Msaada: Laptop yangu imezima kioo lakini sauti inatoka

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,039
3,668
Habari wanaJF,

Nina Laptop yangu aina ya Dell nilikua sijaitumia effective kama miaka 2 hivi, nilikua tu naitoa mara chache chache tu nacheki movie na kuirudisha kwenye begi.

Sasa majuzi kuna mambo yanatakiwa niyafanye na ni lazima niwe la laptop, nikasema ngoja niichukue. Sasa shida yake huwa inakaa na chaji masaa 2 tu tofauti na mwanzo.

Wakat nacheki movie ghafla nikaona imejizima screen yake lakini sauti ya movie naendelea kuisikia nikajiuliza kulikoni? Haikuonyesha chochote ikabidi niizime, na kuiwasha, nikaisha ikawaka tu vizur ikaandika dell ila ghafla ikazima

Sasa ndo shida yake wakuu, ukiwasha inawaka tu vizuri ile tu unataka kuweka password ya kulog in, ghafla inazimika kioo.

Vitaa vya pembeni kwa chini vinawaka kama kawaida ila shida ni screen yake haionyeshi kitu ukiwasha inawaka tu sekunde chache, halaf inazima jee wakuu tatizo litakua nn?
 

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
5,603
9,859
Laptop ina chaji kweli? Embu weka adapter yako kwenye umeme uchomeke kwenye pc then washa
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom