniambia wameshafika na wakaomba awaombee appointment hata ya dakika 30 kipindi alichokuja CHATO na akaenda UGANDA lakini hawakupewa mrejesho. Nikifukua makaburi hapa uzi huu utafungwa sasa hivi
 
Kwanini usifufue makaburi??kwani humu kina dosari gani,,!!!hayo mambo ndio tubayoyataka sasa
Mwaga razi mkuu,,
 
kitomilamkijeje

Senior Member
Apr 26, 2017
135
250
Waende kwa mkuu wa Mkoa ,au mkuu mmoja wapo wa vyombo vya dola Mkoa au Wilaya kama hata huko hawataki, ni majungu!
 
king suleman

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
1,681
2,000
Rais Huwa Ana Angalia Sana Taarifa Ya Habari Kama Watapenda Swala Lao Lisiwe Nyeti Wapeleke Uko Vinginevyo Waanzie Kwa Dc Ingawa Itachukua Mda Na Watuhumiwa Watakua Washagutuka Na Kulekebisha Ma File Kabla Hawajafikiwa Na Mkono Wa Chuma
 
Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
9,064
2,000
Kwanini usifufue makaburi??kwani humu kina dosari gani,,!!!hayo mambo ndio tubayoyataka sasa
Mwaga razi mkuu,,
Hata mimi namshangaa, kampuni hiyo anayoficha kwa haraka haraka ni kampuni ya AKO (Anna Mk... na mbuge Koka) waliifanyia figisu kampuni ya SODEXHO ikapigwa chini na kuingia wababe wa rushwa. Aisee kwa kweli wasukuma tuna laana kwa kigezo cha upole (ndohotabu) laiti mgodi huu ambao hutaki kuutaja ungekuwa kwa Wakurya dharau za kina Kastila zisingekuwepo. Ngoja nimalize kula nije kuyafukua makaburi kama wewe unaogopa
 
stickvibration

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
3,210
2,000
Hata mimi namshangaa, kampuni hiyo anayoficha kwa haraka haraka ni kampuni ya AKO (Anna Mk... na mbuge Koka) waliifanyia figisu kampuni ya SODEXHO ikapigwa chini na kuingia wababe wa rushwa. Aisee kwa kweli wasukuma tuna laana kwa kigezo cha upole (ndohotabu) laiti mgodi huu ambao hutaki kuutaja ungekuwa kwa Wakurya dharau za kina Kastila zisingekuwepo. Ngoja nimalize kula nije kuyafukua makaburi kama wewe unaogopa

kweli mkuu
 
tozi25

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,043
2,000
Hao madiwani waseme wanataka kujiuzulu na kujiunga na ccm. Ndani ya masaa 48 watapata kuonana na Magu na hapo ndio watapata kuelezea kilicho wapeleka.
 
Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
9,064
2,000
Hao madiwani waseme wanataka kujiuzulu na kujiunga na ccm. Ndani ya masaa 48 watapata kuonana na Magu na hapo ndio watapata kuelezea kilicho wapeleka.
Unamawazo hasi kabisa mkuu
Jamaa amesema viongozi serikali za mitaa (vijiji)
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom