Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

kebi

Member
Jan 13, 2012
19
5
Duka la rejareja.jpg

Naomba kufahamishwa kwa mwenye kujua duka la rejareja la kuuza mchele, juice na kadhalika linaweza kuitaji mtaji kiasi gani

Ibravo post:
Habari zenu Wana JamiiForums,

Mimi ni mwanafunzi wa chuo mwaka wa tatu,katika harakati za kujiandaa na kupambana na maisha pindi nitakapohitimu elimu yangu na kurudi mtaani, nimetafuta pesa ikiwa kama mtaji wa biashara milioni moja (1,000,000)hasa ya duka la bidhaa za vyakula.

Tatizo ni kwamba si mzoefu katika biashara na ni mara ya kwanza kutaka kuifanya hii biashara kwan matarajio yangu ni kujiajiri mwenyewe.

Naomba ushauri kwa yeyote mwenye uelewa kuhusu hili kunipa mchanganuo wa bidhaa muhimu zinazotakiwa kuwepo dukani kama vile unga kiasi gani,mchele n.k kulingana na mtaji huo wa Milioni Moja.

Natanguliza Shukrani zangu.

BAADHI YA MASWALI YA WADAU WENGINE KUHUSU BIASHARA HII
Wadau naomba kama kuna mtu anafanya biashara ya duka la rejareja kwenye makazi ya watu anisaidie list ya bidhaa dukani nikahemee. Nataka kufungua duka la rejareja mtaani kwangu nimeshaandaa fremu na mambo mingine kilichobaki ni kuchukua mzigo.

Unisaidie bidhaa zinazotoka sana dukani. Najua maeneo yanatofautiana ila kwa makazi yetu watu wa wastani na kawaida nadhani mahitaji yetu yanafanana. Duka nalifungua maeneo ya kibamba. Nimetenga milioni 5 ya mzigo na nitashukuru kama utanisaidie na bei za jumla za kuchukua mzigo ili nijue nichukue kiasi gani na mahali unapochukulia pia.

Natambua taarifa ni mali, hivyo nimetenga elfu 40 kwa atakaenisaidia hili. Ni PM. I will pay you seriously. Nahitaji anaefanya biashara hii tafadhali.

NB supplier wa unga na mchele nishampata
Sina uzoefu sana wa biashara ila nimepambana, nimefungua duka la rejareja eneo ambalo ni karibu na chuo, kwa hiyo wateja wetu wengi asilimia 90% ni wanachuo.

Natambua mawazo yanatofautiana, ujuzi unatofautiana lakini pia kila siku tunajifunza maana maarifa hayana mwisho. ombi langu kwenu nahitaji ushauri wa bidha ambazo naweza nikaziongezea kwa duka langu au kiti kingine ambacho naweza nikakiongeza dukani kutokana na mazingira (location) ya duka niliyoyataja kikanipa faida.naamini kwa mawazo yenu pengine nitapata mwanga (wazo jipya) ambao sikulifikiria.

Bado naendelea na utafiti binafsi kutokana na mazingira lakini naamini mawazo yenu yanaweza fungua upeo wangu zaidi juu ya biashara.

Nb.duka ni la rejareja, lina vitu muhimu vya majumbani kama vile mchele, vinywaji kasoro bia na sigara (siweki vilevi), sabuni, unga n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi ni kijana umri miaka 23 nina aidia ya kufungua duka la vyakula rejareja maeneo ya kigambon ila sina uzoefu na biashara na nikiazio kipi cha mkwanja wa kuazia hadi sasa nina 60,0000.

NAOMBA MSAADA KWA WENYE UZOEFU NA BIASHARA.
Wakuu,

Natarajia kuwa na duka kwa mara ya kwanza, duka ni la bidhaa za matumizi nyumbani mfano chumvi, sukari, dawa ya meno n.k.

Kwakweli sijui namna bora ya kujua hesabu ya bidhaa zilizouzwa na zile zilizobaki dukani, ukizingatia nitaweka mfanyakazi.

Naomba wazoefu mnisaidie mambo ya kufanya ili angalau mahesabu ya bidhaa dukani yadhibitiwe vizuri.

Karibuni nyote na ahsanteni!
Habari wanaJF,

Naomba kujua kutoka kwa wazoefu na wajuvi wa mambo hayaaa. Nahitaji kujua namna ya kurekod/ kutrak/kufuatilia au kujua faida na hasara katika duka la rejareja hasa unapokuwa na wateja wengi.

Asanteni


MAONI MBALIMBALI KUHUSU BIASHARA HII

Vitu vya msingi kuzingatia
1. Location
Angalia sehemu utaweka hiyo biashara yako kuna watu wa aina/kipato gani hii itakusaidia hata kujua ni bidhaa za aina gani uweke dukani

2. Usimamizi
Nani atakuwa dukani full time
Nani atafanya manunuzi
Nani atakeep records/files zile muhimu 6 ambazo ni:

1.File la mauzo
2.File la Manunuzi
3.File la Gharama za uendeshaji
4.File la Bank
5.File la TRA
6.File la Mikataba/Mengineyo

3. Mahusiano/Mawasiliano
Ili ufanikiwe lazima uwe na Mawasiliano na Kauli nzuri na wateja au jamii inayokuzunguka
Ukiwa na mahusiano mazuri kwa Upande wa suppliers unaweza pata hata bidhaa on credit

4. Timing
Nature ya biashara hizi zinahitajika kila saa hivyo UKICHELEWA kufunga na UKIWAHI kufungua una nafasi kubwa ya kufanikiwa. Timing vile vile inahusiana na ununuzi wa baadhi ya bidhaa ambazo ni za msimu Ukiziwahi waweza hata kuzinunua kwa half price.

Thank You
Zingatia kufanya hivi
  • Hakikisha unanunua bidhaa kidogokidogo kwa kwa kila item.
  • Weka bidhaa ambazo hazitakusumbua sana kuuza kwa eneo lako, mfano. Juice, Maji, Unga, mafuta Kula, sabuni etc, bidhaa ambazo ni mahitaji ya lazima.
  • Weka vocha kwa huvutia wateja. Biashara hii inalipa sana kama utajituma na kuwa na nidhamu ya matumizi.
  • Bidhaa inayo uliziwa Sana na dukani haipo hakikisha unaandika Kisha uininue.
  • Survey maduka ya jirani Kujua bei na baadhi ya bidhaa ambazo hawana we uziweke japo kidogo.

MAHITAJI (ABC's)
Nitakupa ABC kwa biashara unayoiwaza sema waweza kuchanganua na kuamua kuongeza mtaji kwa njia nyingine.

MAHITAJI
1. Cheti cha Vipimo toka kwa Daktari anayetambulika na serikali
2. TFDA certificate cost ~70,000/-
3. Tin number toka TRA na Clearance certificate pia kadirio la kodi si chini ya (360,000+ kwa miezi mi3)
4. Kodi ya nyumba si chini ya 50,000/- kwa mwezi

Kumbuka kuna ununuzi wa mizani, friji (optional) na kupiga mbao za kuoneshea bidhaa kama frame haina hivyo vitu.
Namna bora ya kufanya hesabu dukani

Unahitaji vitabu (nunua hata counter books) vya kumbukumbu za hesabu kama vile:

KITABU CHA MATUMIZI
KITABU CHA MANUNUZI, KITABU CHA MAUZO
KITABU CHA MADENI - kwa unaowadai na wanaokudai
KITABU CHA MALI YA BIASHARA, KITABU CHA STOCK.

Vilevile unahitaji kununua mafaili ya kutunzia stakabadhi za manunuzi, malipo, bank slips, mikataba, na nyinginezo ktk mpangilio kila moja na faili lake.

Pia unatakiwa kuwa na diary au note book kubwa kuandika bidhaa ambazo hautakuwa nazo wateja ambazo wateja wamehitaji (missing items) ili kukupa kumbukumbu za kuzinunua. Kitu kingine panga vitu ktk mpangilio mzuri usifanye duka ili mradi duka, panga vitu vinavyofanana kwa pamoja na usijaze items nyingi katik display kwa pamoja.

