msaada Mlinzi wangu anadai kiinua mgongo. tsh mil 5 nifanyeje?

delusions

JF-Expert Member
Jan 11, 2013
5,003
1,278
Nimekaa naye kwa muda wa miaka 20 akiishi ktk nyumba ndogo iliyopo pembeni anakaa yeye na ndugu zake kwa mshngao leo asbh kaniibukia anadai kwa muda wote huo aliokaa nami anahitaji alipwe kiinua mgongo na tuanze mkataba mpya nilipomuuliza kiasi gani nikapigwa na bumbuazi? Msaada wa kisheria ni halali kweli hili??
 
Kila kitu kina mkataba kama anao mkataba unaomuambia umlipe hiyo pesa mpe...

Ila kiubinadamu kama amekulinda kwa miaka hiyo kiungwana mpe naye ajione mtu.... Pengine uhai wako Mwenyezi Mungu alilinda kupitia huyo jamaa...

Mimi siku hizi mali zangu nazikatia Bima tu nalipa once kwa Mwaka Gari linakaa nje tu mtaani likiibiwa naenda dai bima... Nyumba vile vile... nilipiga hesabu nikaona bima ndio muafaka... kama wezi wa kutoa roho siku ikifika imefika tu roho itatoka hata kukiwa na walinzi tena walinzi wetu ukipita wamelala hadi uwaamishe wewe... lol

Gari kuoshwa kwa siku ni 2,000 kwa mwaka kulindwa kwa usiku tu ni 2,000 kwa mwaka una siku 365 jumla ukilipa ni 730,000/= wakati nikilipa bima ni kama laki tatu hadi nne premium ya mwaka mzima bora nini! na walinzi wetu ukiibiwa hawakulipi... wanakuomba msamaha tu... tena unakuta ni kibabu haswa ukikipiga kibao kimoja hakiamki
 
Gari kuoshwa kwa siku ni 2,000 kwa mwaka kulindwa kwa usiku tu ni 2,000 kwa mwaka una siku 365 jumla ukilipa ni 730,000/= wakati nikilipa bima ni kama laki tatu hadi nne premium ya mwaka mzima bora nini!
Yap hili nalo neno.
Back to Topic
  • Kaa naye huyo mlinzi, mzungumze mtafikia muafaka. Ila miaka 20 ni kipindi kirefu. Mil 5 ni kiasi kidogo waweza msaidia (kiubinaadam zaidi) ili hata kesho na kesho kutwa aweze kukukumbuka.
 
Kila kitu kina mkataba kama anao mkataba unaomuambia umlipe hiyo pesa mpe...

Ila kiubinadamu kama amekulinda kwa miaka hiyo kiungwana mpe naye ajione mtu.... Pengine uhai wako Mwenyezi Mungu alilinda kupitia huyo jamaa...

Mimi siku hizi mali zangu nazikatia Bima tu nalipa once kwa Mwaka Gari linakaa nje tu mtaani likiibiwa naenda dai bima... Nyumba vile vile... nilipiga hesabu nikaona bima ndio muafaka... kama wezi wa kutoa roho siku ikifika imefika tu roho itatoka hata kukiwa na walinzi tena walinzi wetu ukipita wamelala hadi uwaamishe wewe... lol

Gari kuoshwa kwa siku ni 2,000 kwa mwaka kulindwa kwa usiku tu ni 2,000 kwa mwaka una siku 365 jumla ukilipa ni 730,000/= wakati nikilipa bima ni kama laki tatu hadi nne premium ya mwaka mzima bora nini! na walinzi wetu ukiibiwa hawakulipi... wanakuomba msamaha tu... tena unakuta ni kibabu haswa ukikipiga kibao kimoja hakiamki
SDC12876.JPG

1234204_515885698486622_306163655_n.jpg

1234697_515885648486627_851054803_n.jpg
 
Kuna mlinzi na Watchman sasa Mlinzi lazima awe na Silaha na Watchman hatakiwi kuwa na silaha yeyote kwani kazi yake ni Utazamaji tu....
 
