Msaada: Miche ya mikorosho yenye uwezo wa kukua baada ya miaka mitatu na kuanza kuzaa

Void ab initio

JF-Expert Member
Mar 1, 2015
5,703
5,635
Wakuu,

Naomba mnijuze kuhusu miche ya mikorosho ambayo inauwezo wa kukua baada ya miaka mitatu na kuanza kuzaa. Na mahali inapopatikana.

Naishi Dar es Salaam na Pwani.
 
Nenda Naliendele. Mtwara! Hao ndio wazalishaji hasa hapa Tanzania.Hongera kwa kuingia kwenye kilimo cha korosho.una eka ngapi mkuu?
 
Mjomba Miche ya miaka mitatu ni lugha ya kilimo ili kuvutia watu kupanda miche ya kisasa. Ila ukipanda utaona return kuanzia Mwaka wa tano na kuendelea, nimeona nikuambie ukweli ili ukiingia ujue ni project ya mda mrefu. Mimi nachofanya ni kununua shamba lenye mikorosho then napanda miche mipya pembezoni mwa mikorosho iliyozeeka, hivyo mapato madogo nayopata kwenye mikorosho ya zamani ndio hutumika kugharamia usafishaji wa shamba. Hivyo mipya ikianza kuzaa nakata ya zamani.
 
Wakuu,

Naomba mnijuze kuhusu miche ya mikorosho ambayo inauwezo wa kukua baada ya miaka mitatu na kuanza kuzaa. Na mahali inapopatikana.

Naishi Dar es Salaam na Pwani.

Miche inapatika Kisarawe wilayani, ulizia idara ya kilimo watakusaidia.
 
Wakuu,

Naomba mnijuze kuhusu miche ya mikorosho ambayo inauwezo wa kukua baada ya miaka mitatu na kuanza kuzaa. Na mahali inapopatikana.

Naishi Dar es Salaam na Pwani.

Kama upo Pwani kuna kituo cha serikali kinachoshughulika na uendelezajii wa zao la korosho. Ukikwama hapo nenda mikocheni kwenye kituo cha utafiti wa zao la minazi utapata msaada wako barabara ya cocacola. Ukikosa hapo kuna kitalu cha miti kipo Kibiti huwa wanatoa bure kila mwaka ukiwahi mapema unaweza kubahatika.

Kuhusu muda kitu chochote ni matunzo na uangalizi hata hiyo miembe wanayosema ni miaka 3 inaanza kuzaa isipopata matunzo na uangalizi itapita miaka 5 bado haijazaa muhimu ni kufata kanuni bora uangalizi na matunzo. Ukikosea mwanzo huwezi kupata matokeo mazuri na yaharaka.

Pia sishauri ushauri uliotolewa na mdau mmoja kuwa utafute shamba lenye mikorosho upande mipya jirani yake mbegu mpya inamaana kutakuwa na kunyan'ganyana chakula kama ni hivyo mwenye mizizi mikubwa na mirefu ndio atashiba, ushauri wangu tafuta shamba jipata ukaamua kufata vipimo gani vya kilimo mseto au mikorosho pekee.

Miaka 3 mingi lakini sio mingi njia bora ningekushauri kulima muhogo ndani ya shamba la mikorosho misimu 3 utakayolima muhogo mikorosho itakuwa tayari itakuumiza sana kama miana 3 yote utalima mikorosho pekee.
 
Jamani nauza shamba ekari 13 bei ni mil 26 maongezi yapo tafadhali nina shida naomba msaada shamba lina hati miliki na lipo mkuranga km 10 kutoka barabarani kwa mawasiliano wasiliana na CAPgeminixies consulting LLC Iliyopo Ubungo External 0744 008208 na whatsApp namba inapatikana ]
 
Shamba lina mikorosho zaidi ya 50 mananasi zaidi ya 300 na mazao ya muda mfupi kama vile mihogo migomba na mbogamboga ila pia kuna kibanda cha kujihifadhi [ karibuni sana]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom