Msaada: Msimu gani ni Muafaka Kutahiri Mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Msimu gani ni Muafaka Kutahiri Mtoto

Discussion in 'JF Doctor' started by Mkare, Jan 17, 2011.

 1. M

  Mkare JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari.
  Nina jambo linanitatiza kidogo la ki-utabibu. Kipindi cha likizo ya mwisho wa mwaka (December 2010), nilipanga kumtahiri mwanangu. Lakini tatizo lilikuja kutoka kwa wazazi na baadhi ya ndugu wa karibu wakati naulizia ni hospitali gani nitapata huduma hiyo. Kila mmoja alikuwa anasisitiza kuwa hakikuwa kipindi kizuri kumtahiri sababu ni kipindi cha joto, hivyo nisubiri mpaka wakati wa baridi. Ikabidi tu niwe mpole ingawa nikifikiria kipindi cha baridi ni huko mwezi April on wards naona kama kijana nae anazidi kukua na utundu unaongezeka. Nikaona kupitia safu hii niulizie uhalisia na uhusiano wa joto na huko kutahiri mtoto cuz I understand nchi zenye joto pia huwa wanatahiri watoto wao. kama kuna mtu mwenye utaalamu wa sekta hii tafadhali anaomba mawazo au ushauri wa kitaalam.
   
 2. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Mi si mtaalamu sana ila kwa uzoefu mdogo nilionao watoto wadogo wa kiume wa ndugu zangu wote huwa wanatahiriwa kipindi cha baridi. Wazee wanasema kuwa kipindi cha joto ni kizuri maana kidonda kinapona haraka du. Wataalam watakuambia zaidi.
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Sisi wengine huwa atuangalii misimu ya hali ya hewa, mtoto akishafikisha siku saba tangia kuzaliwa tu basi anaingizwa sunna (anatahiriwa). Huwa atusubiri mpaka afikie umri wa kwenda shule, kwa sababu umri huo mtoto ashaanza kukomaa na kuwa mtundu...! na huwezekano wa kujitonesha tonesha ni mkubwa sana.

  Kama mtoto wako keshaanza shule basi mpeleke hospitali kutahiriwa kipindi chocote cha likizo, haswa zile likizo ndefu. Kwa ufupi kupona kwa kidonda hakutegemei hali ya hewa, watoto wote miili yao ina uwezo wa kujiponyesha kwa haraka sana kuliko watu wazima.
   
 4. n

  niwaellyester1 Senior Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hata mie nilivyokuwa natoga sikio nilishauriwa kipindi cha baridi ndio kizuri coz yanapona haraka tho naona haimaanishi kipindi cha joto ndio kidonda hakiponi
   
 5. M

  Mkare JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapana bado hajafikia umri wa shule, ana miezi mitano!
   
 6. P

  Paul S.S Verified User

  #6
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu mwaka jana nilikua na shughuli kama hiyo ya kutahiri, lakini kabla niliona nililete mbele ya wadau wanishauri, na baada ya maoni nilipata njia sahihi na nzuri nakushauri tumia hiyo.
  Njia nzuri ambayo haijalisha joto wala baridi ni kumtahiri kwa njia ya plastiki, tena kwa umri huo ndio mahala pake ni siku 5 kwisha maneno.
  Njia hii nikwamba anavalishwa kiplastiki ndani kwa juu ktk kichwa na juu ya ganda panafungwa na kitu kama waya hivi, kisha inaachwa baada ya kuanzia siku 4 hadi 7 utakuta kiplastiki na ganda vimeanguka vyenyewe.
  Na njia hii haina maumivu na kidonda chake ni chadakika kadhaa na mara nyingi haina maambukizi, pia kuanzia siku ya kwanza mtoto anaoga kama kawa na kaptula anavaa tu.
  Sikushauri utumie njia ya kukata na kushona utamtesa sana mwanao kwa maumivu makubwa.
  kwa ushauri zaidi cheki na thread hii
  https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/65133-umri-gani-ni-sahihi-kumtahiri-mtoto-wa-kiume.html
   
Loading...