Msaada: Nahisi mdogo wetu wa kike kaongopa kuwa yupo field ila nahisi huenda kafungiwa na Mwanaume huko mkoani

Priscallia

JF-Expert Member
Nov 9, 2019
495
2,427
Kama kuna mwanafunzi anayesoma Chuo cha Mipango Dodoma ama mtumishi wa hicho chuo ama mzazi mwenye mtoto anayesoma hapo naomba anithibitishie hili kuna mdogo wetu namlipia ada katika chuo taja hapo juu kozi ya “Bachelor Degree in Human Resource Planning and Management (BDHRPM).

Sasa jumamosi hii nilikuwa katika huo mji mkuu wa serikali nikasema nimpigie simu ili nipate kumkaribisha mahali apate chakula cha mchana na jioni kupokea hakutaka ila akanitext kwamba ana emergence kasafiri kaenda wilaya ya jirani kwa field? na sehemu alipo hakuna network nzuri bora tuwasiliane kwa text.

Alivyotaja FIELD akili yangu ikagutuka kidogo maana miaka yetu field huwa tunafanya mwishoni mwa semester, kengele ikanijia kichwani huwenda huyu mdogo wetu ndio keshaanza kuitembea Tanzania na viunga vyake akiwa hapa dodoma pamoja na wabab wa watu.

Na isitoshe huyu mdogo wetu tunatumia gharama nyingi kumsomesha kwa kweli hata ile morali ya kujiachia nikiwa dodoma ikapotea maana nilikuwa na mawazo mengi kichwani moja wapo ni kuwa huwenda kuna kibaba cha mtu kimemsafirisha mkoani ukitegemea wiki ilikuwa na likizo ndefu kidogo takribani siku nne kupisha sikukuu ya pasaka.

Hivyo nimekuja humu ndani kupata ukweli, hasa ukitegemea JF imesheheni watu wa aina mbalimbali na katika nyaja tofouti tofouti huwenda wakawa na ABC,s kuhusiana na hiki chuo ni kweli hawa wanafunzi wa mipango wameanza field katikati ya masomo, ama huyu mdogo wetu ameamua kunidanganya kuficha uchafu anaofanya pindi akiwa chuo kwa kutoroka vipindi kwenda kufanya maovu mikoani huko.

Naomba nipate ukweli kama kweli wameanza ratiba ama laah.
 
..kupokea hakutaka ila akanitext kwamba ana emergence kasafiri kaenda wilaya ya jirani kwa field? na sehemu alipo hakuna network nzuri bora tuwasiliane kwa text.
Network mbaya ila simu inaita na text anaweza kutuma?

You can’t be this dump.. are you? Hayupo field huyo. Si umuulize mwenyewe yupo wilaya ipi na anafanyia field kwenye institution ipi?
 
Network mbaya ila simu inaita na text anaweza kutuma?

You can’t be this dump.. are you? Hayupo field huyo. Si umuulize mwenyewe yupo wilaya ipi na anafanyia field kwenye institution ipi?
Hawa wadogo zetu hasa wa jinsia zetu hizi hukumbana na ushawishi sana hasa ukitegemea ni hapo dodoma yaani hamu ya kubaki huko ikaniisha kaniambia ni babati manyara.
 
pole mimi dogo alikuwa udom mwaka wa kwanza kaenda kuanza, kwakuwa tulikuwa tunambana sana nyumbani basi alipoenda chuo kaenda kujiachia mwisho kapata mimba, kaenda kutoa ikagoma akataka kufa tukamsaidia kapona. Alipopona likizo ya kwanza karudi nyumbani wote wamegoma kumlipia ada kabaki nyumbani sasa hivi kaenda kwa aliyempa ujauzito wanaendelea na maisha.

Hapo nyuma alikuwa anatudanganya wameenda kihuduma za kiinjili mara singida, mara mwanza mara morogoro kumbe alikuwa anapelekwa na wababa wake huko. Hadi kesho chuo kimesimama tangu mwaka jana kaambiwa mume wake amsomeshe sisi kama wazazi tumeishia hapo. Kuwa makini nawe ndugu yangu
 
Wadada wa MIPANGO DODOMA ni hatari sana hao, hicho chuo ukipeleka mtoto wa kike asiyejitambua vizuri ataliwa sana tu.

Pale maeneo ya CBE kuna Logde moja inaitwa NELISSA, wanaliwa sana mule wadada wa Mipango.

Naombe nieleweke hivyo tu.
 
Bila shaka tayari ana zaidi ya miaka 18 ana haki zote kujiamulia atakavyo kikubwa avunji sheria za nchi, pole sana.

Mengine unabaki kuwa mshauri tu.
 
Ulikuwa dodoma,ulishindwa nini kufika chuoni na kuupata ukweli?
Ulishasema ni likizo mbona tena unasema anadoji vipindi
Kinachokuumiza sio kusoma ila ni mawazo ya kuliwa kwa sista ako,je yule ni mtoto unamchunga(ungekaa naye kwako)
Mwisho
Jifunze kupotezea mengine sio kila kitu akupe taarifa,japo haijakaa poa lakini jitahd i kuyapotezea
N.B miaka ya 2015 UDOM sina kumbukumbu sana wanachuo walienda kujirusha mwanza bahati mbaya wakapata ajali,kiukweli haikuwa nzuri kwa wazazi maana mzazi anajua mtoto yupo dodoma ila taarifa za kifo zinatokea mwanza
Ila mkuu usinipopoe kweli inauma jamani
 
Kama anaperfom vizuri basi achana nae. Binti umri wa chuo ni tayari mtu mzima huyo. Na mtu mzima akiamua lake atalifanya tu.
Kikubwa ukikutana nae mkumbushe kuwa dunia ina majaribu na hapo chuo anatengeneza maisha yake mwenyewe. Mengine ni yeye na akili yake.
 
Back
Top Bottom