Msaada: Nahitaji kujua ilipo Wizara ya Afya

kituli one

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
408
301
Wana JF,

Kesho naingia kwa mara ya kwanza Dar nikitoka Mawemilu Shinyanga Vijijini, sasa naomba msaada wa kuelekezwa wizara ya afya ilipo maana ndo nina shida huko, natanguliza shukurani zangu.

========

Waungwana nashukuru sana nimefika hapa wizarani,na mambo yangu ndo nayashughulikia hivyo...baadae kidogo nitaanza utalii wa ndani hapa daslam na kutumia mahela yangu niliyouza ng'ombe
 
Watu wa mikoani mkija Dar mnatia huruma sana...Ukishuka Ubungo panda Mabasi ya mwendokasi shuka kituo cha posta zamani ...ukitoka ndani ya kituo kodi city cab mwambie Dereva akupeleke Wizara ya Afya.Karibu Dar
Sasa kuna haja ya kunisema mkuu...we wa Dar ipo siku utakuja na kwetu mikoani
 
Screenshot from 2016-09-05 21-55-31.png
 
Hahaaaa kweli jamaa anatia hurumaa, hapo bado sasaa shughuli ataipata kuvuka barabara heheheee. Usijali mkuu, fuata jinsi wadau walivyokuelekeza hapo juu
 
kwani nyie Wanaume wa Dar mnaoshindia Mahindi ya kuchoma yaliyopakazwa pilipil na Miguu ya kuku Mkija huku kwetu Kibondo hamuwez kuuliza Sekondari ya Bitulana iko Maeneo gani? Achen sifa za Kijinga. Mkuu kutoka kwa Wananzengo, ukifika Ubungo Panda Gari zinazotoka Kimara kwenda Posta zipo chache saana. Then Shuka Posta mpya, fuata barabara kule gari lilikokua likielekea mpaka uikute Sanamu ya Askari. Ukiifikia Sanamu ya Askari Pinda barabara ya Kulia kwako uende nayo takriban mita 800 mbele Mkono wako wa Kulia mkabala na IFM utaziona ofisi za Afya.
 
Acheni upimbi nyiee, kwani nyie Wanaume wa Dar mnaoshindia Mahindi ya kuchoma yaliyopakazwa pilipil na Miguu ya kuku Mkija huku kwetu Kibondo hamuwez kuuliza Sekondari ya Bitulana iko Maeneo gani? Achen sifa za Kijinga. Mkuu kutoka kwa Wananzengo, ukifika Ubungo Panda Gari zinazotoka Kimara kwenda Posta zipo chache saana. Then Shuka Posta mpya, fuata barabara kule gari lilikokua likielekea mpaka uikute Sanamu ya Askari. Ukiifikia Sanamu ya Askari Pinda barabara ya Kulia kwako uende nayo takriban mita 800 mbele Mkono wako wa Kulia mkabala na IFM utaziona ofisi za Afya.
Nani aje huko?kufanya nini sasa?kama ni mazao mnatuletea,kama wanawake ndo wanakuja kila siku wakiwakimbia huko,kama huduma za kijamii hapa ndo home kwake,huko tufuate nini?labda tuje kufanya kautalii kakuangalia jinsi mlivyofanana na viumbe wa huko kama tumbiri,ngedere,ng'ombe nk,(usikasirike lakini huuu ni utani wa jadi)
 
Acheni upimbi nyiee, kwani nyie Wanaume wa Dar mnaoshindia Mahindi ya kuchoma yaliyopakazwa pilipil na Miguu ya kuku Mkija huku kwetu Kibondo hamuwez kuuliza Sekondari ya Bitulana iko Maeneo gani? Achen sifa za Kijinga. Mkuu kutoka kwa Wananzengo, ukifika Ubungo Panda Gari zinazotoka Kimara kwenda Posta zipo chache saana. Then Shuka Posta mpya, fuata barabara kule gari lilikokua likielekea mpaka uikute Sanamu ya Askari. Ukiifikia Sanamu ya Askari Pinda barabara ya Kulia kwako uende nayo takriban mita 800 mbele Mkono wako wa Kulia mkabala na IFM utaziona ofisi za Afya.
Hahaaa,harafu wengi wao ndo wametoka hukuhuku wanaona aibu kurudi maana maisha yamewapiga
 
Back
Top Bottom