Msaada kwenye tuta: Matumizi ya kifaa kinachoitwa dehumidifier kwa hapa bongo ni yapi?

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
8,575
2,000
Pamoja wakuu, naomba kufahamishwa matumizi ya dehumidifier kwa hapa bongo na kama kuna maduka yanaziuza na soko lake linakuwa linalenga watumiaji wa aina gani. Nawasilisha.
 
SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
347
500
Pamoja wakuu, naomba kufahamishwa matumizi ya dehumidifier kwa hapa bongo na kama kuna maduka yanaziuza na soko lake linakuwa linalenga watumiaji wa aina gani. Nawasilisha.
Ningekusaidia ila sijaelewa msingi wa maswali yako. Je, unataka kuziuza, na kama unataka kuziuza inakuwaje unataka kuuza kitu ambacho haujui hata kazi yake? Kifaa hicho hicho hakiwezi kuwa na matumizi tofauti kwa sababu tu kinatumika Tanzania. Funguka hasa unachotaka kufanya.
 
Kujua matumizi yake ni kwenye maeneo yepi....
 
Gibeath-Elohimu

JF-Expert Member
Jan 5, 2014
483
1,000
Kama ntakuwa sijakosea kazi ya hicho kifaa ni kuondoa unyevunyevu kwenye chumba,na mara nyingi kinatumika hasa katika vyumba ambayo uhifadhia vitu au mali zisizo hitaji unyevunyevu wa kupitiliza....niko tayari kusahihishawa kama nimetoa boko😁😁😁
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
8,575
2,000
Kama ntakuwa sijakosea kazi ya hicho kifaa ni kuondoa unyevunyevu kwenye chumba,na mara nyingi kinatumika hasa katika vyumba ambayo uhifadhia vitu au mali zisizo hitaji unyevunyevu wa kupitiliza....niko tayari kusahihishawa kama nimetoa boko😁😁😁
Mkuu upo sahihi sana, swala ni maeneo yepi hayo yasiyohitaji unyevu hasa ambayo watu hulazimika kutumia dehumidifier......maana zipo hadi za kutumia majumbani.
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
10,537
2,000
Kama ntakuwa sijakosea kazi ya hicho kifaa ni kuondoa unyevunyevu kwenye chumba,na mara nyingi kinatumika hasa katika vyumba ambayo uhifadhia vitu au mali zisizo hitaji unyevunyevu wa kupitiliza....niko tayari kusahihishawa kama nimetoa boko
Umeongea kinyume chake. Hicho kifaa kazi yake ni kunyemvusha hewa yaani kuipa hali ya umaji maji. Kazi yake inataka kufanana na ile ya feni zenye maji ambazo hufurusha maji mfano wa mvuke hivi.

Kinachofanyika ni kuwa maji yanapokuwa sprayed kwenye hewa particles zote kwenye hewa hushuka chini na particles za maji na kufanya hewa kuwa nyepesi kuvuta na kutokuwa na joto. Yaani hewa inaacha kuwa thick inakuwa nyepesi.

Ndo maana mkoa kama Dar unakiwango cha humidity kizuri joto lipo ila watu hatupauki kama ukiwa dodoma, wilayani Moshi, au mikoa mingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,334
2,000
Pamoja wakuu, naomba kufahamishwa matumizi ya dehumidifier kwa hapa bongo na kama kuna maduka yanaziuza na soko lake linakuwa linalenga watumiaji wa aina gani. Nawasilisha.
Hii kitu inakompresa na iko kama A/C inakigudulia cha kuhifadhi maji. Kazi yake ni kama unaishi sehemu yenye uyevu na ambao husababisha uvundo ukikiwasha kinapoza joto nalo linabeba unyeva, unyevu ukipata baridi huwa maji na kutiririka kwenye guduria la kuhifsdhi maji na chumba hubaki bila uvundo, nzuri kwa watu waishio mabondeni ambako sakafi na kuta huwa mbichi, hivyo huzuia kupata vichomi.
Ukipata fundi mzuri anaweza kuigeuza kuwa ya kupozea maji.
 
Mkuu umeenda chaka, msome jamaa wa juu hapo..
 
Kupozea maji unamaanisha uwe unagema yale maji yanayotuama kwenye kitenki chake kwa ajili ya matumizi? au sijakupata.......je, unaweza kuitumia hapa Dar kufyonza unyevu ndani ya chumba ukizingatia Dar kuna unyevu mwingi sana hewani (high humidity).
 
