Msaada: Mtoto kajigonga kwenye gari na kufariki, wazazi hawataki kesi, traffic wanataka kesi

Ukikosa Mens rea& Actus Rea katika Scenario yoyote ile ni ngumu ku establish bases ya case theme yako.? Kukiwa na state of mind na Kitendo kilichofanya kosa liwepo ni Easy kuanzisha investigation ya such an offence
Ngoja nikurudishe darasani mkubwa kuna kitu kinaitwa Strict liability haya ni makosa ambayo hayahitaji kuthibitisha mens rea (nia ovu) Actus Reus tu inatosha mtu kushitakiwa/kutiwa hatiani na makosa ya usalama barabarani yana angukia hapo
 
DEREVA KAPAKI GARI KASEPA ZAKE YEYE DOGO KAJIPIGA KWENYE GARI LIKIWA NDANI HAKUNA DEREVA HAPO INAKUAJE MAHAKAMA YA NINI?

Ewe mtanzania: ndiyo sababu kuna kitu kinaitwa upelelezi na uchunguzi wa tukio (Investigation at the crime scene). Kama polisi wamechunguza na wanaona wana ushahidi wa kupeleka kesi Mahakamani ni lazima wapeleke.

Mahakama ndiyo mwamuzi wa mwisho, itatamka kama ushahidi unamtia hatiani dereva au hapana. Kama hautoshelezi ataachiwa huru na kurudi nyumbani kwake kuendelea na maisha.

Mnapata wapi U-mungu wa kujiamlia tu kuwa hakuna kesi?! Umeshawahi kujiuliza kwanini kuna polisi na Mahakama?
 
Kwa Mungu kila kitu kinawezekana;pengine alijigonga kwa kunguvu akapasuka bandama au guvu la kichwa,hapo ajabu iko wapi?
 
Ana miaka mingapi? Kujigonga vipi huko? Gari ina ncha Kali? Napata wakati mgumu wa kuelewa!!
 
Kama wazazi wa mtoto hawataki kesi iendelee nadhani hata ikienda mahakamani hao wazazi wanaweza kuwithdraw kesi. ( Not sure though)

Lakini pia nafikiri Jamhuri itataka kujua hapo ulipokuwa umepata gari ni salama, panaruhusiwa?

Lakini pia wahusishe insurance ili wakupe legal view Incase hao wazazi wakiamua wanataka fidia.
Kesi hipo! Yawezekana jamaa alipaki sehemu hisiyoruhusiwa,! Mahakama ndio itaamua, kama kuna jinai imetendeka au la!
 
Police wanayo haki kisheria kupeleka hiyo kesi mahakamani. Wao wanachotakiwa kufanya ni kufanya upelelezi wa kilichotokea, ilikuwaje mtoto ambaye siyo 'udongo' ajigonge tu na kufa!?

Lazima wachunguze je huyu mtoto hakugongwa na mwenye gari? Wazazi hawajapewa rushwa kweli kupotezea haki ya uhai wa mtoto!? Na kikubwa zaidi polisi watachunguza kubaini uwepo wa jinai kwenye hicho kifo. Ni kazi ya serikali kulinda usalama wa raia na mali zao, hivyo basi si kazi ya mzazi kujifanya eti yeye hataki kesi! HANA MAMLAKA HAYO, HIYO NI KESI YA JAMHURI NA DEREVA WA GARI HUSIKA.

Hivyo basi polisi wakipata ushshidi wanaotaka, wakibaini kuna kesi ya msingi, ngoma inapelekwa Mahakamani. Huko ndipo dereva utaelezea vizuri gari yako huwa unaipaki vipi kiasi kwamba binadamu akijigonga tu anakufa hapohapo.
Hapo ambae hajakuelewa anataka tu ubishi au anatakakuelewa zaidi.

Kelesya: in other way around, vipi kama umempeleka mtuhumiwa police kwa kosa la jinai alafu mpelelezi anachukuwa muda mrefu kupeleleza na hawasiliani na mlalamikaji zaidi ya wiki mbili je, upelelezi anaufanya mwenyewe bila kumshirikisha mlalamikaji ambae atakuwa kama shahidi mahakamani?, na je, kunamuda maalum ambao mpelelezi ni lazma awe amepeleka kesi mahakamani?. Tafadhali.
 
Katika hali ya kawaida.....watoto wana maeneo ambayo wanameyazoea kukusanyika.......

Inawezekana kwako ni moja ya maeneo yanayowavutia watoto kucheza......hivyo ungetakiwa uwe makini kwenye ku park......

Inawezekana sehemu uliyopaki siku hiyo si ambapo ulizoea kupark kila siku....na huku akili za watoto zikiwa na taswira kuwa hapo hakuna gari.....ndio maana watoto wakawa huru kucheza.....

Polisi wanaweza wakaanzia uchunguzi wa kwanini wazazi wa marehemu watoe maamuzi ya haraka kabla mambo hayajafika kwenye vyombo husika......
 
Wape hela tu hao trafiki maana hii kesi itakushinda hata kama huna hatia. Hujui kujieleza kwa ufasaha hivyo hata msaada utakaopata hapa utakuchanganya. Siku nyingine fafanua vizuri ili usaidiwe. Mfano:
  1. Gari ulipaki wapi? (Nyumbani, pembeni ya barabara, shuleni, uwanjani, nk)
  2. Ulipaki mahali panaporuhusiwa kisheria?
  3. Ulikuwa wapi wakati mtoto huyo anajigonga kwenye gari yako (inawezekana hiyo unaposema gari ilipaki unamaanisha uliweka 'P' wakati upo ndani ya gari)
  4. Mtoto alikuwa anatumia usafiri gani? Alikuwa katika hali gani? Anatembea? Anakimbia? Amepanda baiskeli/pikipiki?
  5. Ulichukua hatua gani baada ya ajali kutokea?
  6. Askari wanataka wapeleke kesi mahakamani wakikutuhumu kwa kosa gani?
  7. Gari lako lipo ktk hali ya kutembea barabarani? (Bima, Motor vehicle licence, driving licence)
Hapo ndipo watu wanaweza wakakusaidia. Unaweza kutaja vyote hivyo bila kuwa specific (kutaja majina ya sehemu au watu) na hivyo kutoathiri mwenendo wa kesi.
 
Hapo ambae hajakuelewa anataka tu ubishi au anatakakuelewa zaidi.

Kelesya: in other way around, vipi kama umempeleka mtuhumiwa police kwa kosa la jinai alafu mpelelezi anachukuwa muda mrefu kupeleleza na hawasiliani na mlalamikaji zaidi ya wiki mbili je, upelelezi anaufanya mwenyewe bila kumshirikisha mlalamikaji ambae atakuwa kama shahidi mahakamani?, na je, kunamuda maalum ambao mpelelezi ni lazma awe amepeleka kesi mahakamani?. Tafadhali.

Hapo kuna tatizo (uzembe au rushwa kwa mpelelezi wa kesi). Kama mtuhumiwa anajulikana na ameshitakiwa na mlalamikaji, na mlalamikaji ushahidi na mashahidi wengine upo/wapo. Na kosa likaonekana ni jinai kweli kinyume na vifungu vya Sheria za makosa ya jinai inapaswa mtuhumiwa afikishwe Mahakamani haraka sana.

Haiwezekani katika hali ya kawaida mpelelezi kufanya upelelezi bila kuwasiliana na mlalamikaji ambaye "ndiye shahidi namba moja wa upande wa mashitaka/Jamhuri! Hawa wawili ni lazima washirikiane kuweka ushahidi sawa na kurahisisha kesi yao.

Mpelelezi, Mwendesha mashitaka na Mlalamikaji hawa wote ni team moja ya "mashitaka/prosecution.

Uzuri ni kwamba kesi ya jinai haifi, hata ikae muda gani. Onana na viongozi wa huyo mpelelezi uwaeleze tatizo la ucheleweshaji unaofanyika. Na ikibidi wakupangie mpelelezi mwingine ili kesi iende Mahakamani. Jamhuri ikishinda kesi ya jinai na wewe utaweza kufungua kesi ya madai kwa hasara na madhara uliyopata kutokana na jinai husika.
 
Mtoto ameumia kwa ajali ya gari kwa kujigonga ubavuni gari imepaki. Bahati mbaya amekufa. Wazazi wanasema hatutaki kesi ni kosa la mtoto. Polisi wamekomaa wanataka wapeleke mahakamani. Je sheria inasemaje wadau
Sema ukweli pia umegharamia mazishi kwa kutoa jeneza, sanda, chakula msibani na pengine ulishiriki matibabu. Hiyo ni takrima.

Kisheria wazazi hawana ubavu wa kuzuia kesi isiende mahakamani, maana hata ushahidi wao siyo mhimu sometimes.

Busara ya Polisi kupeleka mahakamani ni ili jambo liishe kisheria, sio kindugu, maana baadhi ya wanandugu, baadae hugeuka, na kutuhumu polisi kula rushwa hadi kushindwa kupeleka kesi mahakamani.

Tena wanandugu wengine huanzia malalamiko yao kwa waziri, Ijp, rpc, na ni wakati wamepata elimu kuwa kama kesi ingeenda mahakamani, wangelipwa pesa nzuri na bima.

Hivyo usiwaamini sana wananchi, wanageuka na wanasahau kila kitu.

Niliwahi kuona mfano wa hili, dereva wa coca aligonga mtembea kwa miguu akafa. Kupitia ofisi, wakatoa milioni moja na gunia kadhaa za mchele kuhudumia msiba. Na ndugu wakasema hawana sababu ya kwenda mahakamani. Baada ya miaka sita, baadhi ya ndugu wakafundishwa kuwa, kama ingeenda mahakamani, wangelipwa fidia na bima maana magari yana bima.

Sasa wakajipanga namna gani ya kufufua kesi? Wakaona njia rahisi ni kuwalalamikia polisi kula rushwa wakashindwa kupeleka kesi mahakamani.

Na kesi ilisikilizwa, ya miaka sita iliyopita. Unaona usumbufu wake?
 
Dereva yupi wakati gari limepaki??? Nilidhani itakuwa kesi ya Jamhuri Vs Mwenye gari.
Bwana tembe za kidonge buana, Asprin, tambua kuna makosa ya dereva na makosa ya mmiliki. Wrong parking kwa mfano ni la dereva, lkn gari chakavu lenye tetenasi ni mwenye gari
 
Kama maelezo yako ni kweli basi utashinda kesi...ondoa hofu

kwakuwa mtoto kajigonga kama ambavyo angeanguka chooni ama kujigonga ukutani
Hata kama siyo kweli, kesi za traffic ni upuuzi mtupu. Hata akishindwa kesi, faini kubwa ni tsh. 50,000/-
 
Haya mambo yanahitaji upelelezi usikurupuke kutoa majibu mapesi kama hujui haudhuriki ukikaa kimya hiyo ni ajali kama ajali zingine hata kama kajigonga mwili wa marehemu lazima ufanyiwe uchunguzi hivyo lazima jalada la uchunguzi lifunguliwe pia yawezekana hata gari lilipaki eneo lisilo stahili acha kesi ifunguliwe ili kupata ukweli na huo ndo utaratibu
Kuna kipindi tunawachukia polisi kwa kutokujua kwetu. Yaani mtu haamini kama kesi kwenda mahakamani ni kumsafisha yeye mwenyewe asionekane alisababisha kifo hicho. Ujinga ni mzigo
 
Kesi hipo! Yawezekana jamaa alipaki sehemu hisiyoruhusiwa,! Mahakama ndio itaamua, kama kuna jinai imetendeka au la!
Mkuu andika kiswahili, unanichanganya. Hivi neno 'ipo' na 'hipo' ni sawa? Hafu unakuta ni watu wa pwani ndo wanaandika hivi
 
Hapo ambae hajakuelewa anataka tu ubishi au anatakakuelewa zaidi.

Kelesya: in other way around, vipi kama umempeleka mtuhumiwa police kwa kosa la jinai alafu mpelelezi anachukuwa muda mrefu kupeleleza na hawasiliani na mlalamikaji zaidi ya wiki mbili je, upelelezi anaufanya mwenyewe bila kumshirikisha mlalamikaji ambae atakuwa kama shahidi mahakamani?, na je, kunamuda maalum ambao mpelelezi ni lazma awe amepeleka kesi mahakamani?. Tafadhali.
Ushahidi ukikamilika ndio kesi inaenda mahakamani. Kama kesi haidhaminiki polisi, kesi inaweza pelekwa mahakamani, halafu ikawa inatajwa huku wanasema ushahidi bado kukamilika. Hakuna muda maalumu wa kukamilisha ushahidi
 
Mkuu andika kiswahili, unanichanganya. Hivi neno 'ipo' na 'hipo' ni sawa? Hafu unakuta ni watu wa pwani ndo wanaandika hivi
Usiusishe watu wa pwani na uandishi wa ajabu,pia usiusiche watu wote.
 
Hapo kuna tatizo (uzembe au rushwa kwa mpelelezi wa kesi). Kama mtuhumiwa anajulikana na ameshitakiwa na mlalamikaji, na mlalamikaji ushahidi na mashahidi wengine upo/wapo. Na kosa likaonekana ni jinai kweli kinyume na vifungu vya Sheria za makosa ya jinai inapaswa mtuhumiwa afikishwe Mahakamani haraka sana.

Haiwezekani katika hali ya kawaida mpelelezi kufanya upelelezi bila kuwasiliana na mlalamikaji ambaye "ndiye shahidi namba moja wa upande wa mashitaka/Jamhuri! Hawa wawili ni lazima washirikiane kuweka ushahidi sawa na kurahisisha kesi yao.

Mpelelezi, Mwendesha mashitaka na Mlalamikaji hawa wote ni team moja ya "mashitaka/prosecution.

Uzuri ni kwamba kesi ya jinai haifi, hata ikae muda gani. Onana na viongozi wa huyo mpelelezi uwaeleze tatizo la ucheleweshaji unaofanyika. Na ikibidi wakupangie mpelelezi mwingine ili kesi iende Mahakamani. Jamhuri ikishinda kesi ya jinai na wewe utaweza kufungua kesi ya madai kwa hasara na madhara uliyopata kutokana na jinai husika.
Asante kalesya, nimekupata vizuri sana.
 
Back
Top Bottom