Msaada: Laptop yangu imebrick baada ya kuinstall window 10 insider preview build 17074!

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
39,901
95,385
Natumia laptop aina ya lenovo E51 series core i5 ambayo ni mpya kwani tokea niinunue ina mwaka mmoja tu na inatumia window 10.Mimi siyo IT ila huwa napenda kupokea updates zote pamoja na upgrades zote za window 10 kwa hiyo nimeiset laptop yangu kwenye mfumo huo wa kupokea updates hizo. Jana jioni nilipata alerts kuwa build 17074 ipo hewani na laptop yangu ikaanza kudownlod na kufanya installations kama kawaida. Ilikuwa inafanya installation kama inazingua hivi kwani ilikuwa ikifika asilimia mia inaanza tena basi mimi nikaiacha inafanya hivyo nikaenda zangu kulala.

Sasa nimeamka asubuhi nikakuta imemaliza fresh na inahitaji reboot/restart ili iweze kumaliza mambo yake hayo basi nikairuhusu kufanya restarting ila ikawa inarestart mara nyingi na ikawa inanialert kuwa itafanya several restart ili iweze kumaliza.Sasa kwa sababu nilikuwa nawahi ofisini nikaifungia ndani ikiwa inafanya hizo several restart. Niliporudi jioni nikakuta imeshamaliza na iko poa kwa ajili ya matumizi. Laptop yangu nimeifunga kwa password kwa hiyo nilipofika kama kawaida nikaingiza password ili niweze kuitumia na kuona kuna lipi jipya baada ya kuinstall build 17074. Sasa kizaazaa kimeanza baada ya kuweka password,badala ya kufunguka imebaki blank huku ikiwa na mwanga mdogo sana, kwa hiyo nashindwa kuingia ndani ya laptop!!

Nimeirestart several times kwa kuzima na kuwasha kwa kutumia switch yake ya kuzima na kuwasha ila wapi!!

Wakuu tatizo linaweza kuwa nini?Nifanyeje ili niweze kuendelea kutumia laptop yangu?

Asanteni na nawakilisha!!
 
Shusha OS hiyo! Mim Habari za Update Kwenye Huwa Nazifunga Kabisa Sitak Update Yoyote Kutoka MS Laptop Yangu Ni Dell Inspiron 15 Mwaka Wa 4 Sasa Nateleza Na Win 7 Home Premium! Cjafanya Ku download Win Update Hata Mara Moja
 
mkuu hio ni update ya meltdown na spectre, intel wameonya kwamba watu wasi update kwanza.

rollback kwenye version ya zamani kwa kutumia system restore kama uliwahi au pc iliwahi kutengeneza hio point.

kwa option zaidi utazipata kwenye recovery au safe mode angalia hizi njia kuingia

7 ways to boot into Safe Mode in Windows 10 | Digital Citizen
Mkuu nashukuru sana,nimefuata hizo procedure hapo kwenye hiyo link na nimefanikiwa kurecover and finally my pc is alive again!!
 
nenda setting kisha click updates kisha insider halafu jitoe
Mkuu hakuna option ya kujitoa bali kuna options za kukatisha tamaa tu mara roll back to the first version of window 10,sijui pause for seven day only mara remove window 10!!
 
Mkuu hakuna option ya kujitoa bali kuna options za kukatisha tamaa tu mara roll back to the first version of window 10,sijui pause for seven day only mara remove window 10!!
hakuna kitu kama hiki?
stop-insider-buids-windows-10.jpg
 
windows seven is my favorist window ever! hawa windows 10 wamenisumbua sana na hizo pigo,sasa nina seven yangu wanasumbua tena nii upgrade into 10 na mimi nimekataa sitaki huo ujinga kwanza sionagi hata u special wake zaidi ya ubishololo tuu,window tamu duniani ambazo kuanzia hapo Bilgate alianza kutuzingua tuu ni window XP na window seven,zingine zote ni kupotezeana muda tuu
 
Kiukweli kutakuja na kila aina ya upgrades but I'm among the few ones ambao tutaendelea kua loyal na Win7 premium version. Nina mashaka sana na stability za hizo win 10 maana unaweza ukafanya upgrade halafu hardware yako haisupport ndio majanga yanapoanziaga .
 
Ukiclick hapo (stop insider preview build)ndo zinakuja hizo option za ajabu sasa!!
sasa hivi upo insider hivyo kutoka ni lazima urudi windows 10 ya kawaida. katika hizo option moja wapo ni ya kukurudisha kwenye windows 10 unatakiwa uclick hio.

delay-insider-builds-windows-10.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom