Msaada: Mtoto wangu ana tabia ya kupiga wageni na kusema 'toka kwetu'

mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
10,518
19,883
Habari wakuu,

Nina mtoto wangu wa kiume wa miaka 3. Ni miezi kama miwili sasa ameanza tabia isiniyopendeza, kila akija mgeni especially wakati wa kula atamfukuza mgeni toka kwetu, wacha kula chakula chetu. Nikimkemea analia kilio kama kapigwa.

Juzi nilijisikia aibu sana alipompiga mgeni na fagio wakati wa kula, ni baada ya mgeni kukaidi agizo lake la toka kwetu.

Naomba msaada wakuu jinsi ya kumsaidia mtoto wangu kutoka kwenye tabia hii chafu.
 
Kila akipiga wageni makofi kamnunulie zawadi nzuri na fanya party kubwa na ualike wageni (akiwemo yule aliyepigwa konzi) na umpongeze mwanao.

Maana anafanya Jambo zuri kupitiliza, usisikilize watu wanasema Nini kuhusu wewe. Hao watakua wanamuonea wivu mwanao.

Nirudie Tena kukupongeza, Hongera Mama Junior
 
Ki ukweli miaka ya 2030's kutakua na kizazi kibovu sana kinachotengenezwa na wazazi ambao hawajui majukumu yao kwa watoto. Simlaumu huyo wako ila mitoto mingi siku hizi kauli zao ni balaa.

Hadi vitabu vya dini vimezungumzia hilo kuwa mtoto anachapwa akileta ujinga. Sa endele fuga uzembe.. Kuna kipigo cha kumpa maumivu na sio kumuumiza ambacho ukimpatia yaani hata jaribu huo utumbo wake
 
Ki ukweli miaka ya 2030's kutakua na kizazi kibovu sana kinachotengenezwa na wazazi ambao hawajui majukumu yao kwa watoto. Simlaumu huyo wako ila mitoto mingi siku hizi kauli zao ni balaa.

Hadi vitabu vya dini vimezungumzia hilo kuwa mtoto anachapwa akileta ujinga. Sa endele fuga uzembe.. Kuna kipigo cha kumpa maumivu na sio kumuumiza ambacho ukimpatia yaani hata jaribu huo utumbo wake
Mkuu mtoto wa miaka 3 bado anajifunza,,na kupiga sio Dawa,,natafuta njia sahihi ya kumfunza,,kama kumchapa nachapa kiasi ,,lakini bado haachi...
 
Inaonekana kuna shida ya menu hapo kwako...Hakikisha mtoto anakula vzur.mazaga yote...wengne watoto wetu hata umwekee mikuku hapo sana snaa atalamba lamba tu na kuacha..yaan mtalazimishana kula..

Sasa ukiona mtoto anakua mchoyo hvo ujue kuna tatzo la menu hapo.

Samahan lakin...
 
Samaki mkunje angalia mbichi, inabidi fanya kinachowezekana abadilike kitabia kabla hajakuwa zaidi ya hapo...huna haja ya kusubiri ushauriwe juu ya adhabu au jinsi ya kulea mwanao...
Natanguliza samahani Kama nimekukwaza🤔🤔🤔🤔
 
Hayo maneno makali kuwaambia wageni atakuwa kayapata kwenu kwamba hamtaki wageni hasa wakati wa kula hivyo dogo kajiongeza. Kikubwa acheni kusengenya wageni wanaokuja kuwatembelea. Kuhusu dogo kila akizingua muadhibu mbele ya mgeni akili itamkaa sawa.
Mkuu ukiwa unatabia ya kwenda nyumba fulani fulani kama ni kwa ndugu zako au boss wako...ukitaka kujua hao wenyeji wako wanakuongeleaje/wanakuchukuliaje kipindi haupo wewe cheza na saikolojia za watoto katika nyumba hiyo utapata majibu bila kujali wenyeji wako wanakuonyesha tabasamu la upana gani wakikuona.
 
Back
Top Bottom