MSAADA: Mpenzi wangu ananisachi!

luckyperc

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
495
46
Wadau nina mpenzi wangu kipindi chapita 1 yr, ila ananishangaza na tabia yake ya kusachi mifuko yangu ya shati au suruali!
Halafu sielewi anataka nini kwani anatega muda nikienda msalani, Nilishamtega siku hiyo nikamkuta kuuliza anajibu kuwa hata mavazi ni mali yake kuwa ana uhuru huo wa kufanya!
Nitafanyaje ili tabia hii ikome?
 
anasachi kutafuta pesa/bill ya bar/chochote anachodhani kitamsaidia kumkamata mwizi?
 
Mpuuzi na mjinga huyo...Ukirudi kazini mpe afanya hivyo kazi kabla hata hamjasalimiana!

Aombe Mugu asikutane na trouble shooters...Atajikuta mortuary si muda mrefu kwani BP itakuwa inachezea kwenye 140/120 hadi 180/120 kila siku.
 
Mpatie anaxchokihitaji kwa ukamilifu, ataacha kusachi. Anasachi kwa sababu kile anachokitaka hajakipata
 
nafikiri alisha wahi kua mwizi...au anatokea kwenye familia za kifisadi...nakushauri toa taarifa mapema kwenye kituo cha polisi kilicho karibu nawe....
<br />
<br />
Duuh mkuu akatoe taarifa kisa mpenz wake anamsach? Teh teh teh.. Mi nadhani bora amueleze akome hyo tabia kama haipendi.
 
mpe dau la nguvu..... ni ishara kwamba unamkono wa birika wakati yeye ana mkono mrefu
 
Usikubali ukupige sachi bila kuwa na saearching warrant.akifanya hivyo ni kosa kisheria na unaweza kumsuu.sawa mkuu.
 
kwa vile ushamgundua,usiache wallet yako mfukoni,hta bathroom ingia nayo tu,unaibebea kwa soap dish afu soap unaishikilia mkonon
 
Atakuwa na tabia ya udokozi, kuna tabia ukishindwa kuziacha kwenu ndio hivo unaenda nazo kadi kwa watu, hadi kwa mumeo, looo shame on her,
mwambie umeiona hiyo tabia yake na hupendi,ukimwacha ataendelea hivohivo
 
nafikiri alisha wahi kua mwizi...au anatokea kwenye familia za kifisadi...nakushauri toa taarifa mapema kwenye kituo cha polisi kilicho karibu nawe....

Usikubali ukupige sachi bila kuwa na saearching warrant.akifanya hivyo ni kosa kisheria na unaweza kumsuu.sawa mkuu.
Dah nashukuru wakuu!
Sasa je kwenye uhusiano hapa utakuwaje tena?
 
Atakuwa na tabia ya udokozi, kuna tabia ukishindwa kuziacha kwenu ndio hivo unaenda nazo kadi kwa watu, hadi kwa mumeo, looo shame on her,
mwambie umeiona hiyo tabia yake na hupendi,ukimwacha ataendelea hivohivo
Natamani nijue tabia yake kabla sikuzama kwenye penzi zito kwake ningeweza kukaa pembeni, tabu nimejikuta nimezama kwake.
Mbona siku moja nilimwambia akanijibu anahaki ya kufanya hivyo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom