Msaada: Nahitaji kuelewa kuhusu haya mambo ya ajabu yanayonitokea

The king mswati

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
787
820
Kwa kipindi kama cha miaka miwili hivi sasa kuna mambo yananitokea na naweza kuyaita ni ya ajabu.

Siwezi kuyaweka wazi sana kwa sasa ila nimeanza kuhisi kwamba huenda kwenye hii Dunia tunaishi na viumbe wasioonekana kwa macho ya kawaida.

Na kwa hayo matukio yanayonitokea inaonekana hawa viumbe wana uwezo wa kutuona sisi na kila kinachoendelea juu yetu ila sisi hatuwezi kuviona hivyo viumbe.

Na kuna uwezekano vikawa na uwezo mkubwa tu kifkra kuliko sisi wanadamu na tunaishi navyo humu humu duniani.

Swali langu ni Je, kuna uwezekano kuhusu haya niyawazayo kwamba tunaishi na viumbe humu humu duniani ambavyo havionekani kwa macho ya kawaida ila vyenyewe vinaweza kutuona sisi ? Au ni ndoto tu (ingawa ni ngumu sana kuamini kuwa ni ndoto hata kama ni usiku ila nakuwa macho kabisa najitambua na naona vitu flani vikitendeka ila wanaofanya huwaoni) .
 
Subiru kwanza vipi ushajiunga na masonic maana nakumbuka ulisema uko hatua za mwisho mwisho ...!! Theb tujadili hao vibwengo wanaokutokea.
 
Back
Top Bottom