MSAADA: Mama kabadilika baada ya kuwa Mlokole

sokwe

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
2,022
1,059
Wapendwa wanajf naombeni ushauri, mama yangu ameingia kwenye makanisa ya kilokole japokuwa familia nzima ni wakatoliki, tangu ameingia kwenye makanisa hayo maisha yake yamebadilika sana, hana ukaribu na mumewe yaani baba yetu! Kwa mfano walikuwa wanasali pamoja asubuhi na jioni pamoja sasa haiwezekani tena kwani Ana amini baba yangu ni mchafu! ashirikiani na ndugu zake yaani wajomba na shangazi zetu japokuwa wamefanya jitihada kubwa kujaribu kutafuta muda kuzungumza nae imeshindikana! Kwani anatoka nyumbani saa 11 alfajiri na kurudi usiku.

Baba yetu amekuwa kwenye kipindi kigumu sana kiasi cha kuniomba kuzungumza nae kwani Mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia yetu nimeshindwa kuzungumza nae kwa sasa kwani naishi Japan na familia yote ipo tanzania, natarajia kurudi nyumba kwa likizo fupi mwezi wa 12, kuna kipindi Mdogo wangu alikuwa anasumbuliwa na tumbo akampeleka kwenye maombi akaonekana Ana mapepo yaliyokuwa anadai baba yetu ndie anamloga bwana Mdogo!

Nilipopata taarifa hizo nilishtuka sana nikamuomba Mdogo wangu aende hospital kwa uchunguzi bahati nzuri Nina rafiki yangu tulisoma pamoja ni dr wa matumbo pale muhimbili, baada ya kufanyiwa uchunguzi alionekana na bacteria h. Pylori ambao walisababisha apate ulcers pia, baada ya matibabu amepona kabisa! Baba yangu ni mfanya biashara mkubwa sana na msomi Sio Kwamba najisifia ila ndio ukweli, alifanya kazi kwenye jumuia ya Africa mashariki miaka ya 80, akaamua kuacha kwa hiyari yake na kijiingiza kwenye biashara tangu miaka hiyo, anafanya biashara ulaya na Middle East na marekani, baba yangu anaweza kuwa mchawi?

Japokuwa habari hizi hazijamfikia Kama zikimfikia anaweza akapata heart attack Kama Sio stroke, kuna mama aliyemuintroduce mama yangu kwenye makanisa haya ya kilokole alikwisha fariki na cancer ya ziwa kwani alikataa matibabu ya hospital! Napata Shaka ikitokea mama kuumwa huenda akakataa Kwenda hospital pia au kuficha maradhi yake, poleni kwa post yangu ndefu, naombeni michango yenu.
 
Lol pole sana huyo mama anahitajia ushaui nasaha aisee. Kuna makanisa kadhaa huwa yanahubiri upotofu kabisa na hii inatokea kwenye familia nyingi zinazoamua kujiingiza kwenye imani hizo. Maana alitakiwa awe na mabadiliko mazuri hasa baada ya kuokoka sasa kama inakua mbaya basi hiyo haitokani na Mungu. Wengi wanautata sana maana wanakua brainwashed na hao wachungaji mara mikesha, mara semina na hasa wakiona huyo ni mambo safi hapo kazi ipo kumng'oa ndugu yangu. Cha msingi Muombe Mungu akupe nafasi na hekima ya kuongea nae na jaribu kufuatilia je anaenda kwenye kanisa gani na mchungaji wake ana historia gani. Fuatiia waumini wanaosali kwenye kanisa hilo wakoje. Maana kuna baadhi ya makanisa waumini wao wamekua kama wamelishwa dawa hivi.
 
