Msaada: Mtoto mchanga wa mwezi mmoja hajawahi kulia

Bengazuu

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
1,029
1,236
Mtoto anakaribia kufikisha mwezi toka azaliwe lakini hajawahi hata kulia wala kusema. Nini tatizo? Tumejaribu hosptali nyingi wanasema hana tatizo!

Msaada.
 
Dah!! Kwa Dar hapa hospital nyingi mkuu labda hilo la kuangaliwa ulimi na wazee
 
Kwani kama hospital zote mlizoenda wamesema hana tatizo kwwnn mnalazimisha kuambiwa ana matatizo?

Hamuamini? Kwanini?

Ndio maana hospital nyingi huwa wanatuibia sana, ukienda ukaambiwa huna tatizo unasema hii Hosp feki unaenda nyingine lakini tukiambiwa tuna marelia hata kama hatuna labda ni uchovu tu au stress za kazini tunaona hii ndio hospitali sasa! Tunalipa Malaki na malaki.

Ingekuwa umeenda hospital moja sawa ni haki yako kuwa na mashaka ila unasema hospital nyingi tu na wote jibu hilo hilo hana tatizo, relax Mkuu amini hana tatizo!

Utakonda bure
 
Tatizo hatujui kwanin halii na hospital wanasema mtoto yuko vizuri hana shida
 
...Japo ushapita hospitali nyingi, na kama bado unahisi mtoto ana tatizo...ushauri wangu ni kwamba fanya appointment na Daktari bingwa wa watoto (pediatrician)

Kama upo Dar es salaam itakuwa rahisi kuwapata kwenye clinic zao au hospital kubwa km muhimbili,aga khan, kairuki, hindu mandar...

point yako iwe kuonana na daktari bingwa moja kwa moja amuangalie mtoto pia akuelezee yy anaona kwa nn mwanao hajawahi lia toka kazaliwa uandikiwe na full medical report!!
 
Hata zingine hatoi
Kama hajawahi kutoa sauti yoyote hapo kwakweli lazima mzazi uwe na shaka. Kutoa sauti ni dalili ya kukusaidia wewe mzazi kuelewa kama ana tatizo lolote au laa.

Nakushauri uonane na daktari bingwa wa watoto. Hata kama halii basi awe anatoa hata sauti ya kucheka au vyovyote vile.
 
Kama hajawahi kutoa sauti yoyote apo kwakweli lazima mzazi uwe na shaka. Kutoa sauti ni dalili ya kukusaidia wewe mzazi kuelewa kama ana tatizo lolote au laa. Nakushauri uonane na daktari bingwa wa watoto. Hata kama halii basi awe anatoa hata sauti ya kucheka au vyovyote vile.
Asante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom