Msaada: Mimba ya mke wangu imetunga nje ya kizazi

Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
10,708
12,789
Bila shaka wazima wa afya. Kama wiki moja imepita mke wangu amekuwa anaugulia maumivu ya tumbo, Hali hiyo baada ya kuzidi leo tumeenda hospital na baada ya vipimo imeonekana ana Mimba na imetunga nje ya mfuko wa uzazi.

Mimba Ina Kama wiki tatu na baada ya majibu hayo nimeogopa maana ni Mimba ya kwanza na Sina experience yoyote. Doctor kasema turudi baada ya Kama wiki moja na nusu Kuna dawa atapewa.

Sasa sijajua hiyo dawa itakuwa ni kuirudisha kwenye mfuko wa uzazi au vipi.

Msaada, kwa anayejua Hali hii ikitokea madhara yake yakoje na haiwezi kuleta shida wakati wa kujifungua?
 
Aende hospital kubwa akaonane na gyno wakubwa ectopic pregnancy inaua na Ni hatari Sana kwa afya hasa mrija ukishapasuka, jinsi mnavochelewa ndio inakuwa hatari Sana, maana atapoteza damu na kufa hafu na minor operation juu.
 
Bila shaka wazima wa afya. Kama wiki moja imepita mke wangu amekuwa anaugulia maumivu ya tumbo, Hali hiyo baada ya kuzidi leo tumeenda hospital na baada ya vipimo imeonekana ana Mimba na imetunga nje ya mfuko wa uzazi...

Aiseeeeh! Hiyo ngoma ni balaa, inaua haraka sana yaan haifai! Kimbiza hospital kubwa yenye wataalam wa maswala ya uzazi!
 
Dawa sifahama ka ipo ya kuirudisha kwenye kizazi ila kuna baadhi ya wadau walikuwa wanataka utoaji wa mimba uruhusiwe kutokana na kesi ka hizi za mimba kutunga vibaya. lengo kubwa ilikuwa kunusuru maisha ya mmoja kati ya wawili.

Ushauri unaofaa zaidi nenda katika hosipitali kubwa zaidi utapata ushauri na msaada zaidi wa kimatibabu.
 
Nenda hospital kubwa, afanyiwe upasuaji haraka
Sio lazima upasuaji inategemea na hiyo mimba ipo sehemu gani na ukubwa wake upoje.Anaweza akapewa tu methotrexate akanywa na gestational sac isiendelee kukua na kupotea bila hata kufanyiwa upasuaji.Ila cha muhimu ni aende hosp kubwa akaangaliw kama hali yake inahitaj operation au dawa ya kuzuia kukua.
 
Nishakutana na hii kesi mimba ilitunga nje ya kizazi na baada ya uchunguzi kufanyika ikagundulika Kuna uvimbe mrija was kushoto. Alifanyiwa upasuaji ndogo mimba na mrija vikatolewa. After 6 month alipata tena mimba baada ya kuwa kwenye uangalizi wa Mara kwa Mara. Now the baby is 7 months old.

Hospital ilikua regency.

So nakushauri kafanye uchunguzi zaidi baada ya huo mwezi mmoja.
 
Pia matumizi ya muda mrefu ya vidonge vya uzazi wa mpango uleta matatzo Sana. Ni vyema kama mna mpango na mtoto kustopisha vidonge na kuanza kutumia vidonge vya damu vile kwa miezi mitatu.
 
Bila shaka wazima wa afya. Kama wiki moja imepita mke wangu amekuwa anaugulia maumivu ya tumbo, Hali hiyo baada ya kuzidi leo tumeenda hospital na baada ya vipimo imeonekana ana Mimba na imetunga nje ya mfuko wa uzazi...
Hiyo lazima upasuaji wa kuitoa ufanyike
 
Dawa sifahama ka ipo ya kuirudisha kwenye kizazi ila kuna baadhi ya wadau walikuwa wanataka utoaji wa mimba uruhusiwe kutokana na kesi ka hizi za mimba kutunga vibaya. lengo kubwa ilikuwa kunusuru maisha ya mmoja kati ya wawili.

ushauri unaofaa zaidi nenda katika hosipitali kubwa zaidi utapata ushauri na msaada zaidi wa kimatibabu
Dawa kuitoa tu.
 
Tena uwahi mapema sana.

Mimi kidogp nimpoteze mke wangu mwezi January. Nenda usilembe.
 
Dawa sifahama ka ipo ya kuirudisha kwenye kizazi ila kuna baadhi ya wadau walikuwa wanataka utoaji wa mimba uruhusiwe kutokana na kesi ka hizi za mimba kutunga vibaya. lengo kubwa ilikuwa kunusuru maisha ya mmoja kati ya wawili.

ushauri unaofaa zaidi nenda katika hosipitali kubwa zaidi utapata ushauri na msaada zaidi wa kimatibabu
Unavosoma hii sheria ya kujiongeza ipo ili kuwa kumuoa mama ni kusubili matokeo usiyoyajua unaweza ukawakosa wote hapa
 
Nishakutana na hii kesi mimba ilitunga nje ya kizazi na baada ya uchunguzi kufanyika ikagundulika Kuna uvimbe mrija was kushoto. Alifanyiwa upasuaji ndogo mimba na mrija vikatolewa. After 6 month alipata tena mimba baada ya kuwa kwenye uangalizi wa Mara kwa Mara. Now the baby is 7 months old.

Hospital ilikua regency.

So nakushauri kafanye uchunguzi zaidi baada ya huo mwezi mmoja.
God is great
 
Mtu unaomba msaada, unapewa msaada. Unashindwa kutumia dakika 1 tu kusema ni wapi ulipofikia ili kuepusha au kusaidia na wengine pia wataokuwa na tatizo kama hilo?
 
Bila shaka wazima wa afya. Kama wiki moja imepita mke wangu amekuwa anaugulia maumivu ya tumbo, Hali hiyo baada ya kuzidi leo tumeenda hospital na baada ya vipimo imeonekana ana Mimba na imetunga nje ya mfuko wa uzazi....
Hospital gani hiyo Dr anasema mrudi baada ya wiki? Utampoteza mkeo, mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi ni hatari sana, mpeleke mkeo hospital kubwa akaonwe na gynecologist
 
Feedback tafadhari mimi Imetokea na sasa nipo hospital. Nime declare operation ifanyike.

Nimekuja hapa kutafuta ushauri Lakini nimekutana na mtu ameandika Uzi huu. Japo hakuna further feedback.

Dr. ameshauri kufanya operation, Hii itaokoa maisha ya mama, maana mtoto tayari hapo hawezi kusurvive kuwa nje ya mfuko wa uzazi kwa miezi Tisa atakayokuwa tumboni.

#Asante
DUNIA IMEJAA MAFUNZO KILA KUKICHA.
 
Back
Top Bottom