Mdogo wangu Ablessed put it well.
Alitakiwa achange to the better na sio to the worse. Siamini uwepo wa Mungu kwenye hilo dhehebu lake jipya ambalo badala ya kuimarisha familia linaleta mtafaruku.
Nini cha kufanya, kwakweli sijui sana maana hao watu wanakuwa kama fanatic fulani. Kama mnaweza, book appointment SCOAN pale si tu mtapata derivelence lkn pia counciling yenye lengo ya kuwapatanisha. Nafikiri njia hiyo mama yako anaweza ielewa. Be smart when presenting that issue; mama mwambie tunsmpeleka baba ili kama kuna mavitu ya ukoo au biashara yakavunjwe na familia yote iwe derivered, baba, mwambie mnampeleka mama kwa councilling kwa kuwa anaoweza kuwasikiliza ni walokole wenzake na wewe unaamini the only smart mlokole anayeweza kutazama swala lao kwa rationally ni T.B.Joshua na ministry yake ya reconciliation.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu, haya makanisa mengi yaliyoanza kama uyoga hayana msingi wa imara kusimamia kile wanachokiamini, mara nyingi hukimbilia kwenye hoja nyepesi nyepesi kupata wafuasi. Kwa mtazamo wangu ni kuwa wamechanganya mambo, wamechukua mambo fulani ya imani za kikristu na imani za kiasilii, sasa matokeo yake ni kuwa wamekuwa kama waganga wa kienyeji ambao wanaamini kuwa kila kitu kinasababishwa na roho fulani, ukiangalia kwa undani unaona ni kama wanajaribu kusingizia ukristu kuhalalisha ushirikina.
Sasa tukirudi kwa hilo la familia yako, Pole sana kwa hilo. Ila na dhani ufanye yafuatayo
1. Inabidi uongee na mama yako mzazi, moja kwa moja usihofu, ni ngumu hasa ukizingatia kuwa wameshamteka kiakili, lakini jikaze pindi utakapo rudi uongee nae.
2. Kama kuna viongozi wa kiimani wa kikatoliki ambao ni waelewa jaribuni kuwasiliana nao, na pili kama wanaweza kuongea nae moja kwa moja ili kuweza kumjengea hoja imara.
3. Sitaki kuwasema vibaya ila inaonekana kunatatizo kati ya wazazi toka awali, sasa baada ya mama kukimbilia huko akaanza kujenga hoja ya kutetea kile alichoona kinatokea nyumbani wakati ule, hivyo basi ni vizuri ukaongea na baba ujue tatizo lilianzia wapi. Kina mama ni wadhaifu sana katika hisia hivyo basi wakitendewa kwa muda hukaa na vinyongo baadae vinapochanua hukimbilia kanisani.
Pole sana bro
 
Nina wasiwasi hutapata ushauri muafaka, na hata kama utaupata basi hautakuwa msaada kwako au mama yako.
Wengi watakuja hapa na kukashifu imani ya mama yako na kumuona kama mtu asiyefaa na kapotoka.
Hayo nimeyaandika kwa kutumia uzoefu tu wa kuwepo jamvini hapa muda mrefu na kuoanisha shauri zitolewazo na watu linapokuja suala la imani kali za Kikristo au Kiislamu.
 
Mdogo wangu Ablessed put it well.
Alitakiwa achange to the better na sio to the worse. Siamini uwepo wa Mungu kwenye hilo dhehebu lake jipya ambalo badala ya kuimarisha familia linaleta mtafaruku.
Nini cha kufanya, kwakweli sijui sana maana hao watu wanakuwa kama fanatic fulani. Kama mnaweza, book appointment SCOAN pale si tu mtapata derivelence lkn pia counciling yenye lengo ya kuwapatanisha. Nafikiri njia hiyo mama yako anaweza ielewa. Be smart when presenting that issue; mama mwambie tunsmpeleka baba ili kama kuna mavitu ya ukoo au biashara yakavunjwe na familia yote iwe derivered, baba, mwambie mnampeleka mama kwa councilling kwa kuwa anaoweza kuwasikiliza ni walokole wenzake na wewe unaamini the only smart mlokole anayeweza kutazama swala lao kwa rationally ni T.B.Joshua na ministry yake ya reconciliation.
Unajua Kaunga uliyosema ni kweli sister lkn kuna baadhi ya imani haziko sawa na nadhani waamini wengine walishazistukia japo si rahisi kuzijua. Ni vizuri akaihandle hii issue vizuri. Nimeona jamaa zangu kadhaa wakitekwa na hii mitego ya imani na hasa wanapoonekana wana matatizo. Roho yoyote inayopingana na mafundisho ya kristo haitokani na Mungu . Maana hata Bwana alikua mnyenyekevu , sasa hii inayoleta mtafaruku ktk familia inatia shaka kidogo. Kama ni wakatoliki basi wajaribu pia kwenda pale ubungo EMAUS kuna catholic charismatic renewal ambapo every Saturday na sunday huwa wanakuwepo . Hata hivyo pole Mungu akusaidie tu kuliokoa hilo jahazi bro.
 
