Msaada: Mtoto mchanga wa mwezi mmoja hajawahi kulia

Mtoto anakaribia kufikisha mwezi toka azaliwe lakini hajawahi hata kulia wala kusema. Nini tatizo? Tumejaribu hosptali nyingi wanasema hana tatizo!

Msaada.
Mkuu vipi dogo natumaini atakua amekua, je mliweza kuwaona madaktari na kupata suluhisho lolote? Nitashukuru kwa feedback
 
Kuna mtoto wa dada yangu alikua hafanyii chochote anatulia tu, mpaka ameanza kukaa akiwekwa sehemu anaweza kaa siku zima bila movement yoyote au kulia.

Siku moja nilichukua kijiko nikasagia pilipili afu nikamlambisha, alilia kwa mara ya kwanza na akaanza kuwa active though baadae akaja gundulika ana down syndrome.

semper fidelis
 
Mtoto anakaribia kufikisha mwezi toka azaliwe lakini hajawahi hata kulia wala kusema. Nini tatizo? Tumejaribu hosptali nyingi wanasema hana tatizo!

Msaada.
Ameruhusiwaje kutoka hospitali na tatizo hilo? Mama mzazi huwa haruhusiwi kutoka hadi kuwe na utatuzi wa hiyo changamoto
 
Pole sana ...angalia udata ni kinyama kinachoungana na ulini mtoto akilia hauinuki. Maana mtoto anatakiwa awe Amalia na baada ya wiki 2 (14) akilia anatakiwa awe anatoa machozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kama hospital zote mlizoenda wamesema hana tatizo kwwnn mnalazimisha kuambiwa ana matatizo?

Hamuamini? Kwanini ?...
Wewe kaka mwanao angekuwa na hii shida ungekaa kimya na kuamini kuwa hana tatizo? hospital zetu huwa zina mtindo wa kukwambia tatizo baadae sana huku umeshapoteza muda wa kumshughurikia mapema..

Hili tatizo sio la kawaida kwa mtoto, mtoto lazima acheze na kuongea hata kama anachoongea hakieleweki.
 
....Japo ushapita hospitali nyingi, na km bado unahisi mtoto ana tatizo...ushauri wangu ni kwamba fanya appointment na daktari bingwa wa watoto(pediatrician) km upo dar es salaam itakuwa rahisi kuwapata kwenye clinic zao au hospital kubwa km muhimbili,aga khan, kairuki, hindu mandar....point yako iwe kuonana na daktari bingwa moja kwa moja amuangalie mtoto pia akuelezee yy anaona kwa nn mwanao hajawahi lia toka kazaliwa uandikiwe na full medical report!!
Best Professional Advise
 
Mimi wangu alikuwa balaa ..ikashafika saa 5 usiku..ni kilio mpaka saa 11 alfajiri...full kukesha..ikifika saa 12 morning dogo anachapa usingizi kiroho safi kabisa...hapo mtumzima macho yamenivimba natakiwa kwenda kibaruani hapo...kulea siyo lelemama...
 
Kuna mtoto wa dada yangu alikua hafanyii chochote anatulia tu, mpaka ameanza kukaa akiwekwa sehemu anaweza kaa siku zima bila movement yoyote au kulia. Siku moja nilichukua kijiko nikasagia pilipili afu nikamlambisha, alilia kwa mara ya kwanza na akaanza kuwa active though baadae akaja gundulika ana down syndrome.

semper fidelis
dah we jamaa ni psychopath ah ah dah sio poa
 
dah we jamaa ni psychopath ah ah dah sio poa
Haha haaaaa huwez amin from that material day mtoto amkekua active japo ana hilo tatizo lake. Kipindi namlambisha pilipili alikua chini ya miaka 2, sasa ana 7.

semper fidelis
 
Kwani kama hospital zote mlizoenda wamesema hana tatizo kwwnn mnalazimisha kuambiwa ana matatizo?

Hamuamini? Kwanini ?..

Ishu ni kwamba, mtoto kulia ni dalili njema..., pia kwa umri huo kuwa hajawahi kulia si dalili nzuri. So kuambiwa hana tatizo ni kitu kimoja, lakini kwa nini hajawahi kutoa sauti ni jambo lingine.

Kwa wazazi/walezi wengi tungehangaika kama yeye. Pole mkuu, naamini kitengo cha watoto Muhimbili wana msaada kwenye hili, maana hata watoto ambao ni bubu au wenye kigugumizi huwa wanalia pia.
 
Back
Top Bottom