Kauli nzuri kwa wateja, uharaka, uhakika, ubora na hali ya kujali wateja ndo uchawi wako ktk biashara hii. Usisahau kufuga paka mdogo kufukuza panya. JINGINE MUHIMU, hakikisha kila siku asubuhi unapeleka mauzo ya jana yake benki kabla ya kuyatumia, pia usajili biashara yako na uifungulie akaunti ambayo itakuwa na jina la hiyo biashara (mfano MAJIGO RETAIL SHOP).
Biashara ya duka la rejareja siyo ya kudharau hata kidogo

Inatunza familia kabisa na kusaidia kugharamia baadhi ya matumizi kwenye familia. Watu wengi waliotanguliaga kuifanya hii biashara wako mbali saaana, wenmgine wamejenga na kumudu hadi nyumba 'ndogo nyumba' kwa retail shop.

Wengi wameshaongea mengi mazuri kwenye kurasa zilizopita, na mimi sababu ni mzoefu kiduchu, wacha pia nitoe mawili matatu ambayo sijaona yakiorodheshwa hapa, huenda watu wanafanya katika maduka yao au hawafanyi, kama hufanyi unaweza tendea kazi.

USIACHIE FURSA. Kamwe usiuze 'HAKUNA'
Kitu kikubwa katika maduka ya rejareja ni kuhudmia hitaji la kila mmoja kadri uwezavyo. Kamwe usiuze hakuna ikiwa inawezekana icho kitu/bidhaa inaweza kuuzika katika duka lako. Hata kama mhitaji ni mmoja, mletee anachotaka. Ili mradi kile anachohitaji kipo kwenye uwezo wako na unaridhia kuuzika kwako.

Biashara ya vilevi na sigara.
Siagara, Angalia eneo lako la biashara kama kuna watu wanahitaji sigara wawekee.(ikiwa umeridhia na hufungwi na imani yako pia) Beer unaweza weka bia katika miundo miwili, kuuza take awa y(wanaenda kunywa nyumbani), au kama eneo linaruhusu, kukawa na kasehemu wakawa wanakunywa kwa ndani/bandani (duka-grocery). NB usieke pombe ya banana kama eneo lako ni la wastaarabu).

Pombe za kupima kwa shot
Pima K-Vant, Valuu, Konyagi n.k kuendana na eneo shot 500/1000. Weka vipombe vichupa vidogo: Azura/Rivella/Zed/Highlife/Konyagi ndogo/KVant ndogo, ukinunua kwa caton utapata faida kubwa zaidi, ukinunua kwa maduka ya jumla pia utapata pia.

Mfano kwa maduka ya jumla Azura/Rivella n.k unanunua 1600 unauza 200O kwa piece.
K-Vant unanunua 3000-3100, kuuza ni 4000
Konyagi 2700-2800, kuuza ni 3500 n.k.

Vitu vya kupima pima
Kuna mchangiaji ameshaeleza kuhusu Prestige za kupima kwenye kurasa zilipita. Labda niongezee
Maziwa: Kuna maziwa ya kupima, ya fresh/chai na ya mtindi, itategemea zaidi na eneo ulipo sababu ya usafi/usalama kwa wateja wako. Maziwa bei ya kununua na kuuzia itategemea na maziwa unayapata kwa bei gani. Kuna vitu vingine dukani vinatembea fasta pia, kama unga wa lishe, unaochanganya mwenyewe pia. Ila kwa lengo la kuzungusha hela na kueka ubora unaeza nunua kwa watu na kisha ukaweka marhin kidogo ukauza dukani kwako.

Vitu kama sembe, dona kama unaeza saga mwenyewe, margin inakuwa kubwa zaidi kuliko kununua.

NB: Hakikisha unatoa bidhaa bora inayofanana na hizi unga za special, wateja wengine hawaangalii brand, wanaangalia ubora/ladha basi.

Changamoto:
Changamoto za serikali anzia za kata (Bwana Afya), Manispaa (Ushuru) na TRA -Kodi haivikwepeki, kutana nao utajua jinsi ya kudili nao.

