Msaada: Mwenye elimu juu ya kutembea na Gari kwa kutumia Chasis Number

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
549
785
Wakuu naombeni Msaada, nimetoa Gari Bandarini nataka kulipeleka TBS likakaguliwe njiani wamenikamata Matrafiki mara mbili wanasema siruhusiwi kutembea na Gari ikiwa na Chasis Number hadi isajiliwe,kama nataka kulipeleka TBS nitafute Gari la kuibeba.

Awali mtu wa Clearing aliniambia nikate Bima tu tukafanya hivyo ila akaniambia naweza kwenda nayo TBS ila hairuhusiwi kutembea baada ya saa 12 jioni, ila cha kushangaza niko Barabarani bado asubuhi Trafiki wamenikamata na muda huu wamezuia Gari kabisa.

Nashindwa kupambana kwasababu sina uelewa wa uhakika wa haya mambo, mwenye uelewa anisaidie na kama naweza kupata Sheria zaidi na namna ya kukomboa Gari langu nitafurahi.
 
Wapuuzi hao, hawajui 12 asb Hadi 12 jioni? SEMA hata ukisonga mbele watadai muda ulikuwa alfajiri mmma. ma, eee..za...o
 
Wakuu naombeni Msaada, nimetoa Gari Bandarini nataka kulipeleka TBS likakaguliwe njiani wamenikamata Matrafiki mara mbili wanasema siruhusiwi kutembea na Gari ikiwa na Chasis Number hadi isajiliwe,kama nataka kulipeleka TBS nitafute Gari la kuibeba.

Awali mtu wa Clearing aliniambia nikate Bima tu tukafanya hivyo ila akaniambia naweza kwenda nayo TBS ila hairuhusiwi kutembea baada ya saa 12 jioni, ila cha kushangaza niko Barabarani bado asubuhi Trafiki wamenikamata na muda huu wamezuia Gari kabisa.

Nashindwa kupambana kwasababu sina uelewa wa uhakika wa haya mambo, mwenye uelewa anisaidie na kama naweza kupata Sheria zaidi na namna ya kukomboa Gari langu nitafurahi.
Unakata insurance kwa registration ipi?
 
Wapoze tu ila inatakiwa ndan ya wik mbili uwe umepata namba zisidi apo na umaweza kukata bima kwa kutumia chases no
 
Kuwa mpole, na uwaeleze ulifuata maelekezo toka bandarini;watakuelewa na mambo mengine yataendelea.
 
Waambie waache njaa,watosheke na mishahara yao.
Waoneshe faili la gari waache njaa zao za kingese.
 
Yaani unaendesha gari ina chassis # tu, then traffic wanakupiga mkono na unasimama!!
 
Hapa ndiyo unakuja umuhimu wa kuwa na namba za simu za wakuu wao makao makuu
 
Kwa jinsi nijuavyo Gari ikiwa na Chassis No. unaruhusiwa kutembelea kuanzia 0600 mpaka 1800 bila shida yeyote. Japo kuna watu hata Usiku unapishana nao na hawana tabu.

Kuna Jamaa namjua toka Mwezi wa Kwanza anaendesha Gari lina Chassis No.; kwa maelezo yake ni anasubiri namba E ndiyo alisajili..Hadi mikoani huwa anaenda nalo.

Ila mambo mengine ni ya kufunika kombe mwanaharamu apite tu Mkuu, wakatie ya maji kisha endelea na mambo yako..
 
mwanajeshi huyo ana subaru forester.
 
Back
Top Bottom