Msaada mtoto kaanguka kwenye tiles (Marumaru) naomba kujuzwa huduma ya kwanza

Tuchki

JF-Expert Member
Feb 1, 2017
1,740
1,435
Ndugu naombeni mnisaidie nifanyaje,

Nina ndugu yangu ana mtoto wa miezi Sita leo ameanguka kutoka kwenye kochi mpaka kwenye tiles na kaangukia kisogo mama yake hajiwezi Kwa kilio niko hapa na mtoto sijui nimpe huduma gani ya kwanza maana saa zima mtoto analia tu bila kunyamaza
 
Mungu ni mwema atakua sawa, hata hivyo kama ana zile syrup kama kama paracetamol anaweza kumpa apunguze maumivu, then mpeleke hospitali kwa uchunguzi zaidi, Atakua sawa. kwa watoto inatokea sana hiyo.
 
Ndugu naombeni mnisaidie nifanyaje Nina ndugu yangu ana mtoto wa miezi Sita leo ameanguka kutoka kwenye kochi mpaka kwenye tiles na kaangukia kisogo mama yake hajiwezi Kwa kilio niko hapa na mtoto sijui nimpe huduma gani ya kwanza maana saa zima mtoto Analia tuu bila kunyamaza
Kwa hiyo kama amedhurika atapona kwa hicho kilio anacholia mama yake?

Kama mnahisi kunatatizo kwa nini msimpeleke hospital kujiridhisha? Yaani lisaa lizima, mtoto kilio na mama kilio.
 
Ndio hasara ya usasa hii. Ingekuwa cement au udongo ingesaidia ila haya mavitu. Mpeni pain killers kisha mumuwaishe hospital kwa uchunguzi zaidi. Pole sana. Inabidi watoto wavae helment.
 
Kwa hiyo kama amedhurika atapona kwa hicho kilio anacholia mama yake?
Kama mnahisi kunatatizo kwa nini msimpeleke hospital kujiridhisha?
Yaani lisaa lizima, mtoto kilio na mama kilio.

Yani eti alimuacha mtoto kwenye kochi akaenda toilet anamwambia mtoto wa miaka saba amuangalie yani roho imeniuma sana mtoto amelia kilio cha ajabu hadi sauti haitoki
 
Yani eti alimuacha mtoto kwenye kochi akaenda toilet anamwambia mtoto wa miaka saba amuangalie yani roho imeniuma sana mtoto amelia kilio cha ajabu hadi sauti haitoki
Kama ni mkeo huyo kaka kuna shida..kwanza ilikuaje? Na kwanini akimbilie chooni? Alikua anafanya nini mpaka mtoto anaanguka? Au ngoja tuyaache hayo hayanihusu cha muhimu muwahishe mtoto hospitali.
 
Poleni apewe pain killers then apelekwe hospitali. I hope hajapata madhara zaidi ya kuumia labda na mshtuko tu wa kuanguka. Afterall umbali wa kochi hadi sakafuni sio mkubwa.

It's okay kwa mama kulia ameshtuka pia na it's very natural Mama kuhisi maumivu ya mwanae. Sioni sababu ya mama kulaumiwa... Alienda chooni, ila tu next time amlaze chini kwenye vile vigodoro vya watoto ni salama zaidi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukute aliyekuwa nae karibu alikuwa busy na smartphone akiperuzi Facebook,nimejisemea tu.

Ni vizuri kuwa makini sana kila step anayopitia mtoto kwa kumuweka sehemu sahihi kulingana na umri wake. Mf, miezi sita ndipo watoto hujifunza kujigeuza wenyewe so kama hayupo karibu mtu mzima ni vizuri muda wote mtoto akiwa peke yake atandikiwe chini kuepuka ajali kama hizi.
 
Inawezekana kweli ikawa hivyo.
Mana Kaka kama ni wazoefu wangeshakuwa na maamuzi kabla ya kuja huku mtandaoni na hata huyo mama asingekuwa analia muda wote huo kwani huwa inatokea sana hasa watoto wakiwa katika hiyo stage mana wanakuwa wanagaragara sana hivyo kudondoka si jambo geni hasa kama hana uangalizi.
 
Mungu ana maajabu yake, hakuna haja ya kushtuka sana, kwa kesi ya mtoto kuanguka na apelekwe hospitali kama ada tu kwa ajili ya kuchekiwa lakini kwa mtoto anaweza kuanguka umbali na asidhurike tofauti na mtu mzima ukianguka nusu ya umbali huo lazima udhurike.

ᵃʳᵉᵉᵐ
 
Mtoto ameanguka kwenye tiles na upo naye hapo unakimbilia JF kuomba ushauri badala ya kumuwahisha zahanati au hospitali, mitandao inatufanya tuwe jamii ya watu wapumbavu sana.
 
Mtoto ameanguka kwenye tiles na upo naye hapo unakimbilia JF kuomba ushauri badala ya kumuwahisha zahanati au hospitali, mitandao inatufanya tuwe jamii ya watu wapumbavu sana.

Nimechanganyikiwa jaman si kosa langu
 
Poleni apewe pain killers then apelekwe hospitali. I hope hajapata madhara zaidi ya kuumia labda na mshtuko tu wa kuanguka. Afterall umbali wa kochi hadi sakafuni sio mkubwa.
It's okay kwa mama kulia ameshtuka pia na it's very natural mama kuhisi maumivu ya mwanae. Sioni sababu ya mama kulaumiwa....Alienda chooni, ila tu next time amlaze chino kwenye vile vigodoro vya watoto ni salama zaidi.


Sent using Jamii Forums mobile app

Asante Kwa ushauri ubarikiwe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom