Msaada: Mtoto wangu ana tabia ya kupiga wageni na kusema 'toka kwetu'

Haa🙄🙄 kwan akilia analia damu, kitu anachokifanya siyo kizuri mkataze2 alf Jenga tabia ya kumpa chakula mapema tofauti na mgeni
 
Daah!! Hataree hiyo mtoto umleavyo ndivyo akuavyo maandiko yanasema usimnyime mtoto mapigo ukimuadhibu siku ya kwanza na ya pili atajua kua analofanya ni kosa usixeme inakuudhi na huja take any action broo
 
Hii sio tabia ya mtoto, ni uzembe na ujinga wa wazazi. Kuna umri ukiongea mtoto anasikiliza na anafanya.

Mnaleta uzungu mwingi kwenye malezi ya watoto ndio mnawaharibu. Chukua kiboki, tia viwili harudii tena.

Ikitokea amejisahau akarudia, tia tena vingine viwili na mlazimishe amwombe mgeni msamaha ndipo mambo yaende sawa. Acheni kuharibu watoto.
 
Tandika bakora mtoto adabu yake imekunjika hiyo inatakiwa kunyooshwa. Lakini pia mkanye na kumuelekeza namna ya kuongea na wageni.
 
Mkanye mwanao hiyo si tabia njema. Mi nikija akiniambia hivyo ukijipindua tu nampa signal kali sana ikiwezekana na kifinyo juu
 
Enzi zetu tulikuwa tunafukuzwa mbali na wazazi wetu ili tusiropoke neno la kumkera mgeni na kuaibisha wazazi. Hatukuzengeazengea wageni hata kidogo
 
Samaki mkunje angali mbichi, "UKIMKEMEA ANALIA" baada ya kulia unamuacha, ataendelea hivohivo kwasababu ndio njia uliyomchagulia
 
Kama unavyosema kwamba ukimzuia anaanza kulia, Mm nashauri pale pale pitisha adhabu ya viboko ili akinyama ajue amedhibiwa kwa kosa gani.
Sio anafanya kosa, ukimzua analia then ww tena ndo unambembeleza.
 
Hio tabia atakua ameiga kwenu nyoe ndio chanzo anzeni kusali sala ya bwana mar kumi mkimshirikisha usikukabla ya kula / kulala
 
Habari wakuu,

Nina mtoto wangu wa kiume wa miaka 3. Ni miezi kama miwili sasa ameanza tabia isiniyopendeza, kila akija mgeni especially wakati wa kula atamfukuza mgeni toka kwetu, wacha kula chakula chetu. Nikimkemea analia kilio kama kapigwa.

Juzi nilijisikia aibu sana alipompiga mgeni na fagio wakati wa kula, ni baada ya mgeni kukaidi agizo lake la toka kwetu.

Naomba msaada wakuu jinsi ya kumsaidia mtoto wangu kutoka kwenye tabia hii chafu.
Ana Tabia ya wazazi wake.
 
Mpe huyo mtoto maua yake naona ana tabia kama zangu nikiwa mtotoni
 
Back
Top Bottom