sokwe
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 2,022
- 1,059
Wapendwa wanajf naombeni ushauri, mama yangu ameingia kwenye makanisa ya kilokole japokuwa familia nzima ni wakatoliki, tangu ameingia kwenye makanisa hayo maisha yake yamebadilika sana, hana ukaribu na mumewe yaani baba yetu! Kwa mfano walikuwa wanasali pamoja asubuhi na jioni pamoja sasa haiwezekani tena kwani Ana amini baba yangu ni mchafu! ashirikiani na ndugu zake yaani wajomba na shangazi zetu japokuwa wamefanya jitihada kubwa kujaribu kutafuta muda kuzungumza nae imeshindikana! Kwani anatoka nyumbani saa 11 alfajiri na kurudi usiku.
Baba yetu amekuwa kwenye kipindi kigumu sana kiasi cha kuniomba kuzungumza nae kwani Mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia yetu nimeshindwa kuzungumza nae kwa sasa kwani naishi Japan na familia yote ipo tanzania, natarajia kurudi nyumba kwa likizo fupi mwezi wa 12, kuna kipindi Mdogo wangu alikuwa anasumbuliwa na tumbo akampeleka kwenye maombi akaonekana Ana mapepo yaliyokuwa anadai baba yetu ndie anamloga bwana Mdogo!
Nilipopata taarifa hizo nilishtuka sana nikamuomba Mdogo wangu aende hospital kwa uchunguzi bahati nzuri Nina rafiki yangu tulisoma pamoja ni dr wa matumbo pale muhimbili, baada ya kufanyiwa uchunguzi alionekana na bacteria h. Pylori ambao walisababisha apate ulcers pia, baada ya matibabu amepona kabisa! Baba yangu ni mfanya biashara mkubwa sana na msomi Sio Kwamba najisifia ila ndio ukweli, alifanya kazi kwenye jumuia ya Africa mashariki miaka ya 80, akaamua kuacha kwa hiyari yake na kijiingiza kwenye biashara tangu miaka hiyo, anafanya biashara ulaya na Middle East na marekani, baba yangu anaweza kuwa mchawi?
Japokuwa habari hizi hazijamfikia Kama zikimfikia anaweza akapata heart attack Kama Sio stroke, kuna mama aliyemuintroduce mama yangu kwenye makanisa haya ya kilokole alikwisha fariki na cancer ya ziwa kwani alikataa matibabu ya hospital! Napata Shaka ikitokea mama kuumwa huenda akakataa Kwenda hospital pia au kuficha maradhi yake, poleni kwa post yangu ndefu, naombeni michango yenu.