Msaada: Nahisi nimefungwa kishirikina na mke wangu

Wade 3

Senior Member
Mar 26, 2018
180
423
Habari Wana JF

Ninaishi na mke wa watoto wetu wadogo ambao ni mapacha wana mwaka mmoja.

Nimekuja hapa kuomba msaada baada ya kuona kuna mambo hayaniendei sawa tofauti na mwanzo. Nilipooana na huyu mke wangu mambo yalikuwa vizuri tu hadi mwezi wa 10 mwaka huu mambo yakabadilika baada ya yeye kuziona meseji za mwanamke mwingine kwenye simu yangu, kweli nikiri lilikuwa ni kosa nilijitahidi sana kumuomba msamaha akakubali kunisamehe lakini ikawa haiishi wiki lazima akumbushie, ugomvi unaanza upya kati yetu ,mambo yakawa ni hivo tu hadi nilipoondoka kwenda mkoa mwingine kikazi ambako ndio nipo hadi sasa.

Baada ya kufika huku naona kuna mambo hayapo sawa kabisa kwenye maisha yangu tofauti na mwanzo hasa kwenye sekta ya mapenzi. Nahisi huyu mke wangu amenifunga nisiweze kupata mwanamke yeyote wa kufanya nae mapenzi.

Ni kweli nimeoa Ila nipo safari mwezi mmoja na nusu kama mwanaume ambae nina hisia lazima nipate kipozeo kidogo ,lakini imekuwa tofauti kabisa hadi leo kila nitakojaribu sipati kitu.

Nikasema labda nijaribu basi kwa wanaojiuza nako mambo ni yale yale hamna nilichopata, licha ya kwamba pesa kidogo zipo lakini kila sehemu natolewa nje.

Naombeni msaada wa ushauri nifanye nini, maana nahisi kama mke wangu kanifunga nyota kishirikina ili nisiweze kupenzika ,mpaka niwe na yeye tu.

Au Kama kuna mtu amewahi kupitia ishu kama hii alifanyaje kujiokoa.
 
Mkuu ni vitu vitatu tu binadamu akivikosa alanaweza kupata madhara kiafya hata Kufa:

1. Chakula
2. Mavazi
3. Malazi

Heshimu ndoa yako bro, ngono sio hitaji la msingi kwa binadamu, mpende na mheshimu mkeo. Analea watoto wako kumbuka
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom