Msaada: Mwanaume ninayeishi naye haoneshi kunipenda na hataki tuachane

Bi dentamol

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
987
1,912
I hope mko poa guys

Naitaji ushauri hapa serious kabisa

Mimi ni mwanamke nina miaka 30 nina mchumba ambaye wazazi walishatupa ruhusa ya kuishi pamoja

Mwaka 2016 nilipata kazi ya muda mfupi katika kampuni fulani nilifanya kazi ndani ya miezi minne nilikutana na kaka ana 33 kwa a

Huyu Kaka nilimpenda sana alikuwa mtu fulan mpole hana Mambo ya ajabu ukweli nilitokea tu kuvutiwa nae. Nikafanya juhudi tukawa marafiki wa karibu, kusaidiana mambo mbalimbali haikupita muda tukawa tumeanza mahusiano ya kimapenzi

Uzuri jamaa alikuwa hayupo katika mahusiano serious, alikua na mwanamke ambae walikua hawafahamiani aliunganishiwa na jamaa tu so wakawa na mapenzi ya kwenye simu

Baada ya miezi 6 jamaa akanipeleka kwao kunitambulisha ilikua Desemba mwaka jana, Februaru mwaka huu alihamishwa mkoa mwingine kikazi nami nikaacha pale nikaanza biashara zangu binafsi. March akaja nyumbani kwetu kujitambulisha, Juni kupanga na kutoa mahari.

Oktoba Wazazi pande zote mbili walikutana kupanga mambo ya ndoa, wazazi wake wakaomba tuchukuane tu kwa sasa hawana uwezo tutafunga ndoa mwaka kesho. Hii ni sawa kwa jamii ya wasukuma wa kijijin kwani huamini ukishamtolea mahari mwanamke tayari wanakuja kumchukua. Familia yangu ikakubali

Kilichonileta kwenu

Baada ya kukaa kiuchumba na jamaa nilikua nahisi hanipendi tangu kabla hajanipeleka kwao nikawa najiondoa kwake ajabu nikikaa nae nikimwambia tuachane hakubali kabisa anaweza hata jitupa chini akibembeleza nisimuache

Nikimuangalia ni mtu ambae haoneshi kama ananipenda anaweza kaa siku 1 au 2 bila kunipigia. Ninaweza pata shida kunisaidia akawa mzito mno. Ni mtu ambaye hajali unaumwa, umepata matatizo unaishi vipi haelewi

Mwanzo nilihisi labda anamahusiano mengine lakini nilifanya uchunguzi sikubaini hicho. Mi nampenda najikuta naumia nahitaji kupata attention yake, muda wake, nilishaongea nae sana. Ni mtu ambae hata kuniambia nakupenda au nimekumiss au kuniita tu mpenzi wangu ni ngumu labda muwe kitandani kapandwa na hisia anaweza fanya hivyo au muwe mna ugomvi anakubembeleza au ndio mmeelewana

Atafanya hivyo for 2 days then anarudi katika hali yake

Nilishaongea nae kama hanipendi nimeshamuomba aniache niumie badae nitazoea hataki. Kuna kipindi nilimwambia aniache tu atafute mwanamke anaempenda na nikamchunia kweli

Aliteseka sana alinitafutia washauri sio ndugu zake, rafiki zake na zangu. Nashindwa kuelewa nitaishije na huyu mtu jamani. Sielewi ni maumbile yake yuko hivi, makuzi au tu hanipendi!

Amekulia kijijini hasa tena hasa nashindwa kuelewa labda ndivyo alivyo. Nawaza labda yupo kwangu kimaisha tu sababu yeye ana kazi nzuri mshahara mkubwa lakini familia ya kwao inamuelemea ukoo mzima unamtegemea yeye

Mimi kipato changu kidogo kwake lakini nina maendeleo kidogo namzidi na ninafanya vitu vya msingi. Nahisi labda jamaa amefata maisha!

Wadau samahani kwa kuwachosha naombeni mawazo yenu
 
haya maneno wakat mwingine ni magumu kutamka kama humpendi mtu

kimawazo yangu: jamaa hakupendi ila amekuzoea hivyo kuwa ngumu kukupoteza ndo maana anaomba msamaha .

jamaa anakupenda ila hajakulia kikanjanja hivyo kutamka nakupenda, nisamehe inakuwa ngumu kwake.

asa afate maisha vp ikiwa anakuzidi kipato
 
Huna sababu za msingi za kuachana nae maadam anakupenda hizo ni tabia tu binafsi za mtu. Hata Mimi Sikumbuki mara ya mwisho kumwambia mkewangu nakupenda ni lini lakini mahitaji na mambo mengine nampatia. Muhimu wakati mpo pamoja atajifunza mengi usikate tamaa.
Sasa najuaje Kama ananipenda?
 
Back
Top Bottom