Sabayi
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 2,310
- 991
Eucalyptus ni deal kali bro, unaanza kula kuanzia miaka 6 tu na kuendelea. Naiotesha sana sasa hivi.
Nitakutafuta mkuu kwenye hili bado natafuta Shamba huko Njombe kwa ajili ya Miti
Eucalyptus ni deal kali bro, unaanza kula kuanzia miaka 6 tu na kuendelea. Naiotesha sana sasa hivi.
Nitakutafuta mkuu kwenye hili bado natafuta Shamba huko Njombe kwa ajili ya Miti
Kama utakuwa mjini siku ya 09 feb 2013, njoo Lunch Time Hotel ukutane na jf wenzako wanaootesha miti huko unakotafuta wewe shamba.
Sitakuwa mjini ila naweza kuipanga hiyo safari nikaja kwa ajili hiyo najua wanaweza nisaidia kupata mashamba huko ntajitahidi ratiba zikikaa sawa
Nakushauri peleka Mwanza inalipa zaidi kuliko DSM
Nakushauri peleka Mwanza inalipa zaidi kuliko DSM
Habarini za jioni waungwana, samahanini wakuu ninakusudia kuja kufanya biashara ya kununua na kusafirisha mbao toka makambako ama njombe kwenda Dar.
Sina uzoefu na biashara hiyo naomba mwenye clue au aidia ya hii biashara anitupie kabla sijaanza.
Natumaini msaada toka kwenu.
Ahsanteni
Nipo Iringa kama utakuwa tayari naomba tuwasiliane. Nina ekari 20 Kidabaga - Kilolo naona hazitoshi na huku bei kwa ekari moja imepanda sana. Nahitaji shamba huko Njombe.KVM naona hii kazi uliinza muda mrefu kidogo, mimi binafsi naipenda sana hii biashara maana nilishawahi onja utamu wa pesa yake baada ya kuuza miti kidogo niliyopanda nikiwa sekondari. Nimefanikiwa kunua ekari 200 huko njombe najipanga kuanza kupanda january 2013 na 2014 ili mwaka 2022 niwe milionea sio kuanza kulalamikia mafao!
Nipo Iringa kama utakuwa tayari naomba tuwasiliane. Nina ekari 20 Kidabaga - Kilolo naona hazitoshi na huku bei kwa ekari moja imepanda sana. Nahitaji shamba huko Njombe.
Kidabaga vijiji gani mkuu? Uko karibu na hawa New Forest kule Magome au Ng`ang`ange? Maeneo hayo bei iko juu sana sababu ya hawa NF. Jaribu kwenda Ng`ingula au Masisiwe, kule bado ardhi ipo, ila Lupilo bei iko juu sana.
Njombe mambo bado hayajaharibika sana. Wahi wahi.
KVM naona hii kazi uliinza muda mrefu kidogo, mimi binafsi naipenda sana hii biashara maana nilishawahi onja utamu wa pesa yake baada ya kuuza miti kidogo niliyopanda nikiwa sekondari. Nimefanikiwa kunua ekari 200 huko njombe najipanga kuanza kupanda january 2013 na 2014 ili mwaka 2022 niwe milionea sio kuanza kulalamikia mafao!
MIMI NIMEPANDA MITIKI LINDI ndo nimeanza, mbegu zinapatikana wakala wa mbegu za misitu, Morogoro (kihonda) barabara ya kwenda Dodoma.hii mitiki(teak) inachukua muda mrefu sana kuwa na bei nzuri ni ya miaka 15 na kuendelea, ila ukiwa unafanya thining ya shamba unaanza kuuza kuanzia miaka saba, na ina hela mti unaweza fika hadi milioni moja (wanatumia kwa nguzo za umeme, kujenga meli na fenicha za gharama), kuhusu mbegu sifahamu ila european union wanafadhili mradi huko kilombero nasikia tayari wana hekta 3000.
MITIKI INAPANDWA SEHEMU ZENYE JOTO, mikoa ya pwani yote LINDI,MTWARA, PWANI, TANGA, DAR, MORO, na mbegu zinauzwa WAKALA WA MBEGU ZA MISITU MOROGORO
Bei ya mitiki ipoje kwa sasa? kwa mti mmoja wa miaka kama 10