Msaada: Nahitaji kulipa deni langu benki ya NMB ila wanazungusha kunipa taarifa, nifanyeje?

womanhood

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
609
881
Wakuu nilikuwa na mkopo Benki ya NMB sasa nataka kulipa deni lote lililobaki.

Ila nimekuwa nikizungushwa sana, hii wiki ya pili hawataki kunipa barua kuonesha deni lililobaki, wanasema bado Makao Makuu hawajawatumia hiyo taarifa

Hivyo, naomba kwa anaejua anisaidie nifanyeje ili nipate hiyo barua au niende wapi wanisaidie, maana wanakwamisha mambo yangu ya msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda BOT, nadhani kuna dawati la malalamiko. Niliwahi kumsikia kimei akiwaambia watumishi benki ikikataa kuwapa statement za madeni yao au kukataa wasiuze madeni waende kuwaripoti BOT
 
Ni mtu binafsi!?

Salary Slip huna?
Salary slip ninayo, ila unapotaka kuuza den bank nyingine au kulilipa lote kwa mkupuo, Kuna utaratibu lazima ufuatwe ndo hiyo barua Sasa, ukishapewa ndo una clear deni,
( nahisi kiwango hupungua kidogo sio sawa na kwenye slip sbb unalipa lote , nahisi wanao elewa wataelezea Zaid)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni Mteja wa NMB BANK

Nenda Playstore
Download hii app inaitwa
"Loan Calculator Bank"

Ingiza kiasi ulichokopa
Riba mlokubaliana
Muda wa mwisho kurejesha mkopo wote(kwa miezi).

Kisha Bonyeza kitufe cha "ANNUITY"

Itakuletea Full Statement ya Ulipaji wako wa Mkopo.

Kulingana na miezi uliyokwisha rejesha,
Utaweza kujua ni kiasi gani kimebaki hakijalipwa chote pamoja na Riba yake.

Note:
Bila kua Makini, Loan officers huwa wanatabia ya kujiongeza sana wakupige cha Juu kama Unataka Kuclear loan yako haraka.

Niliwahi Muumbua Loan officer mmoja pale K'koo msimbazi kwa kumuonyesha Ushahidi kwny hiyo APP

Soon alipojaribu kunipigia hesabu za PWAGU na PWAGUZI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Screenshot_2019-01-03-16-49-39.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pakua app yao ya nmb klik, jisajili kisha kila taarifa yako utaipata. Deni unalodaiwa(deni msingi au principle) ambalo ni tofauti na deni linaloonekana kwenye slip.

Wewe umishaliangalia ni million 20, kawalipe milioni 20, maana kwenye slip hua ni deni na riba, unaweza kukuta ni milion 30 kwenye slip ila halisi ikawa milion 18.

Nenda kwa branch manaja, mwambie unataka kulipa deni lote uondokane nao.
 
Nenda katume malalamiko haya haya instagram page yao, ndani ya 30mins watakuwa wamesha respond
Wakuu nilikuwa na mkopo NMB Sasa nataka ku clear deni lote lililobaki.
Ila nimekuwa nikizungushwa Sana hii wiki ya pili hawataki kunipa barua kuonesha Deni lililobaki, wanasema bado makao makuu hawajawatumia hiyo TAARIFA,

Hivyo, naomba kwa anaejua anisaidie nifanyeje ili nipate hiyo barua, au niende wapi wanisaidie, maana wanakwamisha mambo yangu ya msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom