Msaada: Mama yangu kaolewa na kijana umri sawa na sisi wanae

Pole Sana ndugu na maswaibu yaliyokukumba. Uzee huwa una mambo mengi sana kuna watu huwa wanazeeka vibaya na kuna baadhi wanazeeka kama hivyo alivyo mama yako.

Huyu mama hayo ni maisha aliyochagua kuishi na kwa huta weza kufanya chochote as long as huyo ni mama yako mzazi so fuata alichokushauri baba kwa chochote mtakachokifanya hakita msaidia kubadilika sana sana utakuja kuingia kwenye matatizo makubwa sana.

Kutembea na kijana mdogo sio shida kikubwa inatakiwa kumsii mama ajiheshimu asioneshe tabia za ajabu hadharani.
 
Nikirudi nyuma ktk Stori yako mama aliuza mashamba ya familia,na alikuwa na madeni mengi,nadhani hayo ambayo anayafanya sasa hivi huenda ni stress zinazo tokana na msongo wa mawazo.

Anyway yametokea ya kutokea na huna namna ya kuyabadilisha ingawa ni mazito kuyabeba ukiwa kama kijana wa kiume,kubwa ambalo naona ni la muhimu Sana ni wewe ujitahidi usiathirike na hayo yanayotokea mpaka kufikia kushindwa kutimiza ndoto zako,wazazi wameishi Maisha Yao basi na wewe jitahidi uishi Maisha yako,umetoa mfano mzur Baba amekupigia ukamwambia mwache mama kama alivyo nae akakusikiliza basi nawe uwe imara kama Baba yako.

Mwisho mama yako hata awe vipi ni mzazi wako,mpokelee Simu yake na msalimiane usimuwekee kinyongo,kitendo cha wewe kutotaka kuongea nae kitamkera na akinung'unika huenda kwako ikawa mtihani Sana,maana Hilo Linakuwa bifu lako na Mola wako na sio na mama yako.

Broo be strong, kuna a lot of things a head of you,kwahiyo SONGA MBELE na endelea kupambana
 
Jifanye kama huoni wala kusikia,tatizo mawazo yako umeyapeleka kwa kijana jinsi anavyomkunja mama kama wewe unavyofanyaga kwa mademu zako, ndio mana unaumia sana achana na hayo mawazo ,we focus kwenye mambo yako in deep ,usijiingize kwenye kwenye maisha binafsi
 
Kijana bado uko chuo hapo unatengeneza future yako wewe kama wewe we ni kama mm sema mm huwaga sifuatilia mambo ya nyumba ntkupa baadhi ya hints zangu mm the way I don't my anyone's business

Mimi nakaa na wazazi sijui migogoro yao ila wametengana likizo kama ni mwezi naenda wiki moja huku wiki nyingine huku wiki mbili zilizobaki narudi Dar kupiga mishe zangu na kupumzika sitaki kufuatilia nikipata pesa nagawa nusu kote watajua wenyewe baadhi ya matatizo ya wazazi huwezi kuyabeba wale ni binadamu Kama wewe usijipe stress sana kaa mbali si kaolewa kamsalimie kwani unataka kunyonya ushakuwa mkubwa piga mishe zako maana hukai nae tena
 
Muamini mzee wako,kwa kua ameshakuambia kua usiwaze.

Habari yenu wana JF,poleni na mihangaikio ya kuendelea kulijenga taifa.

Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja kikubwa hapa nchini,hivi majuzi nilipokea taarifa kutoka mbeya nyumbani za kuumiza sana moyo wangu,taarifa ilikuwa hii...
Amini maamuzi atakayochukua mzee wako,kwa kua ameshakuambia kua usiwaze,yote muachie yeye,wewe piga shule usichoshe akili

Atakalo amua mzee wako ndio sahihi
 
Haijalishi anafanya nini huyo ni mama yako. Hata kama anajivunjia heshima yake, wewe usimvunjie heshima yake kama mama.

Usijipe jukumu la kumrekebisha ama kumkanya maana utamvunjia heshima tu.
Kama kuna wakubwa kama wajomba na mababu/bibi basi ongeeni nao wamuweke chini ndugu yao.

Maongezi yote yakishindikana, basi ni bora kujitenga nae kabisa kuliko kujaribu kumrekebisha wewe kama mtoto.

Kuhusu ndoa yake na kijana mdogo, hiyo ipo nje ya mamlaka yenu. Yeye ni mtu mzima na huyo kijana mdogo pia ni mtu mzima kisheria. Jaribio lolote la kutaka kuingilia hayo mahusiano yatapelekea kusikia/kuona mambo yatakayokukera na kukufedhehesha zaidi. Kwa kifupi ukimya wako katika hili ndio busara yako.
 
Habari yenu wana JF,poleni na mihangaikio ya kuendelea kulijenga taifa.

Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja kikubwa hapa nchini,hivi majuzi nilipokea taarifa kutoka mbeya nyumbani za kuumiza sana moyo wangu,taarifa ilikuwa hii...

Kwanza pole sana. Nadhani hili ni sehemu kubwa ya changamoto kwako kama kijana. Ingeeleweka kama mzee angekuwa amefariki ila kwa hali uliyoelezea, hata kama mzee atakuwa ni mkosaji kwenye ndoa yake, bado mama yako ataonekana napinda zaidi.

Pili, nakushauri ukae mbali na mahusiano ya wazazi wako. Ninamaanisha, usimruhusu mzee au mama akakupa upande wake wa story kwa namna yoyote ile. Wote ni wazazi wako, cha kufanya ni kutafiti na kuamua kulingana na taarifa na ushahidi wako binafsi.

Hii itakuondoa kwenye mgogoro na wazazi.

Mwisho kabisa, kwa mujibu wa maelezo yako, historia inaonyesha mama kaamua mwenyewe kuvunja nyumba yake, sasa hapo utajitafakari na kuamua, aidha ujitenge naye mazima au ujaribu kuongea naye atambue mnavyojisikia watoto wake. Akishindwa basi utakuwa umetekeleza wajibu wako.
 
Mambo ya wazazi waachie wenyewe maana hujui kwanini wamefikia hapo, kikubwa ni kuzingatia kuwaheshimu na kufanya yako

Mama kufikia hivyo ni matokeo ya migogoro baina yao na kamwe kuna mambo mengine huwezi kuwekwa wazi maana ukiyajua yanaweza kuwa aibu zaidi kwako,

Kwenda migodini na kuamua kuishi hivyo inaonekana Mama amekosa wa kumsikiliza na kumsaporti japo kwa makosa ambayo ameyafanya hivyo anajihisi mpweke mwenye kukataliwa kila sehemu ndio maana ametafuta mtu wa kumfariji(huyo kijana) pia wewe kukataa kuongea na mama yako ndio unaongeza tatizo ebu jaribu kuwasiliana nae na muonyeshe bado kuna watu wanampenda na wanaweza kumsikiliza japo kidogo

Pia usipende kujaji kwa kusikiliza upande mmoja Mama anaweza kuwa na makosa lakini namna ya kumuhukumu ndio ikampoteza kabisa.
 
Ni vigumu sana kumbadilisha, kama unaweza mpotezee vingenevyo atakupotezea muda tu.
 
Back
Top Bottom