Msaada na ushauri wa nini cha kusoma, kitakacho niwezesha kujiajiri baada ya kuhitimu na sio kutegemea kuajiriwa.

Joined
Nov 24, 2017
Messages
23
Points
45
Joined Nov 24, 2017
23 45
Wapendwa wanajukwaa habari.
Poleni na majukumu ya hapa na pale.

Kama kichwa cha habari kinavojieleza hapo juu, ninaomba msaada wa kimawazo na ushauri wa kipi nikasomee chuoni ili baada ya kuhitimu niwe na uwezo wa kujiajiri mwenyewe kwa kutumia elimu nitakayoipata.

Ninafahamu zipo kozi ngingi tu zinazoniwezesha kujiajiri lakini naamini kupitia wataalamu wa jukwaa hili ninaweza kupata msaada wa kimawazo na ushauri juu ya kozi ambazo zipo sokoni na zinalipa sana kwa sasa kulingana na mahitaji ya leo na hapo baadae.

Hata kama kozi husika haipatikani katika vyuo vya hapa nyumbani tanzania, ila inapatikana nchi jirani kama kenya nk. nisaidie tu nitaifuata hukohuko ilimradi tu iniwezeshe kujiajiri 100% baada ya kuhitimu.

Ndugu kwa kuanzia tu ni kwamba, nimepewa wazo la kusoma
1: PHARMACY
2:UFUNDI WA UMEME WA MAGARI YA UJERUMANI

KUHUSU ELIMU YANGU
Binafsi elimu yangu ni form six nilimaliza mwaka 2017 katika mchepuo wa PCM, kwa bahati mbaya tangu nilipokuwa A-level niliugua masikio (uwezo wangu wa kusikia ulishuka sana) lakini kwa msaada wa Mungu nilifanikiwa kumaliza advanced level salama na kufaulu japo kwa taabu.

Baada ya kumaliza kidato cha sita ilinilazimu kutoendelea na masomo ya chuo ili kushughulikia kwanza tatizo la masikio, walau kuongeza uwezo wa kusikia ili nikija kwenda chuoni niende nikiwa nime-improve uwezo wa usikivu wa masikio yangu. Sasa ninashukuru Mungu nimefanikiwa hilo japo sio kwa 100%. Lakini walau ninaweza kumudu suala zima la "mawasiliano" , masomo na pilikapilika za maisha ya kila siku.

Ninatanguliza shukrani.
 
Mlenge

Verified Member
Joined
Oct 31, 2006
Messages
825
Points
1,000

Mlenge

Verified Member
Joined Oct 31, 2006
825 1,000
Pole kwa kuumwa.

Kwa vile umesoma PCM, naamini unaweza kujifunza chochote. Unahitajika kuwa na dhamira na nia ya kuthubutu kujifunza.

Ni vema kupata Professional Certification kwenye field of your choice.

Refer: 
Joined
Apr 1, 2019
Messages
78
Points
150
Joined Apr 1, 2019
78 150
Wapendwa wanajukwaa habari.
Poleni na majukumu ya hapa na pale.

Kama kichwa cha habari kinavojieleza hapo juu, ninaomba msaada wa kimawazo na ushauri wa kipi nikasomee chuoni ili baada ya kuhitimu niwe na uwezo wa kujiajiri mwenyewe kwa kutumia elimu nitakayoipata.

Ninafahamu zipo kozi ngingi tu zinazoniwezesha kujiajiri lakini naamini kupitia wataalamu wa jukwaa hili ninaweza kupata msaada wa kimawazo na ushauri juu ya kozi ambazo zipo sokoni na zinalipa sana kwa sasa kulingana na mahitaji ya leo na hapo baadae.

Hata kama kozi husika haipatikani katika vyuo vya hapa nyumbani tanzania, ila inapatikana nchi jirani kama kenya nk. nisaidie tu nitaifuata hukohuko ilimradi tu iniwezeshe kujiajiri 100% baada ya kuhitimu.

Ndugu kwa kuanzia tu ni kwamba, nimepewa wazo la kusoma
1: PHARMACY
2:UFUNDI WA UMEME WA MAGARI YA UJERUMANI

KUHUSU ELIMU YANGU
Binafsi elimu yangu ni form six nilimaliza mwaka 2017 katika mchepuo wa PCM, kwa bahati mbaya tangu nilipokuwa A-level niliugua masikio (uwezo wangu wa kusikia ulishuka sana) lakini kwa msaada wa Mungu nilifanikiwa kumaliza advanced level salama na kufaulu japo kwa taabu.

Baada ya kumaliza kidato cha sita ilinilazimu kutoendelea na masomo ya chuo ili kushughulikia kwanza tatizo la masikio, walau kuongeza uwezo wa kusikia ili nikija kwenda chuoni niende nikiwa nime-improve uwezo wa usikivu wa masikio yangu. Sasa ninashukuru Mungu nimefanikiwa hilo japo sio kwa 100%. Lakini walau ninaweza kumudu suala zima la "mawasiliano" , masomo na pilikapilika za maisha ya kila siku.

Ninatanguliza shukrani.
Kuna walakini kwenye haya maelezo yako ndiyo maana wengi wanashindwa waanzie wapi kukushauri.

By the way, kama mpango wako ni kujiajiri kama ulivyosema nakushauri ukasomee elimu ya ujuzi kwenye vyuo vya VETA vinavyotambulika na serikali.

Ni hayo tu!
 
Joined
Nov 24, 2017
Messages
23
Points
45
Joined Nov 24, 2017
23 45
Kuna walakini kwenye haya maelezo yako ndiyo maana wengi wanashindwa waanzie wapi kukushauri.

By the way, kama mpango wako ni kujiajiri kama ulivyosema nakushauri ukasomee elimu ya ujuzi kwenye vyuo vya VETA vinavyotambulika na serikali.

Ni hayo tu!
Ahsante nimekupata
Ingekuwa poa sana kama ungenisaidia ni wapi maelezo yangu yanapwaya, taarifa zipi zinapelea au zinakosekana ili kupata ushauri mzuri zaidi.

Shukrani
 
SUKAH

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Messages
582
Points
250

SUKAH

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2013
582 250
Kasome ufundi wa umeme wa magari. Nadhani ni vizuri kuanza na biashara zinahusisha utoaji wa huduma.

Huwezi kuporwa ujuzi utakaokuwa nao, kikubwa uwe updated kila baada ya muda fulani. Maana mambo hubadilika kwa kasi sana.
 
Rohombaya

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Messages
11,325
Points
2,000

Rohombaya

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2011
11,325 2,000
Dah...bado nasisitiza....hakuna fani yoyote mbaya....mbaya ni mwanafani....hakuna fani yoyote isiyolipa...asiye na pesa ni mwenye fani....Chagua fani unayoipenda ili ukitembea unaiwaza...kila unachokiona unafikiria fani yako itakiboresha vipi...utakuwa mbunifu....utakuwa radhi hata kutoa huduma bure kwa fani yako kwa sababu kila unachofanya kinakupa furaha.... Vinginevyo utakuwa daktari anayelipwa vizuri lakini anawachukia wago jwa wanaoingia wakati yeye anajifunza namna kupika visheti kwenye kompyuta
 
Forum statistics

Threads 1,367,249
Members 521,703
Posts 33,392,843
Top