Msaada kwenye tuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada kwenye tuta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sokomoko, Oct 26, 2008.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  WanaJF napenda ufafanuzi kwa mwenye uweledi kuhusu Mfumo wa Wizara zetu. Wizara za zisizo za Muungano kule Zanzibar zipo chini ya Serikali ya Zanzibar zisizo za Muungano huku Bara zinasimamiwa na Serikali gani?
   
 2. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu wewe na muungano naona umeamua.

  This is what people are talking about, kunaonekana kama wazanzibar wamemezwa na tanganyika, hii inatokana na muundo kuwa mbaya kiasi cha kuacha maswali ambayo hayana majibu kama hilo.

  Perhaps serikali moja ingekuwa suruhisho la matatizo yote haya na zanzibar hiwe codd sawasawa na sehemu nyingine za tanzania, kwani idadi ya watu wake ni ndogo kuliko hata mkoa wa mwanza.

  Hii itapunguza matatizo ya kunyonywa na kunyonya kama tunavyoyaona, watu wa bara tunakata tujitenge kwa kuwa muungano hauna faida kwetu wakati wazanzibar wanataka wajitenge kwa kuwa muungano unawanyonya, nani ananyonywa hapa?

  Fikirieni hili swala la serikali moja kama linaweza kuwa solution nzuri muungano wetu kwani kutengana sio solution nzuri kwa kuwa naiona pemba ikiwa ni nchi nyingine zanzibar ikiwa nje ya muungano au pemba kuwa kisiwa kinachotawaliwa kimabavu na unguja.

  Hii ni kweli kabisa kwani nje ya muungano wapemba watauliza hivi unguja na pemba ziliungana lini?

  Unguja mtajibu nini?
   
 3. M

  Mama JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Hivi Mtanganyika anafaidika nini na muungano? mbona naona kama ni hasara juu ya hasara. Hivi wanavijiji wa bara wana umeme? wana maji ya bomba? Bado fedha nyingi zinahamishwa kwenda kuikimu serikali ya zanzibar; ambao wananchi wake hawaappreciate sacrifice ya hawa watanganyika wasio na umeme wala maji ya bomba hadi leo, ilhali kodi wanazotozwa kwenye ng'ombe zinaenda kuendesha serikali ingine!
   
 4. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mama I can see how busy you are! Sikutegemea hilo jibu kabisa. Anyway ukweli ni kuwa uliyozungumza ni maoni yako ninayaheshimu mie ni mtanganyika na nina intrest na Tanganyika nataka kufahamu Wizara zisizo za Muungano Bara zinasimamiwa na Serikali gani?
   
 5. M

  Mama JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Nahisi huku Tanganyika wizara hakuna isiyosimamiwa na serikali ya Muungano. Naomba mnitajie kama ipo.

  Nadhani iliyobaki ni kuua wizara zote za Zanzibar na kuacha zile za Muungano tu, ikishindikana basi kila nchi iwe na wizara zake na wizara inayohusika na masuala ya muungano ndio ibaki chini ya mwamvuli wa Muungano...worse come worse, huu muungano na uvunjwe. Ni mzigo kwa Watanganyika.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,575
  Trophy Points: 280
  Sometimes hapa JF maneno mengi. Mtu kauliza swali. Kama una jibu toa jibu halafu weka maoni yako. Kama huna jibu, sema sina jibu halafu toa maoni.

  Jibu ni muungano wetu ni muungano wa pekee na wa aina yake. Unaserikali 2. Ya Zanzibar kwa mambo yasiyo ya muungano na serikali ya Tanzania inayoshughulikia mambo yote ya muungano ambayo ndiyo ya Tanzania, Tanganyika ilikufa Aprill 26/1964.
   
 7. M

  Mama JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  ......thibitisha uswahili. Pole.
   
Loading...