Msaada: Mtaji wa kiasi cha chini kuanzisha biashara ya mbao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Mtaji wa kiasi cha chini kuanzisha biashara ya mbao

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Game Theory, Jan 22, 2011.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi nina chenel ya high quality mbao (zilizokatwa na ambazo bado hazijakatwa) for export toka nchi jirani...documents na leseni zote zipo

  nafikiria masoko ya Far East na Middle East...hivyo UAE, SAUDIA, IRAN na kule Malaysia, Vietnam na kadhalika ndio nakutaka

  Je kuna mtu anaweza kunipa links au ushauri?

  ===================================
  Nasikia Biashara ya mbao au ukataji mbao na inalipa? Au kama mtu yeyote mwenye ufahamu wowote wa hii biashara naomba anisaidie.

  ============================================
  MICHANGO WA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
  =============================================
   
 2. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,934
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  soft wood au hard wood

  ushauri... tafuta market ya semi processed wood
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ukiweza kumtafuta tiger itakuwa vizuri,tiger ni member humu jf na amekuwa akihangaikia hiyo biashara. Na yeye anatoa mzigo toka nchi jirani na kuleta bongo,yy ni mbao ngumu. Jaribu kumtafuta kwa pm na kama hapatikani nitakupa namba zake mobile phone.
   
 4. s

  smilingpanda Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari yako bwana, mimi niko China . Huku kuna soko zuri sana la mbao, zote hardwood au softwood. hii mimi nimekua nikijaribu kuifanya ila nikawa na matatizo ya supply chain nikashidhwa kuingia mikataba nao. kama wewe uko serious, na uko tayari kufanya biashara basi wasiliana nami kwa email aaronsonandcompany@gmail.com. ili tuendelee na mazungumzo.
   
 5. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  mkuu nakuomba tuwasiliana kupitia e-mail hii. miundombinu2010@yahoo.com. kama uko serious soko lipo kubwa tu.
   
 6. E

  Edylux Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Nipatie majina ya mbao ulizo nazo, quality, quantity, contract duration na bei in US$ FOB dar.
   
 7. A

  Ameir JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 248
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Nasikia Biashara ya mbao au ukataji mbao na inalipa? Au kama mtu yeyote mwenye ufahamu wowote wa hii biashara naomba anisaidie.

  ============================================
  MICHANGO WA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
  =============================================
   
 8. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  inalipa aisee kamata hela nenda Ira leta mbao kama una mtaji byee kabs go for it aisee
   
 9. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Nimekutumia ujumbe nafikiri utausoma. All the best.
   
 10. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  Una hela ya kuhonga ili upate vibali vya kuchana mbao?nasikia wizarani mpaka wanahonga ths 30m na bado hawapati vibali
   
 11. A

  Ameir JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 248
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Kuna jamaa namjua anawahonga wale watu wa maliasili. Wanatoa Millioni 1 wanapewa kama mwezi mmoja au miwili. Kuna mtu yoyote mwenye ufahamu wa hii biashara ningefurahi sana mgenifahamisha vizuri
   
 12. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,355
  Likes Received: 6,539
  Trophy Points: 280
  wezi wote wanachofikiria ni kuharibu maliasili tu ili wapate hela za nyama choma na bia, kwani mkilima badala ya kukata miti ndio mtakosa pesa.. acheni upuuzi wa kuharibu mazingira kwa tamaa za vijisenti
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Siyo jambo la kushangaza kwenye serikali legelege
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kama viongozi wetu wanaweka kipao mbele wizi unaofanya uharibifu na hakuna action yoyote inayochukuliwa we unadhani wananchi wafanye je ili nao wapate hela za fasta fasta?
   
 15. A

  Ameir JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 248
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Thankyou kwa kunisaidia kumjibu huyo jamaa maana hajalazimishwa kuchangia mada.
   
 16. K

  KVM JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Mimi nigependa kuwahamasisha wanJF kupanda miti ya mbao hasa mbao nyeupe (pines and cypress). Miti hii inasitawi sana sehemu za nyanda za juu kusini.

  Mimi nilianza kupanda miti hii kama miaka kumi iliyopita. Nimepanda miti mingi kila mwaka bila kukosa. Kwa sasa ninazo ekari nyingi za miti hii. Vile vile miaka ya karibuni nimepanda eucalyptus.

  Wakati naanza kupanda miti mche mmoja nilikuwa nanunua kwa Shs 50 na kuupanda kwa Shs 20. Kwa vile napanda miti mingi (zaidi ya laki moja kwa mwaka) baadaye niliamua kuotesha miche mimi mwenyewe ili kupunguza gharama.

  Gharama zaidi ya miche na upandaji ni barabara za moto kuzunguka msitu. Hata hivyo nilinunua ngómbe na kuwaweka kwenye shamba ili wale majani yanayozunguka msitu. Wamenisaidia sana.

  Unaweza kupanda miti kidogo kidogo kila mwaka kutumia mshahara wako kama nilivyofanya mimi. Baada ya miaka kadhaa utakuwa na miti mingi na utaweza kuwa unauza miti au kupasua mbao kila mwaka.
   
 17. W

  Wenger JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Hiyo biashara Mufindi, Njombe na Makete inalipa sana. Kule Njombe vijijini kwa sasa mti mmoja wa kupasua mbao ukiuza jumla unakwenda kwa bei kati 10,000 mpaka 15,000 kutemegea na size yake na wateja wapo sio wakutafuta wanakufuata wenyewe, sasa ukiwa na miti 100,000 tayari milionea. mwenye nimenunua mashamba huko kwaajili ya kupanda Pines .
   
 18. c

  collezione JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  pia kuna mpango wa kimataifa unakuja. Utakuwa unalipwa hela kutokana na idadi ya miti unayotunza...

  This has been started by international organisations, concerning with environment and global warming.

  Nia kubwa ni Ku_promote upandaji na utunzaji wa mazingira. So ukiwa na shamba la miti, utakuwa unalipwa kila mwezi hela kadhaa.

  Mradi umeanza nchi za ulaya na asia. Kwa africa bado. Sina uhakika kwa nn kwa africa, bado haujaja.
   
 19. K

  KVM JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Kwa mti unaoweza kutoa angalau mbao tatu ndefu za 2" x6" hiyo bei ni ndogo sana ukilinganisha na atakachopata mnunuzi. Ubao mrefu wa 2x6 na uliopakwa dawa DSM una siyo chini ya Shs 17,000. Bei ya mti moja pale Mafinga (Sao Hill) ni zaidi ya Shs. 50 000. Tatizo kule vijijini watu wananunua vimiti vichanga sana.
   
 20. k

  kakaamiye Senior Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ninashukuru sana kwa hii topic, hata mimi nipo interested sana na kupanda miti na ni idea ya muda sasa, issue kwangu ni namna ya kuanza especially kupata shamba kwa ajili ya kupanda. Ningeomba kupata japo idea kama ninaweza kupata eneo huko njombe na kwingineko ukizingatia mimi ninaishi dar. Na price inakuwaje, pia gharama za miche kwa sasa ni kiasi gani na kuotesha plus kutunza. Please please mwenye data ninaomba
   
Loading...