Msaada: Maana na matumizi ya TAARIFA na HABARI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Maana na matumizi ya TAARIFA na HABARI

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by MAMMAMIA, Dec 17, 2010.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikisikia redio na televisheni zetu zikitumia neno "Taarifa ya Habari". Huwa nina wasiwasi na matumizi ya maneno haya mawili kwa pamoja. Ninaomba wataalamu wa kiswahili wanisidie kujuwa:
  1. Nini maana ya neno TAARIFA?
  2. Nini maana ya neno HABARI?
  3. Kwa nini lisitumike neno moja tu kati ya haya mawili, hasa hili la pili?
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Dec 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Haya yote yana asili ya Kiarabu, Habari (khabar), Taarifa (taareef ). Na tafasiri yake ni:

  Habari (Khabar) news/information/report/rumor/notice

  Taarifa (Taareef) explanation/description/praise/definition

  Kwa maelezo haya mafupi ni matumaini utakuwa umepata mwanga kidogo.
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Asante sana X-Paster kwa maelezo yako mazuri. Lakini bado napata mashaka kwa matumizi sambamba ya maneno haya. Tuseme Taarifa ya Habari ni sawa na kusema kwa mfano ni sawa na "News Explanations", "News description"...?
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Dec 20, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nadhani hapo ina maana ya kuelezewa (una taarifiwa) hizo Habari zilizokuwepo siku hiyo ndio maana ya Taarifa ya habari.
   
 5. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Safi sana X-Paster.

  Kwa kuongezea (kwa maana lugha tuliyokopa maneno kwake ni pana) Taaref ni Kujuzwa na Khabar ni kama ilivyo habari!

  Hivyo basi neno hilo litaleta maana KUJUZWA HABARI na kwa maana hiyo wako sawa!
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Dec 20, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,343
  Trophy Points: 280
  Niongezee senti sumuni.
  Habari ni maelezo[information] zinazosikika, zinaweza kumhusu mtu moja kwa moja au kwa kupitia. Mathalani unaweza kusikia habari ya ndege kuanguka na ukakumbuka kuwa ndugu yako alikuwa msafiri ndani ya ndege hiyo. Hapa imekugusa [indirectly] na [directly]. Utakapokwenda nyumbani kuwaambia kuwa ndugu yenu alikuwa ndani ya ndege iliyoanguka hiyo si habari tena ni taarifa.
  Kwa maneno mengine huwezi kuletewa habari za msiba wa anayekuhusu moja kwa moja, ila utaletewa taarifa Baba/Mama/Dada/ n.k amefariki. Lakini utakaposikia mchezaji fulani amefariki hiyo ni habari, kama anakuhusu basi hutatoa habari bali taarifa.
   
 7. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2015
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Marahaba umeweka vitu vizuri Nguruvi3
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...