Udokozi wa muuzaji: Usipokuwa makini na stock zao utashangaa binti/kijana wa dukani anabadili nguo,saa na vitu vingi kwa kukuibia, kama hufanyi stock kwa kubanwa na muda, funga camera hata mbili tu, zinawaogopeshaga kuiba.


 
Inategemea na unataka kuweka vitu kiasi gani!ila kwa kuanzia milion 2 au 3 inatosha kabisa.
 
naomba kufahamishwa kwa mwenye kujua duka la rejareja la kuuza mchele, juice na kadhalika linaweza kuitaji mtaji kiasi gani

Mkuu majibu mengine ni simple sana, fanya hivi.

Chukua kalamu na Note book then neda kariakaoo na kwingineko tembelea maduka ya jumla chukua bei theni ukukaa chini ukipiga mahesabu utapata kila kitu.

Mkuu ili ufanikiwe katika biashara unatakiwa kuumiza kichwa sana, inatakiwa akili ifanye kazi mara 6 zaidi ya uwezo wake wa kawaida, fanya tafiti mwenyewe mkuu.
 
Ukifanya business plan yako itakupa jibu sahihi kuliko kupoteza muda kwamba hapa tutakupa jibu sahihi kesho utakapoenda kutumia majibu ya hapa ukaona kama umedanganywa.
 
Mie nilimfungulia mama yangu kijijini kwenye frem ya ukubwa wa 3*3 mwanzo wa last year ilinicost jumla ya 3m, I mean niliweka kila kitu kinachostahili katika duka la rejareja.Nafikiri hiyo taarifa inaweza kukusaidia.
 
naomba kufahamishwa kwa mwenye kujua duka la rejareja la kuuza mchele, juice na kadhalika linaweza kuitaji mtaji kiasi gani

Mkuu mtaji alioanza nao Kimario sio lazima na masawe aanze nao huo huo. Halafu mahitaji na gharama yanabadilika kulingana na eneo ulilopo. Kwa mfano kama upo sehemu haina umeme unaweza ukaambulia ushauri uliojumuisha mpaka fridge ya umeme wakati kwako si mufaka.

Kama ungetaka ushauri halisi basi ungeweka data zote hadharani ili ushauriwe lakini kulingana na maelezo yako mimi ninakushauri uanze na hicho kiasi ulichonacho (kama unaeneo la kufanyia biashara), hivyo vitu vingine utaongeza taratibu baada ya kupata faida au fedha za ziada.
 
inategemea na unataka kuweka vitu kiasi gani!ila kwa kuanzia milion 2 au 3 inatosha kabisa.

Sasa Parachichi, hapa ndipo tunapokosea halafu tunalalamika kwamba biashara ni mbaya. Wewe hupasi kuwa na vitu vyako unavyotaka kuweka dukani. Wewe unapaswa kuwa msilikilizaji tu, na unalisikiliza soko linakwambia nini.
 
Mkuu kwani wewe ulikuwa na mtaji wa sh ngapi labda tuangalie ni vitu gani vya muhimu vya kuanzia hiyo biashara yako.
 
Salaam zenu wote! Naomba ushauri wenu kwa mwenye uzoefu wa aina hii ya biashara, je ni mtaji kiasi gani unafaa kuanzia, na faida iko je na jinsi ya kutunza kumbukumbu. Siku hizi ajira ndio hiziii.

Karibuni kwa ushauri.
 
Wakuu,

Natarajia kuwa na duka kwa mara ya kwanza, duka ni la bidhaa za matumizi nyumbani mfano chumvi, sukari, dawa ya meno n.k.

Kwakweli sijui namna bora ya kujua hesabu ya bidhaa zilizouzwa na zile zilizobaki dukani, ukizingatia nitaweka mfanyakazi.

Naomba wazoefu mnisaidie mambo ya kufanya ili angalau mahesabu ya bidhaa dukani yadhibitiwe vizuri.

Karibuni nyote na ahsanteni!
 
