Msaada msaada msaada nasumbuliwa na ugonjwa wa kisasa!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada msaada msaada nasumbuliwa na ugonjwa wa kisasa!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by amu, Oct 31, 2012.

 1. amu

  amu JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Leo asubuhi mida ya saa 1 na robo nipo kwenye gari natokea nyumbani mtaa wa pili nasikia kipaza sauti kinasema''msaada msaada nasumbuliwa na ugonjwa wa kisasa mwenye 100,200,500 anisaidie atalipwa na mungu'' kumwangalia ni kijana mmoja kwa kumcheki age yake ni ndogo sana haizidi 27 na pengine nilimuona hivyo kwa vile anashida za dunia akazidi kuonekana umri umefika hhapo nilipokadiria.Kavaa kipaza sauti kajirekodi maneno hayo anapita na kusimama mtaani na mfuko wake
  jamani mimi hata sikumuelewa na pia mpaka sasa sikumuelewa na ukifikiria ni kijana mwenye miguu 2,mikono 2 na macho mawili mashaallah hana ulemavu.
  Nimeamua kushare na nyinyi hiki kisa..
  Kazi njema wadau
  nawasilisha
   
 2. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Duh hii dunia bwana imefika pabaya sana,ni ugumu wa maisha,mtu yuko radhi afanye kitu chochote ili apate hela.Kuna siku nilikuwa hospital AAR karibu na Victoria,akatokea kijana mmoja,akaja kwenye bench nililokuwa nimekaa akatoa barua akanipa bila kuongea kitu,kumbe ni bubu,nikaisoma ile barua ilikuwa ya utambilisho toka serikali ya mtaa kwamba yule kijana ni bubu na ni yatima,amefauru kwenda shule maalum ya sekondari lakini uwezo hana kwa hiyo anaomba msaada.
  Huruma iliniingia lakini nilikuwa na wasi wasi na ile barua kama haikuwa sawa kwani hata muhuri wa serikali ya mtaa ulikuwa umechongwa sio kiprofessional.
  Nilimpatia yule kijana elfu 30,000/=,akaondoka.Baada ya muda kidogo akaja mdada akaniambia kuwa kaka umeliwa yule sio bubu hiyo ni njia yake ya kutapeli watu hela.Honestly nilikasirika sana na ujinga nilioingizwa nao na nikakumbuka kwa nini nili-doubt ule muhuri kwenye ile barua.
  Nifikiri ni kuwa waangalifu sana,kuna watu kweli wana matatizo na wengine ni njia ya kupata hela sasa utamjuaje yupi mwenye matatizo na yupi ni muongo ndio issue
   
 3. JICHO LA TATU

  JICHO LA TATU JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mbona wamejaa kibao tu hao....siku hizi akili kumukichwa
   
 4. Ufunguo

  Ufunguo JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Usilie kijana, utalipwa na MUNGU wako. Hata hivyo next time uwe makini, katoe kwenye vituo vya yatima vinavyotambuliwa na serikali. We are all human beings,we need to support each other but with caution.
   
 5. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wapo kibao kitaa ugumu wa maisha nao unachangia!
   
 6. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Huo ndiyo utafutaji wa liziki kwa njia yeyote hile imradi hiwe ya halali.
   
 7. piper

  piper JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Cku hizi ujanja umekuwa mwingi
   
 8. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ugonjwa wa kisasa ndo ugonjwa gani, ombaomba au uvivu?
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280


  haya ndo mambo yaliyotia ganzi moyo mwangu nisisaidie hawa watu, unless ni mlemavu kabisaaaaaaaa.....

  Kuna mwanamama alinifuata pale st joseph tena kwenye grotto akaniambia ana mtoto na mumewe mhonjwa hajala.... Moyo wangu ulisita sana kumsaidia yule mwanamke ila mwisho wa siku nikaamua kumpa 500 (mwaka 2007 sh 500 ilikuwa kubwaaaaa hihiiiiiiii) cha ajabu mpaka leo bado yupo pale, ni mkamilifu wa viungo sijui tatizo nini.....

  Mwaka juzi kuna dreva mmoja alinisimulia kuna mama mmoja anaombaga somewhere mjini, amebeba kama mtoto mgongoni, kuna siku aliamua kumfunua mgongo huyo mwanamama amuone mtoto (sio kila siku wanamsaidia tu) ndipo alibaini kuwa kafunga matambara anajifanya mtoto....

  Hivyo ni vyema kuwa makini na wa kuwasaidia, heri ununue mchele, mafuta na sabuni upeleke kwenye vituo vya watoto yatima, au ukajitolee kusaidia wagonjwa waliokwama mayibabu ocean road au hospitali kuliko usanii huu ulioingia.... Sisemi kua wote wasanii ila kuwa makini......

  Sometimes sh 200 heri umpe kijana anayeosha vioo vya gari kuliko mtu mzima
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  akikuambia na mie unijulishe

   
 11. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Shosti naomba kura yako miss chit chat
   
 12. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kongosho naomba kura yako miss chit chat
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ciello , wenzio watoa vitenge na wewe utatoa nini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wapo wengi saaaana
   
 15. amu

  amu JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  haya mjibu na madam X
  mi hata sikumuelewa na hakunivutia kumuuliza maswali ila nahisi alimaanisha ukimwi maana kiwazi unaitwa ugonjwa wa kisasa au ugonjwa wetu
   
 16. amu

  amu JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  madam x nahisi alimaanisha ukimwi maana kiswazi zamani walikuwa wanauita ugonjwa wa kisasa au ''maradhi yetu''ila hata sikumuuliza maana hakunivutia na ile style aliyotumia ndo kabisaa akazidi kunichanganya
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. amu

  amu JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  japo hujaniomba kura nitakupigia usijali d
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. amu

  amu JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  yaani mi ndo kabisaaa sitoi hela siku hizi
  ilinikuta posta mmama anaomba nauli akaniomba 1000 nikampa nikajua atapanda daladala
  ha ha si nikamuona anaendelea kuomba omba kumuuliza nikashindwa nikamuacha tu
  mjini hapa
   
 19. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  aha ha ha...siku hizi hata mwenye shida ya kweli hasaidiwi maana usanii umezidi
   
 20. amu

  amu JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Kuna mwingine humuhumu jf akasema kapata chuo sasa hana uwezo wa ada na matumizi
  nikamwambia sie ofisi yetu wanwasomesha watu wenye matatizo kama yeye nipm nikuelekeze tena nikampa na njia za kuanzia kabisa
  pia nikmwambia nimekuonea huruma mtoto wa kike ila ile topic yake aliiandika kisanii sasa
  nikampa ushauri edit topic utasaidiwa tu hapa
  katokomea mpaka kesho hajarudi tena
  jamani kazi ipo
  kila siku nasema kuishi mjini tabu
   
Loading...