Chukua chupa ya maji iliyo ndani ya friji huwa kavu ila ukiitoa nje ya friji inaanza kumwaga maji kwenye mzunguko wake, hayo maji ni unyevu ulioko hewani hasa sehemu za joto tofauti na sehemu za baridi. Hayo maji baridi ndani ya chupa tufanye ndiyo baridi itengenezwayo na kompresa. Ukilifungua kasha la hicho kifaa utakuta bomba zimezungushwa kama koili na feni kuvuta hewa ya joto yenye unyevu ipenye kwenye koili na kupozwa, maji unayoysona hayana tofauti na yale ya kwenye A/C.
Usipoelewa hili nitaacha kuziunda nitafunga kiwanda.
 
Feb 6, 2021
60
125
Pamoja wakuu, naomba kufahamishwa matumizi ya dehumidifier kwa hapa bongo na kama kuna maduka yanaziuza na soko lake linakuwa linalenga watumiaji wa aina gani. Nawasilisha.
Hii kitu inatumika kuweka unyevu kwenye hewa hasa sehemu zinazohitaji joto la wastani ,mara nyingi nimeziona kwenye viwanda vya nguo hasa kwenye carding section ,kama unahitaji nicheki ninaweza kukusaidia zinapatikana wapi.
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
8,575
2,000
Chukua chupa ya maji iliyo ndani ya friji huwa kavu ila ukiitoa nje ya friji inaanza kumwaga maji kwenye mzunguko wake, hayo maji ni unyevu ulioko hewani hasa sehemu za joto tofauti na sehemu za baridi. Hayo maji baridi ndani ya chupa tufanye ndiyo baridi itengenezwayo na kompresa. Ukilifungua kasha la hicho kifaa utakuta bomba zimezungushwa kama koili na feni kuvuta hewa ya joto yenye unyevu ipenye kwenye koili na kupozwa, maji unayoysona hayana tofauti na yale ya kwenye A/C.
Usipoelewa hili nitaacha kuziunda nitafunga kiwanda.
Umetisha mkuu, mimi ya kwangu inatengeneza lita 5 za maji ndani ya masaa sita, napanga kwenda nayo kongwa kwa mzee ndugai maana huko nasikia maji ni shida usipime......
 
FURY BORN

JF-Expert Member
Jul 11, 2020
642
1,000
Pamoja wakuu, naomba kufahamishwa matumizi ya dehumidifier kwa hapa bongo na kama kuna maduka yanaziuza na soko lake linakuwa linalenga watumiaji wa aina gani. Nawasilisha.
Dehumidifier nikifaa kinachotumika kutoa humidity au hewa ya unyevu kwenye chumba, mara nyingi vinatumiwa sana kwenye mahotel hyaliyoko znz ili kutoa hewa ya unyevu na fungus zinazojitokeza vyumbani.
Ndicho ninachokijua, ukishawasha kinakusanya unyevu wote na ukienda kukizima unatoa maji hata lita 5
 
cool d

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
1,279
2,000
Umeongea kinyume chake. Hicho kifaa kazi yake ni kunyemvusha hewa yaani kuipa hali ya umaji maji. Kazi yake inataka kufanana na ile ya feni zenye maji ambazo hufurusha maji mfano wa mvuke hivi.

Kinachofanyika ni kuwa maji yanapokuwa sprayed kwenye hewa particles zote kwenye hewa hushuka chini na particles za maji na kufanya hewa kuwa nyepesi kuvuta na kutokuwa na joto. Yaani hewa inaacha kuwa thick inakuwa nyepesi.

Ndo maana mkoa kama Dar unakiwango cha humidity kizuri joto lipo ila watu hatupauki kama ukiwa dodoma, wilayani Moshi, au mikoa mingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ndo kinafanya hivyo basi kazi yake kitatumika pruva za mikate, maandazi sehemu za baridi maana vinakuwa haviumuki so kama anataka kuziuza ajikite sehemu zenye baridi.
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
8,575
2,000
Dehumidifier nikifaa kinachotumika kutoa humidity au hewa ya unyevu kwenye chumba, mara nyingi vinatumiwa sana kwenye mahotel hyaliyoko znz ili kutoa hewa ya unyevu na fungus zinazojitokeza vyumbani.
Ndicho ninachokijua, ukishawasha kinakusanya unyevu wote na ukienda kukizima unatoa maji hata lita 5
Wewe umedadavua vizuri sana, tena umeeleza na mahali zinapoweza kutumika....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom