Msaada Muongozo wa namna ya kununua ardhi ambayo tayari ipo kwenye process ya kupimwa

vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
6,310
10,345
Wataalamu naomba msaada wenu, kuna Ardhi nataka kununua, muuzaji tayari alishalipia kwaajili ya upimaji na usajili lakini wapimaji bado hawajafika kwa ajili ya upimaji, je ni namna gani bora ya kuweza kununua kiwanja hiki ili kuepuka migogoro ya umiliki ambayo inaweza kuja kujitokeza baadae?
 
Wataalam watakuja kuweka sawa, ila kama makaratasi yako vizuri ya mauziano na hatua za kupima hazijaanza, ni vizuri kwenda kwa hiyo kampuni ili jina lako ndio lisomeke kuanzia hatua za awali kabisa za upimaji. Ukiacha hati ikatoka kwa jina lake mchakato wa kubadili umiliki wa ardhi sio mwepesi.
 
  • Thanks
Reactions: vvm
Back
Top Bottom