Msaada mwenye namba ya Mkuu wa Mkoa Dar katuachia majanga

LEGE

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
5,123
9,168
wiki hii mkuu wa mkoa alitembelea mwenge stendi na maeneo yanayozunguka mwenge stendi ziara hiyo imegeuka kuwa chungu kwa vijana mafundi wanaofanya kazi eneo la mwembeni karibia na zahanati ya mwenge.

karibia na zahanati ya mwenge kwenye geti la kuingilia mazingira nimachafu sana kuna chemba inatema maji machafu na mita kadhaa mbele yake kuna dampo limeanzishwa hapo.kiukweli maeneo hayo ni kero harufu ni mbaya sana.

kabla mkuu wa mkoa hajafanya ziara yake serikali ya kijiji ilipita kuhamasisha na kutoa maagizo usafi ufanyike kweli vijana walifanya usafi wa mitaro na kufyeka nyasi pamoja na kukata baadhi ya miti iliyokuwepo mbele ya dampo hilo ambapo mbele yake kunabalabala ya rami.kiukweli kiuhalisia kitendo kile nikizuri kutokana na manyasi hayo na kichaka hicho kiligeuka kama mazaria ya mbu na choo kwa wafanya biashara ndogondogo na watu wanaopatikana maeneo hayo.

lakini kwa upande wa pili kitendo hicho kimetafsiriwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria na nikosa kubwa sana na uongozi wa mwenge.
ishu nikuwa baada ya kufanya usafi hasa kukata miti ndipo jarara hilo likawa linaonekana kwa upande wa mbele wa barabara ambapo mtuyoyote akiwa anapita na gari au kwamiguu lazima alione na ndipo lilipo onekana jalala hilo na mkuu wa mkoa na kumpigia mwenyekiti wa serikali za mtaaa. kilichofuata hapo wao viongozi wa serikali za mtaa pamoja na mabaunsa waliendesha operation ya kuja maeneo hayo kukamata vijana na kupiga na wengine kuwaweka ndani wakilaani kwanini wamewavua nguo na kuwaacha uchi?? inamaana kitendo chakufanya usafi hasa kukata miti na kufanya dampo hilo kuonekana ndio kosa kubwa.
mpaka hivi sasa kuna vijana 4 wamekamatwa na kupelekwa mabatini viongozi wa serikali za mitaa wamefuatwa wanadai hawatolewi mpaka watoe laki 6.hizo ni garama za kuhamisha dampo hilo maana magari ya city yanapokuja kuchukua taka hizo yanalipwa.

chakushangaza zaidi nikuwa takataka hizo hazijatupwa bahati mbaya au na watu wasio fahamika ni kuwa dampo hilo wao wenyewe ndio wanao limiliki na kunamikokoteni huwa inakuja kushusha takataka hapo na huwa wanawachaji pesa.
tumechoshwa na huu ubabe unaoletwa na hawa mapapa wa mwenge wanaonenepeana kwa pesa za wanyonge
SEREMANI CHAU NA WENZIO mnakumbuka ni siku chache zimepita mmewatia hasara sana watu wa mwenge. unakumbuka kuna pesa ilitolewa watu wakufanyie kitu mbaya ulikuwa unaishi mafichoni/?? ushasahau sio??.
 
Back
Top Bottom