Msaada: Maji yameingia sikioni nikiwa naoga, nafanyaje kuyatoa?

evart

JF-Expert Member
Sep 4, 2016
2,838
2,771
Habari wana JF?

Kama kichwa cha mada kinavyojieleza maji yameniingia sikioni wakati naoga siku ya jana, nifanyeje kuondoa hali hii.

Nawasilisha!
 
Ingiza maji kidogo kwenye hilo sikio halafu laza kichwa sekunde 5 ubavu mwengine halafu laza tena ubavu wa pili hapo yatatoka.
 
Huwa narukaruka kidogo kwenye sakafu nikiwa bila viatu na kutua kwa visigino..maji hutoka.
 
Weka maji mengine kwenye hilo sikio mpaka uyasikie yameingia ndani, baada ya hapo inamisha kichwa upande wa hilo sikio huku ukiruka ruka kama unaruka kamba yatatoka!
Hivi huu ushauri ni kweli au? Yaani aongeze maji mengine,naomba ufafanuzi tafadhali.
 
Dondoshea Tena matone mawili au Matatu ya maji Yakishaingia inamisha sikio ili maji yatoke.

Harafu Njoo Unipe Mrejesho..
Huu ushauri uko vizuri hata mimi nilishawahi kujaribu kudondoshea matone mengine ya maji ili kuyatoa maji yalioingia sikioni.
 
Njia niliowahi tumia ikafaa ni kuruka ruka huku umeinamisha kichwa upande ambao ndio wa sikio lenye maji.

Simama kama Zombie.
 
Na uchafu pia utakuwamo kama itasumbua sana nenda clinic usafishwe

Maana maji hayachukui muda mrefu
 
Back
Top Bottom