Unahitaji vitabu (nunua hata counter books) vya kumbukumbu za hesabu kama vile:

KITABU CHA MATUMIZI
KITABU CHA MANUNUZI, KITABU CHA MAUZO
KITABU CHA MADENI - kwa unaowadai na wanaokudai
KITABU CHA MALI YA BIASHARA, KITABU CHA STOCK.

Vilevile unahitaji kununua mafaili ya kutunzia stakabadhi za manunuzi, malipo, bank slips, mikataba, na nyinginezo ktk mpangilio kila moja na faili lake.

Pia unatakiwa kuwa na diary au note book kubwa kuandika bidhaa ambazo hautakuwa nazo wateja ambazo wateja wamehitaji (missing items) ili kukupa kumbukumbu za kuzinunua. Kitu kingine panga vitu ktk mpangilio mzuri usifanye duka ili mradi duka, panga vitu vinavyofanana kwa pamoja na usijaze items nyingi katik display kwa pamoja.

Kauli nzuri kwa wateja, uharaka, uhakika, ubora na hali ya kujali wateja ndo uchawi wako ktk biashara hii. Usisahau kufuga paka mdogo kufukuza panya. JINGINE MUHIMU, hakikisha kila siku asubuhi unapeleka mauzo ya jana yake benki kabla ya kuyatumia, pia usajili biashara yako na uifungulie akaunti ambayo itakuwa na jina la hiyo biashara (mfano MAJIGO RETAIL SHOP).
 
Ni biashara ngumu kidogo kuidhibiti mfano mfuko wa sukari kg 50 badala ya kutoa faida unaweza kukuletea hasara kubwa sana maana akiuza kg 3 na asiweke kwenye hesabu si rahisi kutambua hivyo basi ni vizuri ufahamu mtaji wako ni kiasi gani na ufanye mahesabu ya mali yote dukani mara nyingi uwezavyo kujua dhamani halisi ya duka lako.
 
Ni biashara ngumu kidogo kuidhibiti mfano mfuko wa sukari kg 50 badala ya kutoa faida unaweza kukuletea hasara kubwa sana maana akiuza kg 3 na asiweke kwenye hesabu si rahisi kutambua hivyo basi ni vizuri ufahamu mtaji wako ni kiasi gani na ufanye mahesabu ya mali yote dukani mara nyingi uwezavyo kujua dhamani halisi ya duka lako.

Mkuu umekumbusha suala muhimu ila kufanya stock si mchezo, itabid angalau niwe nafanya kila baada ya wiki 1
Nashukuru sana!
 
Unahitaji vitabu (nunua hata counter books) vya kumbukumbu za hesabu kama vile : KITABU CHA MATUMIZI, KITABU CHA MANUNUZI, KITABU CHA MAUZO, KITABU CHA MADENI - kwa unaowadai na wanaokudai, KITABU CHA MALI YA BIASHARA, KITABU CHA STOCK. Vilevile unahitaji kununua mafaili ya kutunzia stakabadhi za manunuzi, malipo, bank slips, mikataba, na nyinginezo ktk mpangilio kila moja na faili lake.

Pia unatakiwa kuwa na diary au note book kubwa kuandika bidhaa ambazo hautakuwa nazo wateja ambazo wateja wamehitaji (missing items) ili kukupa kumbukumbu za kuzinunua. Kitu kingine panga vitu ktk mpangilio mzuri usifanye duka ili mradi duka, panga vitu vinavyofanana kwa pamoja na usijaze items nyingi ktk display kwa pamoja. Kauli nzuri kwa wateja, uharaka, uhakika, ubora na hali ya kujali wateja ndo uchawi wako ktk biashara hii.

Usisahau kufuga paka mdogo kufukuza panya. JINGINE MUHIMU, hakikisha kila siku asubuhi unapeleka mauzo ya jana yake benki kabla ya kuyatumia, pia usajili biashara yako na uifungulie akaunti ambayo itakuwa na jina la hiyo biashara (mfano MAJIGO RETAIL SHOP).

Imekaa vizuri.
 
Back
Top Bottom