Msaada: Nahitaji mtu wa kunifundisha gari

Stori yangu ya mimi kujua gari ilikua hivi

Mwaka 2014 natoka zangu school (boarding) nakuta Wazee wamenunua gari RAUM hawakuniambia walisema walitaka iwe saprize basi mzee nikafurahi kwakua ndo ilikua Mara ya kwanza kwa familia yetu kumiliki ndinga ila mimi nilipoiona tuu gari nikawa nawaza kuendesha tuu nikaanza hadi kuangalia video za YouTube jinsi ya kuendesha gari.

Nikimuomba mzee ananiambia subili mpk umalize SIX ndo ntakufundisha nikasema hapa nisipokua mjanja wenzangu school wataendelea kunitambia tuu. Nikawa nasubil wakiondok naenda naliwasha kidg nazima baadae video za YouTube zikanisaidia jinsi ya kuitoa gari naanza naitoa hatua kadhaa alafu nailudisha. Sasa ikaja mother amesafiri ameenda zanzibar na mzee nae yupo mkoa home nipo mimi na madogo na sister wa kazi.

Nikapania Siku hiyo lazima niitoe nyumbani kweli nikaiwasha nikazunguka nayo sana mitaani Luna mjinga akampigia simu mother mother akanipigia mimi akanichimba mkwala mpk ikabidi nikimbie home niende kwa bibi. Siku niliyopewa ndinga ilikua harusi alafu mzee wangu ndo msimamizi yeye na bwana harusi wakaja home kuvaa na kujiandaa shida ikatokea hamna dereva wakuwapeleka kanisani Mzee akaniuliza si unajua kuendesha gari nikajibu kwa ujasiri kabis NDIO basi nikapewa funguo nakumbuka nilitetemeka kidg lakin nilijiamini na tangu siku hiyo nikaamini home nikaanza kupewa ndinga.

So brother jiamini usikubali kusema siwezi
We liongoooo sana unajifunza gari kupitia you tube, kawadanganye wasiojua kuendesha.
 
Wanafanya lakini siyo ya muda mrefu. Wazo lake ni zuri anataka apate uzoefu wa barabarani hasa katika hali halisi sio ile ya kuwa na mwalimu tena unaendesha kidogo tu. Huyu amewaza vizuri.
Asante kwa kunielewa
 
Kiluvya kwa Komba
Mbali sana ila ahsante pia kwa msaada nia yako njema ya kujitolea Mungu akubariki sana sana.
Kuna mdau amejitolea kunisaidia kwa kuniunganisha na mtu hukuhuku Kigamboni, mambo yakienda fresh nitawaletea mrejesho. Asanteni kwa mioyo yenu iliyojaa wema
 
Ningekuwa free ningekusaidia mkuu,

Naelewa shida yako.
Nashkuru sana sana kwa moyo wako mkuu na mungu akubariki!
Hatahivyo kuna mdau amenipatia namba ya kuwasiliana na mtu ambaye yupo hukuhuku kigamboni nashkuru kwa msaada wenu na mungu awazidishie
 
Kwa hiyo VETA wanawapa watu Vyeti na Leseni bila uwezo wa kuendesha gari? Ina maana vijana wetu wanapoteza pesa bure kusoma VETA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio wote wanaoenda VETA kusoma na kupata leseni na vyeti wanapoteza pesa zao hapana.
Wapo ambao tayari wanajua kuendesha hawa hawana cha kupoteza.
Ila kama hujui gari kabisa na nyumbani pia hamna gari ya mazoezi basi amini kile nilichoandika.
 
Kuna wanafunzi wanamaliza miaka saba ya std VII hawajui kusoma na kuandika!

Vipi ushangae mimi kusomea gari mwezi mmoja nisiwe na control?
Ulikuwa unasomea nini?
Nilisoma chuo cha driving mwezi
Week moja darasani week tatu barabarani masaa 2 kila siku tena gari manual .sema hukuwa serious
 
Mbali sana ila ahsante pia kwa msaada nia yako njema ya kujitolea Mungu akubariki sana sana.
Kuna mdau amejitolea kunisaidia kwa kuniunganisha na mtu hukuhuku Kigamboni, mambo yakienda fresh nitawaletea mrejesho. Asanteni kwa mioyo yenu iliyojaa wema
Amina mkuu
 
Ulikuwa unasomea nini?
Nilisoma chuo cha driving mwezi
Week moja darasani week tatu barabarani masaa 2 kila siku tena gari manual .sema hukuwa serious
Muwe mnaelewa na siyo kukurupuka. Driving school za binafsi ni tofauti na VETA. Veta ni theories pale kwa wingi. Veta ni title ndiyo kubwa, lakini kimsingi ni ngumu kujua gari ukimaliza kozi bila kujiongeza pembeni. Kwa anayetaka kujua tu gari kwa masuala binafsi haishauriwi kwenda VETA.

Wewe hujasoma VETA, umesoma private driving school. Mpende kushughulisha bongo!
 
Habari Wakuu,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30 elimu yangu ni form IV natokea kwenye familia ya kimaskini iliyopo Kigamboni jijini Dar.

Kutokana na changamoto na ugumu wa maisha nikaamua kujiunga na kazi ya ulinzi (nimepitia kazi nyingi za msoto).

Hivyo kutokana na changamoto nikaona nisave kipato changu ili angalau niwe na fani yoyote, nashukuru mungu nilifanikiwa kusave nikaenda VETA kusomea udereva (basic driving course) na nikafanikiwa kupata cheti na leseni.

Sasa hapa lindoni kwangu ninapolinda (nalinda nyumba ya mtu binafsi masaki) huyu boss nimejaribu kumwelezea changamoto za maisha ninayopitia alichoniambia kama naweza kuendesha gari nimpelekee cheti na leseni yangu, hivyo vyote nnavyo tatizo sina experience/control hasa vurugu za barabarani naogopa kulitia mtaroni gari la watu nikapata lawama zaidi.

Mwenye nia na uwezo wa kunisaidia niweze kupata uzoefu naomba anisaidie.
Kuhusu pesa ya mafuta nitakuwa nachangia kadri jinsi tutakavyokubaliana.

Naombeni msaada wenu please.
Ahsanteni

Jiamni tu..nilijifunzia manual siku tatu tena kwa mtu tuu ,nilienda kujifunza baada ya kuona mzee kanunua gari na hawezi nipa gari yake niendeshe hadi niwe na leseni.Baada ya hapo nikawa naingia barabarani changamoto zilikuwepo ni kile kiuoga fulani hvi but nilikuja nikazoea na hapo naingia barabarani sheria nayo ijui ni kukaa kushoto tu hayo mengine nikaanza jifunza mtandaoni taratibu sasa wewe mbona uko vizuri mno

Niamini ukiendesha hiyo gari wiki tu utakuwa umezoea na utaanza na kuchomekea wenzio
 
Jiamni tu..nilijifunzia manual siku tatu tena kwa mtu tuu ,nilienda kujifunza baada ya kuona mzee kanunua gari na hawezi nipa gari yake niendeshe hadi niwe na leseni.Baada ya hapo nikawa naingia barabarani changamoto zilikuwepo ni kile kiuoga fulani hvi but nilikuja nikazoea na hapo naingia barabarani sheria nayo ijui ni kukaa kushoto tu hayo mengine nikaanza jifunza mtandaoni taratibu sasa wewe mbona uko vizuri mno

Niamini ukiendesha hiyo gari wiki tu utakuwa umezoea na utaanza na kuchomekea wenzio
ataanza na kuchomekea wenzake hahaha
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom