Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Acha roho mbaya na Ushamba wa kipekee pekee.
Kaa na lea huyo janja
Inakugharimu Nini sasa?

Bei gani huyo mtoto anakula?
Huwezi jua Kesho wako atakua Nani na wapi
Kesho huenda huyo akawa vzr kuliko hata mwanao
Kaeni nao wote hata hamna shida.
 
Mkuu hapo naona ngoma draw ya kufanya ni either 2...
-kama una mtoto wa ndugu yako wa jinsia moja na mwanao,,mfungie safari kila weekend uwe unamleta washinde hapo..tena sio mmoja hata wawili, nyumba iwe na watoto wanne ...in long run atakomaa mwanao,,,,

-kama ana umri wa kwenda boarding ,, peleka mwanao boarding
tatu kama unashindwa kufanya maamuz a inaelekea hunaga maamuzi magumu na mkeo anakuamulia vitu basi kuwa mpole deal na mkeo..au mtazame tu
 
Habari wakuu mke wangu ana dada yake ambaye kazalishwa mtoto mmoja na Dada yake hayuko katika ndoa, hajaolewa na aliyemzalisha alikuja akaoa mwanamke mwingine
Huyo ashakua Mwanao (technically). Wanawake wa kichaga pasua kichwa
 
Una element za uchoyo. Kama unaweza kumsaidia msaidie tu unless uwe huna uwezo au mtoto ana tabia ya kishenzi na huko kulia kwake ni watoto ndivyo walivyo.

Au mwisho wa yote mkataze asije kabisa kama humuhitaji kwako kuliko kuishi nae huku unachukia
Hapo labda atoe Talaka kwa mkewe kwa Hali ilivyo huyo kashapelekewa mtoto wa shemeji amlee.
**Wamachame Ni shida aisee
 
Dunian tunatofautiana mm naishu ya hivyo nilimfata mwenyewe na nalipa hadi ada ,msiwe mnaoa mkiwa hamjaamua kuoa kikweli kweli huyo ni mwanao kabisa ukikua utajua,wewe unaweza ruhusu baba mkubwa aliemuoa dada yake na mamayako ateseke? Jibu unalo ,upendo utaompa huyo mtoto utakurudia
 
Asee mal
Habari wakuu mke wangu ana dada yake ambaye kazalishwa mtoto mmoja na Dada yake hayuko katika ndoa, hajaolewa na aliyemzalisha alikuja akaoa mwanamke mwingine

Sasa basi mimi na mke wangu tuna mtoto mdogo wa umri sawa na mtoto wa Dada yake.. mke wangu amekuwa akimchukua mtoto wa Dada yake kila Ijumaa na kumrudisha Jumapili kwa Dada yake

Sasa akiwa anataka kumrudisha mtoto hataki kurudi kwa mama yake anataka kuendelea kuishi nasi wakati huo baba wa mtoto hana muda na mtoto wake kwa mahitaji ya mtoto yaani hamuhudumii.

Mama wa mtoto hataki hata siku moja kumpelekea mtoto kwa baba yake sababu ana mke mwingine atamtesa, Sasa amekuwa akimsukumia kwangu kwa kigezo cha kuja kucheza na mwenzake

Je, ni sawa baba wa mtoto yupo na mama wa mtoto kukataa mtoto kwenda kwa baba kutembea kwa kisingizio Cha mama wa kambo atamtesa hivyo kuona ni sahihi aende kwa mama yake mdogo hali ya kuwa baba yupo na anajichana na maisha?
Asee malalamiko kama haya nilitegemea yatoke kwa mwanamke...... Mi mchoyo Ila umenizidi mbali.... Angekua huyo mtoto ni mtu mzima sawa pengine anaweza akawa na Mambo yake.... Ila ushasema mtoto na pengine unaeza Kuta anakuona kama baba yake kabisa afu we unakuja kumfungulia Uzi huku...... Eti ni sahihi kukaa na mtoto wa dada yako... Kweliiii??? Hili nalo swali???? Kama unashindwa kukaa na mtoto wa shemeji yako hata kinafki akiwa hai, siku akitangulia mbele za haki utamkumbuka hata uyo mtoto??? Mungu atusamehe
 
Kuwa baba kwa watoto wote bila kujali ni wa kwako au la, inaelekea humpendi kabisa huyo mtoto mwingine..acha ubaguzi.
Huwezi lazimisha ampende.
Kumbuka huyo kamuoa mdogo wa dada yange huyo single mother.
Huyo mtoto ana baba yake kabisa wa ukoo wa huko ambao haujulikani.
Hakuna undugu apo.
 
Dunian tunatofautiana mm naishu ya hivyo nilimfata mwenyewe na nalipa hadi ada ,msiwe mnaoa mkiwa hamjaamua kuoa kikweli kweli huyo ni mwanao kabisa ukikua utajua,wewe unaweza ruhusu baba mkubwa aliemuoa dada yake na mamayako ateseke? Jibu unalo ,upendo utaompa huyo mtoto utakurudia
Ujaeleweka mkuu
 
Huwezi lazimisha ampende.
Kumbuka huyo kamuoa mdogo wa dada yange huyo single mother.
Huyo mtoto ana baba yake kabisa wa ukoo wa huko ambao haujulikani.
Hakuna undugu apo.
Ila mwanaume angekuwa na mtoto wa mwanamke mwingine amlete kulelewa hapo mngetarajia mtoto apendwe na mama wa kambo.
 
Back
Top Bottom