Last edited by a moderator:
Nina wasiwasi hutapata ushauri muafaka, na hata kama utaupata basi hautakuwa msaada kwako au mama yako.
Wengi watakuja hapa na kukashifu imani ya mama yako na kumuona kama mtu asiyefaa na kapotoka.
Hayo nimeyaandika kwa kutumia uzoefu tu wa kuwepo jamvini hapa muda mrefu na kuoanisha shauri zitolewazo na watu linapokuja suala la imani kali za Kikristo au Kiislamu.
Naamini nyakati zote kua mtu akileta hoja yake hapa jamvini lazima kuna watakaokua na mawazo hasi lkn asife moyo kuna wachache watakaomshauri vema na ni vizuri post inayokashifu asiijibu yeye aipotezee tu, cha msingi achukue kitakachomfaa basi. Naona kuna waliopost hapo juu, na Kaunga hapo kasha mpa muongozo kiasi sasa asubiri na wengine watamueleza nini.
 
Last edited by a moderator:
Pole. Yalinikuta kwa mke wangu alivyohamia kwa makanisa hayo na kutaka kuwahamishia huko watoto. Mimi nimetumia udikteta kidogo na tunakaribia mwaka wa kumi. NiPM tuongee. Pole.
 
Pole. Yalinikuta kwa mke wangu alivyohamia kwa makanisa hayo na kutaka kuwahamishia huko watoto. Mimi nimetumia udikteta kidogo na tunakaribia mwaka wa kumi. NiPM tuongee. Pole.
don't dare na husijaribu kumshauri atumie udikteta kwa Mama yake mzazi, mama mzazi ana tofauti kubwa sana na mke....kama hujaelewa tafuta kueleweshwa:yell:
 
...kuna baadhi ya imani haziko sawa na nadhani waamini wengine walishazistukia japo si rahisi kuzijua.

Hebu tueleze huwa unatumia kigezo gani au kipimo gani kujua kuwa imani fulani haipo sawa na nyingine ipo sawa....

NB:
IMANI ni hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
 
Wapendwa wanajf naombeni ushauri, mama yangu ameingia kwenye makanisa ya kilokole japokuwa familia nzima ni wakatoliki, tangu ameingia kwenye makanisa hayo maisha yake yamebadilika sana, hana ukaribu na mumewe yaani baba yetu! Kwa mfano walikuwa wanasali pamoja asubuhi na jioni pamoja sasa haiwezekani tena kwani Ana amini baba yangu ni mchafu! ashirikiani na ndugu zake yaani wajomba na shangazi zetu japokuwa wamefanya jitihada kubwa kujaribu kutafuta muda kuzungumza nae imeshindikana! Kwani anatoka nyumbani saa 11 alfajiri na kurudi usiku.

Baba yetu amekuwa kwenye kipindi kigumu sana kiasi cha kuniomba kuzungumza nae kwani Mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia yetu nimeshindwa kuzungumza nae kwa sasa kwani naishi Japan na familia yote ipo tanzania, natarajia kurudi nyumba kwa likizo fupi mwezi wa 12, kuna kipindi Mdogo wangu alikuwa anasumbuliwa na tumbo akampeleka kwenye maombi akaonekana Ana mapepo yaliyokuwa anadai baba yetu ndie anamloga bwana Mdogo!

Nilipopata taarifa hizo nilishtuka sana nikamuomba Mdogo wangu aende hospital kwa uchunguzi bahati nzuri Nina rafiki yangu tulisoma pamoja ni dr wa matumbo pale muhimbili, baada ya kufanyiwa uchunguzi alionekana na bacteria h. Pylori ambao walisababisha apate ulcers pia, baada ya matibabu amepona kabisa! Baba yangu ni mfanya biashara mkubwa sana na msomi Sio Kwamba najisifia ila ndio ukweli, alifanya kazi kwenye jumuia ya Africa mashariki miaka ya 80, akaamua kuacha kwa hiyari yake na kijiingiza kwenye biashara tangu miaka hiyo, anafanya biashara ulaya na Middle East na marekani, baba yangu anaweza kuwa mchawi?

