Msaada mtu mzima kukojoa kitandani

swahiba92

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2016
Messages
2,029
Points
2,000

swahiba92

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2016
2,029 2,000
Nina Mdogo wangu wa Kiume sasa Ana Miaka 18 na Yupo Kidato cha nne Sasa anatarajia kufanya Mtihani wa Taifa, tatizo lake ni moja Anakojoa Kitandani Toka utotoni.

Ametumia dawa za Kienyeji hadi tushachoka, kapelekwa kwa Wachungaji kaombewa lakini hakuna Mabadiliko.

Hii imekuwa ikimnyima Uhuru hasa akiwa ugenini hulazimika hata kulala Chini au kutokusafiri kabisa hata kwenda kutembelea Ndugu wakati wa likizo.

Ameshauriwa hata kutokunywa maji kabisa Jioni au Baada ya chakula cha Usiku Lakini Bado Haijasaidia.. Msaada Tafadhari.
 

Vuitton

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2016
Messages
345
Points
500

Vuitton

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2016
345 500
WAKUU NAHITAJI MSAADA.

Nina Mdogo wangu wa Kiume sasa Ana Miaka 18 na Yupo Kidato cha NNE Sasa anatarajia kufanya Mtihani wa Taifa.. Tatizo lake ni moja Anakojoa Kitandani Toka utotoni. Ametumia Dawa za Kienyeji hadi Tushachoka, kapelekwa kwa Wachungaji kaombewa lakini hakuna Mabadiliko..

Hii imekuwa ikimnyima Uhuru hasa akiwa ugenini hulazimika hata kulala Chini au kutokusafiri kabisa hata kwenda kutembelea Ndugu wakati wa Likizo, Ameshauriwa hata kutokunywa maji kabisa Jioni au Baada ya CHAKULA cha Usiku Lakini Bado Haijasaidia.. Msaada Tafadhari..

Nawasilisha.
Pole Sana mkuu
 

KANYIMBI

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Messages
519
Points
500

KANYIMBI

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2011
519 500
Kuwa kikojozi sio ugonjwa. Ukiachana na watoto, hawa wakubwa Wengi wao wana asili ya uvivu wa kuamka na uoga wa kutoka chumbani usiku na kwenda chooni, maana wengi wetu hatulali kwenye vyumba vyenye choo chumbani. Mimi binafsi najikumbuka kabisa nilikuwa Kikojozi mzuri tu hadi nikiwa darasa la saba. Nilisaidiwa mbinu za kuamka na Baba yangu baada ya kuninunulia simu. Alikuwa anahakikisha kabla ya kwenda kulala nishaenda chooni na alikuwa ananiwekea alam niwe naamka saa 5:00 usiku, 8:00 na saa 11:00 na kwa kuwa alinijua ni muoga wa kutoka chumbani usiku alinipa chombo niwe kakaa nacho chumbani. Baada ya miezi mitatu akanibadilishia muda nikawa naamka mara mbili, baada ya muda akatoa zile alam. Nikajikuta naamka asubuhi nikiwa sijafanya utundu wangu.
 

charrote

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2017
Messages
893
Points
1,000

charrote

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2017
893 1,000
Mkuu kuna uzi wa vikojozi humu utafute uusome wala hautahangaika tena. Kifupi tu hakuna dawa ya kuacha kukojoa ila ataacha automatically. Wengi kwenye huo uzi waliacha tu bila dawa vuta subra.
 

Forum statistics

Threads 1,366,664
Members 521,539
Posts 33,375,053
Top