Msaada: Nahitaji kujua wapi nitapata daktari wa kutibu matege kwa watoto

Wakuu poleni na majukumu,naombeni msaada wenu ni wapi nitapata daktari kwa ajili ya matibabu kwa mtoto wa mwaka mmoja na nusu anaonekana kuwa na matege ..Pia nimewahi kumpeleka ccbrt niksambiwa nimrudishe akifika miaka miwili hawakumpatia tiba yoyote..nitashukuru kwa msaada wenu na Mungu awabariki.
Nawakilisha
Usiogope kadri anavyokuwa yatapotea cha muhimu chakula kizuri chenye vitamini d samaki dagaa nk yatapotea amna dr wakutibu matege yataisha yenyewe
 
hata...mmi..picha zangu zinaonesha nilikuwa na matege...but kwa sasa nipo kawaida.....
 
Mkuu usipate presha we subiri kama ulivyoshauriwa na ccbrt hao jamaa nawakubari sana Mimi mtoto wangu wakati anajifunza kutembea alionesha dalili ya kutokuganyaga kisigino yaana mguu mmoja anakanyaga fresh lakini wa kulia akawa anakanyagia vidole mshipa mkubwa ulikuwa haukunjiki nikaambiwa nisihofu nimuache hadi akitimiza 2yrs. Kwasasa hana shida yoyote na sikurudi yaani ulijirekebisha wenyewe pia now Nina shemeji yangu anamtoto wa tatizo kama la mtoto wako naye ameambiwa asubiri afikishe 2yrs.
Nakushauri usihangaike hangaike utapoteza pesa bure we fuata ushauri wa ccbrt tatizo watalitatua.
 
Asante kwa ushauri mkuu
 
Namfahamu bwana mmoja alimfanyia binti yake akiwa mdogo upasuaji mbalimbali kwa ajili ya matege;
lakini kadri alivyokuwa anakua ndivyo miguu ilizidi kuharibika.

Matege siyo ugonjwa, endelea kumpa vyakula stahili na navyokuwa miguu itanyooka tu;

Usije ukamharibu mtoto na huko kutoelewa kwenu.
 
Sawa sawa mkuu,asante kwa ushauri
 
Mkuu kama kwenu hakuna matege usiogope, kadri anavyokuwa yatapotea.Nilikuwa na Mdogo wangu mtoto wa Baba Mdogo ilikuwa balaa.Yaani yalipinda utadhani ni zero kabisa, ila saiv ukimuona huwezi amini, halafu tall
Ilikuwaje ikawa hivyo
 
Back
Top Bottom