Msaada: maumivu ya tumbo la siku na uzazi wa kwanza wa mwanamke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: maumivu ya tumbo la siku na uzazi wa kwanza wa mwanamke

Discussion in 'JF Doctor' started by JS, Jan 27, 2012.

 1. JS

  JS JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wandugu habari zenu binafsi!

  Hebu nisaidieni tafadhali. Nishawahi kusikia mara nyingi tu katika mazungumzo ya hapa na pale kuwa mwanamke akishajifungua mara ya kwanza maumivu ya tumbo la siku huwa yanapungua kwa asilimia kubwa kwa wale ambao huwa wanapatwa na maumivu hayo.

  Naombeni kujuzwa kama ni kweli angalu nitegemee furaha huko mbeleni maana haya maumivu yananitesa kwa kweli si utani.

  Na kama ni kweli uhusiano wa kujifungua na kupungua kwa maumivu umekaaje kitaalamu?

  Na kuna uwezekano kadri miaka ya mwanamke inavyosonga mbele maumivu yatapungua?

  Shukrani sana sana ziwafikie kwa michango yenu yote.

  Love, JS
   
 2. n

  ngwana ongwa doi Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa utafiti mwingi uliofanywa na wataalau unaonyesha maumivu ya tumbo wakati wa siku zake mwanamke hupungua tofauti na yule hajajifungua.
  pia ningependa ujue kuwa wanawake wengine wakiwa wananyonyesha watoto baada ya kujifungua huwa hawapati kabisa siku zao mpaka hata miezi sita kutegemeana na unyonyeshaji,wengine hupata mara i baada ya miezi 3 nk.lakini ni hali ya kawaida.

  Nikweli kabisa maumivu haya hupungua, kumbuka haya husababishwa na prostaglandin hii tunaweza kueleza kwa maneno ya kawaida ni uchungu unaofanya uterus icontract na kutoa mtoto nje, au kutoa uchafu wote uliokuwa ndani ya uterus mara baada ya kukosekana mimba,yaani hapo ndo mama anaona damu inatoka ukeni.

  kumbuka kwamba mwanamke huacha kupata siku zake akiwa na umri kuanzia miaka 45 ila hutegemeana na mtu wengine mpaka 50yrs,hivyo prostaglandin nazo hupungua maana kazi kubwa yake inakuwa imekwisha au imepungua.kama hakuna ovulation prostaglandin nazo hazitakuwepo kwa ajili ya kufanya uterus i contract.Ndo maana teens na twenties inawasumbua sana kuliko wa umri mkubwa.

  swali kwamba kuna uhusiano gani kati yamaumivu kupungua baada ya kujifungua wakati wa siku,ni kwamba mama akijifungua protaglandin nyingine huenda kwa mtoto na mtoto anapozaliwa huwa anazo nyingi sana hupungua kadri anavyoendele kukua,na kiasi kingine hubaki kwa mama.lakini kwa mwanamke ambayo hajajifungua zote zinakuwa mwilini mwake zote.
   
 3. JS

  JS JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Asante sana Ngwana kwa majibu yako fasaha. Maana nilikuwa sielewi uhusiano uko wapi. shukrani.
   
 4. n

  ngwana ongwa doi Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana hapana shaka Mungu anaweza kukusaidia ukawa mmoja wa wenye neema ya kutopata siku zao hata miezi 6 au zaidi kama unanyonyesha vizuri.
   
Loading...