Msaada, mtoto wangu anaweza kupata ulemavu kutokana na uzembe wa madaktari wetu

CalvinD

JF-Expert Member
Feb 5, 2016
243
347
Wakuu naandika huu uzi nikiwa na majonzi makubwa sana, naomba niende moja kwa moja kwenye mada
mwezi wa 8 tarehe 15 mke wangu alijifungua kwa shida sana katika hospitali ya serikali kwa njia ya mkasi, kutokana na uzembe wa madaktari kuchelewa kumfanyia operation kwa haraka, mtoto alimeza maji mengi akazaliwa akiwa ame acore below average(wale wenye uzoefu wanaelewa).mtoto akawekwa ICU kwa muda wa wiki moja baadae wakamruhusu atoke hospital.

Kinachoniuma zaidi ni kwamba mtoto amepata athari kwenye ubongo wake hali itakayopelekea kupata matatizo katika makuzi yake , siku nne zilizopita mtoto alikua analia sana usiku tukaenda hospital ya private kufanya check up.

Dokta akatuambia mtoto aliruhusiwa mapema kutoka kabla ya kufanyiwa uchunguzi wa kina
Wakuu roho inaniuma sana nikifikiria mtoto wangu anaweza kupata ulemavu kutokana na uzembe wa madaktari wetu, naombeni ushauri wakuu kama kuna njia yoyote ya kumnusuru mwanangu kutokana na haya majanga.

Niko tayari kusikiliza ushauri wenu.
 
Du,,pole sana. Yani Tanzania bado sana,,napata uchungu sana nikiskia hizo habari.

Ngoja wataalamu waje na wengine tupate maarifa
 
Sijajua shida ipo wap watu wenye taaruma zao kufanya uzembe wa namna iyo....

Kuna vitu vinauma kias kwamba ukivisikia unaweza kufa kwa presha

Jaribu kuvaa viatu vya mhusika....
 
Emotions n mbaya sana....mzgo walionao wafanyakaz wa afya n mkubwa kulko hata inavodhaniwa,huenda n kweli uzembe wao ukawa ulichangia hali ya mwanao lkn kwa upande mwngne huenda sio uzembe bali n kutokana na kuelemewa na majukumu ya kuhudumia wagonjwa wengi ilhali wao i.e madokta wakiwa n wachache...hakuna daktari anayependa mgonjwa wake asipone ila hali ya nchi zetu na mazingira mabovu ya kazi huchangia mambo kama haya...pole sana mkuu ,nakushaur umpeleke hospital nyngne huenda akapatiwa tiba ila punguza emotions japo inauma
 
Back
Top Bottom