Msaada: Laptop yangu imejizima baada ya kuangalia movie muda mrefu ikiwa kwenye godoro

ngosha2011

JF-Expert Member
Aug 20, 2011
681
87
PC yangu (Toshiba) nilikuwa nacheki movie huku nimeiweka kwenye godoro kwa muda mrefu, ghafla ikazima.

Nikiwasha inatoa signal kama imewaka lakini kioo hakionyezi kitu chochote na taa ya chaji inawaka kuonesha inapokea moto.

Msaada wadau..
 
Unaweza ukaua processor kwa kuiweka PC kwenye godoro kwani PC inapokuwa inatumika hupaswi kuiweka maeneo yoyote ambayo fan yake haitaweza kutoa joto ndani ya pc kwenda nje.

Unashauriwa kuweka kwenye maeneo mazuri kama juu ya meza, ikiwa joto halitatoka maana yake litabaki ndani na kuharibu processor. Hii ni moja ya onyo kuhusu utumiaji wa PC.

Hata kama hutaki kutumia ukiwa mezani ihakikishie kuwa yale matundu ya karbu na fan yanaweza kutoa hewa.

Hivyo basi, tatizo ni huenda processor imekwishakufa ndio hilo swala hutokea, lakini pia zima kabisa toa betri usiwashe kwa masaa kadhaa kisha rudishia, jaribu isipowaka nunua processor weka itawaka.

Mtu asikudanganye sijui window tatizo au HDD usijepoteza mambo muhimu ok?
 
Inategemea na saizi yake kuna 2GHZ laki na 40 nenda maduka ya accessories na hiyo pc wataangalia model sawa na pc yako nakushauri bora ununue dukani usichukue ya kishikaji utalia zaidi halafu kama hauna elimu ya kuweka processor nenda kwa awezae ila mi niko SUA MAZIMBU MOROGORO
 
Unaweza ukaua processor kwa kuiweka pc kwenye godoro kwani pc inapokuwa inatumika hupaswi kuiweka maeneo yoyote ambayo fan yake haitaweza kutoa joto ndani ya pc kwenda nje unashauriwa kuweka kwenye maeneo mazuri kama juu ya meza ikiw joto halitatoka maana yake litabaki ndani na kuharibu processor hii ni moja ya onyo kuhusu utumiaji wa pc hatakama hutaki kutumia ukiwa mezani ihakikishie kuwa yale matundu ya karbu na fan yanaweza kutoa hewa hivyo basi TATIZO NI UENDA PROCESSOR IMEKWISHA KUFA NDIO HILO SWALA HUTOKEA LAKINI PIA ZIMA KABISA TOA BETRI USIWASHEF KWA MASAA KADHAA KISHA RUDISHIA JARIBU ISIPO WAKA NUNUA PROCESSOR WEKA ITAWAKA MTU ASIKUDANGANYE SIJUI WINDOW TATIZO AU HDD USIJE POTEZA MAMBO MUHIMU OK.

si kweli kaka huwezi kuua processor kirahisi namna hio. cpu ikipata joto zaidi ya inavyotakiwa inajizima hapo hapo kuepusha uharibifu. unless hio technology iwe ya kizamani sana
 
RAM imekaa vibaya mkuu, pia usiwe unatumia Laptop wakati Processor haipati hewa nzuri.
 
Back
Top Bottom