Japokuwa habari hizi hazijamfikia Kama zikimfikia anaweza akapata heart attack Kama Sio stroke, kuna mama aliyemuintroduce mama yangu kwenye makanisa haya ya kilokole alikwisha fariki na cancer ya ziwa kwani alikataa matibabu ya hospital! Napata Shaka ikitokea mama kuumwa huenda akakataa Kwenda hospital pia au kuficha maradhi yake, poleni kwa post yangu ndefu, naombeni michango yenu.

Uzoefu kidogo nilio nao ni kwamba mtu anapoingia kwenye 'hizi imani', juhudi zozote mtakazokuwa mnafanya 'kumkomboa' zitapelekea yeye kujichimbia zaidi huko ili 'kukemea roho zenu mbaya'...
Kwa kiasi fulani method ambayo inafanya kazi, ni kuonyesha kumsapoti (sio kwa maneno), bali kwa kuwa karibu nae, kumpenda zaidi, kutumia mda wowote utakaopatikana kustorisha nae, akileta stori za kushawishi uingie ulokoleni, usipinge, msikilize, then kaa kimya, au mwambie aendelee kukuombea ili siku ukifunuliwa uingie humo (kimoyo moyo unajua kuwa hutaingia), nk...
Lengo la kufanya hivi ni kumjengea hali kuwa nyumbani kuna 'kampani', na ni mahali pa furaha kwake. mda si mrefu (atakapopata frustration huko), atapakumbuka nyumbani na 'kurudi kundini.
But mkimtreat kama 'aliyepotea', mjue kwamba atazidi kupotea.
By the way, kwa hali ya kiuchumi nyumbani kwenu, it is likely mama ameenda huko out of frustration za aina fulani. Nyumbaza matajiri mara nyingi watu wako 'bize' na hazina furaha...
 
Haya mambo yasikie tu kwa watu. Yanaweza kuwavuruga hadi mkasambaratika. Muhimu ni msikubali kutenganishwa hata kidogo. Mtatajwa wachawi mmoja baada ya mwingine hapo. Endeleeni kuongea na mama kwa upendo na mumsaidie majukumu. Muambie dingi, sasa ndo wamefikia stage ya kuchukuliana mizigo kwa upendo. Aendelee kusali na kumuombea mkewe pia kuwa Mungu azidi kumuonyesha upendo wake.

Acheni jamani! Kuna mtu anaenda kulala church 3 days anaacha familia ati!
 
Biblia inasema mtawatambua kwa matendo yao. Tena inasema asiyetunza wa kwao hafai, ni bora asieamini.

Kama mama ama baba atakuwa na imani itakayompelekea akose hata muda wa kuonyesha upendo kwa familia, hiyo ni imani gani? Na atawaambukizaje imani watu wa nyumbani kwake kama hataki kusali nao wala kuongea nao? Kama imani inakufanya ushindwe kazi ama familia, hiyo sio imani tena.
Hebu tueleze huwa unatumia kigezo gani au kipimo gani kujua kuwa imani fulani haipo sawa na nyingine ipo sawa....

NB:
IMANI ni hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
 
Kuna jamaa alimfukuza mkewe kwa kesi kama hiyo...Mke aliambiwa afanye maombi ya mvua yani siku tatu mfululizo bila kupumzika usiku ni mchana.....Basi jamaa kwa kuwa alikuwa ni mtu wa kusafiri masafa marefu, siku anarudi kutoka safari amechoka atleast apumzike ale chakula cha nyumbani na mkewe;,,, ile kuingia tu ndani kakuta mke ana roroma kwa maombi wala ajigusi...

Basi pale pale jamaa alimpiga kipigo kitakatifu na takalaka juu....Mke yupo mtaani kama amechanganyikiwa anazunguka tuu...