Mlipe watu wa nchi nyingi ndio style hiyo, kwa wewe kuja kuuliza humu hadi sheria unaonekana ni mbairi sana labda hata mshahara haumpi haki yake. Mpe muanze upya 20 yrs duh na unataka kwenda mahakamani kweli watu wengine ni roho mbaya tu.

Embu jiulize mshahara unaompatia tangu 1993 hadi leo ni haki ulifanya? Ulimuongezea au kumlipa on time pia?
 
Kiinua mgongo anapewa mtu anaestaafu. Kuna formula ya labour laws nadhani, inasema mishahara ya miezi kadhaa mara muda kadhaa. Sina hakika lakini. Ila ukimlipa make sure unakuwa na ushahidi umemlipa.
 
severence pay..au kiinua mgongo analipwa mtu aliestaafu au alie achishwa kazi kwa sababu ambazo si za kinidhamu yani kustafishwa kwa lazima eg. kupunguzwa kazi.ambayo huwa ni basic pay for seven days times miaka ulivo fanyia kazi isizidi kumi
 
Mbofu naona amemaliza; Kinua mgongo kwa Mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini No.6/2004 ni malipo ya mshahara wa siku 7 kwa mwaka mara idadi ya miaka aliyofanyia kazi lakini isizidi miaka 10 tu, atakama amefanyaka kazi miaka 20 au zaidi inachukuliwa 10tu. na ili mfanyakazi awe na sifa ya kulipwa kinua mgongo ni shariti mkataba wake uwe umesitishwa au mwajiri ameamua kusitisha mkataba na si-vinginevyo.
Ila jamani ''kama unaweka mtu/mfanyakazi akufanyie kazi jaribu kuzingatia haki na kufuata taratibu jinsi zilivyo kisheria hii itapunguza sintofahamu inayojitokeza mwisho wa siku''

.
 
asanteni kwa ushauri Nimemalizana naye nimemlipa tsh 347,000/= baada ya kwenda Chodawu na kunipa formula tena nimempa na mishahara ya hadi januari mwakani kwa kumsaidia. Kwa mazingira haya kisheria sikupaswa kumlipa hata senti moja kwakuwa yeye ndo kavunja mkataba ila kiubinaadam nimetumia formula hiyo kumlipa kama vile mimi ndo nimemuachisha kazi.
 
Kama kweli mmemalizana hongera ila nahisi atarudi tena baada ya muda mfupi kuja kudai tena
 
Mfukuze unipe mimi kazi ya ulinzi........mi nataka ugali na nyama choma tu!
 
Yap hili nalo neno.
Back to Topic
  • Kaa naye huyo mlinzi, mzungumze mtafikia muafaka. Ila miaka 20 ni kipindi kirefu. Mil 5 ni kiasi kidogo waweza msaidia (kiubinaadam zaidi) ili hata kesho na kesho kutwa aweze kukukumbuka.

inategemea mshahra wake ulikuwa ngapi. kiinua mgongo ni mshahara wa siku saba kwa miaka 10
 
Miaka 20 unamlipa laki3 tu? Kweli sometime law is an ass.
We kilaza wa sheria nn hujasikia maprofesori chuo mshahara mil 3 wanastaafu na kiinua mgongo cha mil 4 sembuse huyu mshahara wake ulikuwa sh 45,000/= tena nimefanya uungwana kumlipa maana hakupaswa kupokea hata senti
 
mnyonge mnyongen ila haki yake mpeni mbona hicho kiwango kidogo sana mpe bwana,utazidishiwa hacha kutafuta cjui msaada wa kisheria,ujui unaweza ibiwa ukapata hasara kubwa zaid ya iyo, tena kwa njama ya uyo kwa kuwa anajua nature yako kisa umemtosa
 
Back
Top Bottom