Msaada: Mwalimu mwenye cetificate akijiendeleza mpaka degree, je mshahara utaongezeka?

Mar 30, 2016
38
12
Ningependa kujuzwa mwalimu mwenye certificate akienda kujiendeleza na kuhitimu degree je akija kwa waajili atakapopanda daraja atakuwa na salary tofaut na wengine wenye certificate japo wameajiliwa pamoja ni hilo tu.
 
Mishahara inalipwa hivi
Ukiwa na cheti tgts B1
Diploma tgts C1
Degree tgts D1
Sasa ukijiendeleza ukapata degree unastaili D1 kama umeishaifikia u abaki hapo hapo isipokuwa unabadilisiwa muundo wa utumishi
 
Mwl mwenye certificate mwisho wake wa kupanda daraja ni F1 wakati aliejiendeleza ataendelea kupanda hadi daraja J1kwa sababu ya kubadilishiwa muundo
 
Ukweli mshahara unaongezeka sana mdau,kama hutajiendeleza,utapanda madaraja mpaka ukifikia TGTS F,ambapo basic yake ni kama 1,235,000/=Hivi halafu hutapanda tena. Lakini ukijiendeleza mpaka Degree utapanda madaraja mpaka TGTS I,kitu km mil.2 na kitu hivi.
Hayo ndiyo maelezo kamaili,kwahiyo kama unataka kusoma,fanya hivyo mkuu
 
Sasa mkuu kwa hiyo kwa mfano ukimaliza kusoma degree je kama ukikuta unapanda kwenda daraja D je watakurusha daraja lingine au utapanda D na wenzako japo wana certificate
 
Baada ya kumaliza Degree kitu cha Kwanza Unabadilishwa kutoka Muundo wa ngazi ya Cheti na Kuwekwa kwenye Muundo wa Degree, ambao TGTS YAKE NI D.kWAHIYO kama ulikuwa nawenzio waliokuwa ngazi yacheti na walikuwa hawaja fikia Tgts D, basi wewe utawaacha utapewa muundo mpya, kama watakuwa wameshafika,basi utapanda nao ,ila utakuja uwaache kwenye madaraja ya ukomo.
 
Umuhimu wa kujiendeleza unakuja pale unapogota ktk kupanda madaraja ndio unatumia cheti cha degree kuendelea kupanda wakati wenye certificate mwenzio ndo anaishia hapo anangojea increment tu
 
ndio unapanda. ila naskia tanzania hamna mshaara wa masters! naomba wataalamu wanieleweshe hapo .
 
Back
Top Bottom