Kwa kweli wanawake ndo wanaidanganyika na haya makanisa kwani asilimia 80% ya waumini wao ni wanawake...
 
Wanawake wanadanganyika kwa sababu ya frustration za mahusiano. Akiambiwa njoo huku kuna tumaini, anakimbia mbio! Ndo maana hata kutumiwa kingono ni rahisi.
Kwa kweli wanawake ndo wanaidanganyika na haya makanisa kwani asilimia 80% ya waumini wao ni wanawake...
 
Nina wasiwasi hutapata ushauri muafaka, na hata kama utaupata basi hautakuwa msaada kwako au mama yako.
Wengi watakuja hapa na kukashifu imani ya mama yako na kumuona kama mtu asiyefaa na kapotoka.
Hayo nimeyaandika kwa kutumia uzoefu tu wa kuwepo jamvini hapa muda mrefu na kuoanisha shauri zitolewazo na watu linapokuja suala la imani kali za Kikristo au Kiislamu.

mbona amepewa ushauri mzuri tu hapo juu? stop being negative.
 
Mdogo wangu Ablessed put it well.
Alitakiwa achange to the better na sio to the worse. Siamini uwepo wa Mungu kwenye hilo dhehebu lake jipya ambalo badala ya kuimarisha familia linaleta mtafaruku.
Nini cha kufanya, kwakweli sijui sana maana hao watu wanakuwa kama fanatic fulani. Kama mnaweza, book appointment SCOAN pale si tu mtapata derivelence lkn pia counciling yenye lengo ya kuwapatanisha. Nafikiri njia hiyo mama yako anaweza ielewa. Be smart when presenting that issue; mama mwambie tunsmpeleka baba ili kama kuna mavitu ya ukoo au biashara yakavunjwe na familia yote iwe derivered, baba, mwambie mnampeleka mama kwa councilling kwa kuwa anaoweza kuwasikiliza ni walokole wenzake na wewe unaamini the only smart mlokole anayeweza kutazama swala lao kwa rationally ni T.B.Joshua na ministry yake ya reconciliation.

Hivi hiyo appointment SCOAN nyinyi mnaipataje kirahisi...

Maana mama yangu ameomba hiyo chance ya ku visit muda mrefu lakini mpaka leo haieleweki,, kwanza alienda kwa agent wao pale karibu na Mariedo akakuta hapaeleweki utaratibu unakwendaje maana watu kibao wanalalamika,,, then tulijaza fomu kwenye website ya SCOAN na baada ya kumaliza tukapewa namba za simu za kupiga ku confirm kama inakuaje.. Hizo namba hatujawai kuzipata kila ukipiga ni busy au not rechable

Kuna njia yoyote ya kumsaidia Mama apate visiting appointment there maana amekwama kabisa japokuwa ameshajiandaa kwenda hata kesho akipata chance..
 
Last edited by a moderator:
Kisaikolojia ni kwamba kadri mtu anavyoendelea kuzeeka ndivyo anavyoendelea kumtafuta mungu zaidi, ni muda ambao huhitaji kufarijiwa zaidi na walio karibu nae na kama ikitokea hakuna, hutafuta mahali ambapo anapofikiri pana matumaini. Kina mama wengi hasa wazee hukimbilia makanisani kama tumaini pekee kwao kwani wakati huo huwa katika stage ya integrity vs despair; huanza kujiuliza ni nini alichofanya katika ujana wake(kiroho) kitakachomfanya baadaye auone ufalme wa mungu? Kama alisali na kukua kiroho vizuri katika maisha yake ya ujana basi hutulia pale alipo na kuendelea kusali bila shida ila kama katika ujana wake aliendekeza anasa na starehe bila kuwa na mahusiano mazuri na mungu basi uzeeni huangaika kutafuta huruma ya mungu na hapa ndipo huenda kanisa moja baada ya lingine akitafuta ukamilifu.

Ushauri; muwe karibu na mama kwani kinachofanya afanye hivyo ni kutafuta acceptance mbele za mungu, mpendeni san ana kuonyesha ushirikiano mkubwa kwake bila kuonyesha kama kakosea. Kwa kufanya hivyo hakika mama atazeeka vizuri bila ya stress!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom