Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

"Ndevu za mahindi"

Chemsha hizo ndevu iwe kama chai

Bilauli moja asubuhi moja jioni (lets say saa mbili asubuhi na saa kumi na mbili jioni)

Inasaidia kukaza misuli ya "sphinta" .

Pia saa tano usiku jitahidi akojoe chooni, na saa tisa usiku.

Fanya hivyo kwa wiki mbili utaanza kuona mabadiliko, endelea hadi wiki sita.
 
"Ndevu za mahindi"

Chemsha hizo ndevu iwe kama chai

Bilauli moja asubuhi moja jioni (lets say saa mbili asubuhi na saa kumi na mbili jioni)

Inasaidia kukaza misuli ya "sphinta" .

Pia saa tano usiku jitahidi akojoe chooni, na saa tisa usiku.

Fanya hivyo kwa wiki mbili utaanza kuona mabadiliko, endelea hadi wiki sita.
Hii ya ndevu za mahindi nilishawahi isikia... Jaribu hii sambamba na zoezi la keagel muscle ulilotajiwa..la kumtrain kucontrol flow..pia kumuamsha usiku saa tano, saba na tisa/kumi hapo.
 
Miaka 9 ishu? Embu pitia hapa uone watu waliolishsusha mpaka 18+

 
Nina Mdogo wangu wa Kiume sasa Ana Miaka 18 na Yupo Kidato cha nne Sasa anatarajia kufanya Mtihani wa Taifa, tatizo lake ni moja Anakojoa Kitandani Toka utotoni.

Ametumia dawa za Kienyeji hadi tushachoka, kapelekwa kwa Wachungaji kaombewa lakini hakuna Mabadiliko.

Hii imekuwa ikimnyima Uhuru hasa akiwa ugenini hulazimika hata kulala Chini au kutokusafiri kabisa hata kwenda kutembelea Ndugu wakati wa likizo.

Ameshauriwa hata kutokunywa maji kabisa Jioni au Baada ya chakula cha Usiku Lakini Bado Haijasaidia.

Msaada Tafadhali.
 
Kuwa kikojozi sio ugonjwa. Ukiachana na watoto, hawa wakubwa Wengi wao wana asili ya uvivu wa kuamka na uoga wa kutoka chumbani usiku na kwenda chooni, maana wengi wetu hatulali kwenye vyumba vyenye choo chumbani. Mimi binafsi najikumbuka kabisa nilikuwa Kikojozi mzuri tu hadi nikiwa darasa la saba.

Nilisaidiwa mbinu za kuamka na Baba yangu baada ya kuninunulia simu. Alikuwa anahakikisha kabla ya kwenda kulala nishaenda chooni na alikuwa ananiwekea alam niwe naamka saa 5:00 usiku, 8:00 na saa 11:00 na kwa kuwa alinijua ni muoga wa kutoka chumbani usiku alinipa chombo niwe kakaa nacho chumbani.

Baada ya miezi mitatu akanibadilishia muda nikawa naamka mara mbili, baada ya muda akatoa zile alam. Nikajikuta naamka asubuhi nikiwa sijafanya utundu wangu.
 
Mkuu kuna uzi wa vikojozi humu utafute uusome wala hautahangaika tena. Kifupi tu hakuna dawa ya kuacha kukojoa ila ataacha automatically. Wengi kwenye huo uzi waliacha tu bila dawa vuta subra.
 
Nina bint wa miaka 9 ila ana tatizo la kukojoa kitandani, yaani anaweza kukojoa hata mara mbili kwa usiku mmoja. Pia hata mchana akilala anaweza akakojoa pia.

Msaada please.
 
Back
Top Bottom