Yani iko nyeusi kabsa haina mwanga hata kidog na wala haineshi kama inataka kuwaka halafu inazimaJe ukiangalia kwa karibu unayaona maandishi kwa mbali? Kama maandashi yanaoneka kwa mbali sana hiyo itakuwa imeunguza circuit inayoendesha taa za screen. Hiyo circuit inaitwa display inveter au display switch.
Habari zenu.
Naomben msaada leo asubuhi nilivyoiwasha ikawaka ila haikutoa mwanga kwenye screen feni pia halizunguki...
Samahani mkuu! Naomba kuuliza, ivi bahadhi ya vifaa vya motherboard vikiharibika suluhisho lake ni kubadili vifaa vilivyoaribika ama motherboard kiujumla?Kwa kuwa hujatoa inferences za moja kwa moja acha nijaribu jibu tokana na uzoefu wangu.
Hapo sababu zaweza kuwa kama ifuatavyo:
Kama screen haiwaki kabisa na kuonesha andishi hata moja tokea mwanzo ubonyezapo power button, then matatizo yaweza kuwa ni RAM imekufa, ama LCD display imekufa
Pia umezungumzia FAN kutozunguka, hilo ni tatizo jingine. FAN kazi yake ni kufanya mzunguko wa hewa katika circuit board na kupoza vifaa vilivyomo juu yake.
Kama nilivyotajwa hapo juu i.e RAM na display ni vizima na FAN pekee ndio haiwaki then ungeona laptop inawaka kwa dakika kadhaa na kuzima ikiwa njiani kufanya booting ya O.S. Hii ni sababu joto litapanda tokana na FAN kushindwa supply hewa ya kupoza motherboard na imedesigniwa temperature ikizidi kiwango fulan laptop ijizime ili kuondoa further damage including kuungua kwa on board equipments.
Na mwisho kabisa sababu ya kutowaka yawezekana motherboard yenyewe tayari imeshaungua baaadh ya equipmens zake. Na hivyo kuifanya laptop yako kutowaka kabisa.
Nadhan 90% tatizo linaweza kuwa ndani ya nilichokielezea. Jaribu kufanya trace na unaweza vumbua tatizo linaloisibu laptop yako.